Dak. David na Teresa Ferguson ilm Great Commandment resources
Kutunza Ndoa Vizuri Dak. David na Teresa Ferguson
Hakimiliki © 2000 Huduma za Maisha ya Usahibu 2000 haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya kitabu hiki kinaweza kutolewa tena au kupitishwa kwa mbinu yoyote ile au njia yoyote ile, kielektroniki au kiufundi, pamoja na nakala, rekodi au hifadhi ya habari na mifumo ya upatikanaji, bila ruhusa ya Huduma za Maisha ya Usahibu.
Yaliyomo UTANGULIZI SURA YA KWANZA Mpango wa Mungu kwa Ndoa Ukurasa wa 1 SURA YA PILI Kwa kweli tunahitaji nini kutoka kwa yule mwingine Ukurasa wa 14 SURA YA TATU Je! ni nini kinachojaza kikombe chako cha mhemko Ukurasa wa 31 SURA YA NNE Kuponya Machungu Kupitia Kukiri na Msamaha Ukurasa wa 44 SURA YA TANO Kuchanganyisha Viambatano Vinne Ukurasa wa 57 SURA YA SITA Ukoo Ukurasa wa 69 SURA YA SABA Kuwa huru kutokana na mawazo mabaya Ukurasa wa 88 SURA YA NANE Usahibu kuwa hali ya maisha Ukurasa wa 103
Shukrani Imekuwa fursa yangu kushirikiana kiinjili na wale wote ambao wamechangia vilivyo toleo hili lililosahihishwa la kitabu cha Kutunza Ndoa Vizuri, Shukrani hasa zinamwendea Tim na Eleanore Barlow, Mart na Di Westacott, John na Julie Lancaster, Jo na Susie Marriott, Julia na Keith Mills, Karen na Bernie Holford, na Stuart na Wendy Rushton. Asante kwa wale wanaotoka St Mark’s Leamington Spa ambao waliwasaidia Christine na Alister Mort katika mchakato wote wa kutoa kitabu hiki kwa Waingereza hasa Jonathan na Andy Mort, Sarah na Martyn Jackson, Paul na Heather Howell, Sarah na Andrew Lee, Gareth na Liz Callan, Katy na Terry Fermor, Amanda na Tom Di Giovanni.. Tunashukuru sana. Maharusi wengi nchini Uingereza wamepitia uhusiano ulioboreshwa na uliyofanywa upya kama matokeo ya ujumbe ambao uko kwenye kitabu hiki. Mungu aendelee kutumia njia hii kuleta umoja katika ndoa ambayo amechagua kwa heshima Yake na utukufu Wake na kwa baraka zetu. Septemba 2003 Kutunza Ndoa Vizuri David na Teresa Ferguson Dondoo zote za maandiko isipokuwa kama imeashiriwa zimetolewa kutoka kwa Biblia Takatifu, Hakimiliki ya Toleo Jipya la Kimataifa 1973, 1978, 1984, na Shirika la Kimataifa la Biblia. Zimetumiwa na ruhusa ya Nyumba ya Uchapishaji ya Zondervan. Haki zote zimeifadhiwa. Hakimiliki ni za Intimacy Press. Haki zote zimeifadhiwa.Hakuna sehemu ya kitabu hiki inaweza kutolewa tena kwa njia yoyote ile bila ruhusa ya RelationshipPress. RelationshipPress 2511 S. Lakeline Blvd., Cedar Park, TX 78613 USA www.RelationshipPress.com ISBN 0-9642845-8-8
Kutunza Ndoa Vizuri Utangulizi wa Kitabu Karibu kwa nafasi hii ya kuchukua muda wa kuzingatia juuu ya ndoa yako. Ni rahisi sana kwa sababu ya shinikizo nyingi na majukumu tunayo leo kwa muda kama huo kutopatikana mara kwa mara. Tunawashukuru kwa kujitolea ambao mnafanya sasa. Lengo letu kwako ni kwamba uhusiano wako utaimarika na matokeo yake yatakuwa kuridhika, kujali na usahibu zaidi. Mungu ana kusudi na ndoa yako. Anatamani kwamba kila mume na mke anapaswa kujua wingi wa baraka anazotoa. Tunapata katika Neno Lake kweli ambayo inaimarisha usahibu wetu na Yeye na tunapata kweli ambayo itajenga usahibu katika ndoa zetu. Anatamani kwamba tusiwe wapweke sana. Mojawapo wa utofauti wa kitabu hiki ni kwamba tutapitia mistari ya Biblia kwa pamoja ambayo itafanya Neno la Mungu katika nyumba zetu kuwa hai. Kitabu hiki kina sura au vikao vinane. Kinaweza kutumiwa na wahusika katika kozi ya vikao vinane au na maharusi kivyao. Kila sura inajumuisha nafasi yako ya kupitia yaliyoshughulikiwa katika ndoa yako mwenyewe. Kama usaidizi wa ziada, maonyesho ya video ya dakika 25 kwa kila moja ya sura nane inapatikana. Muda unaotengwa ili mzungumze pamoja ni sehemu muhimu ya kozi hii. Wakati wa Maharusi Kushiriki kila kikao na Mikutano ya Timu ya Ndoa katikati ya vikao hutoa nafasi hizo. Wale ambao wanahusika katika kozi ya Kutunza Ndoa Vizuri pamoja na wengine, pia wana nafasi ya kuuliza kufafanuliwa suala lolote linaloshughulikiwa kutoka kwa kiongozi cha maharusi. Viongozi wa kozi wako hapo ili watoe usaidizi. Ni nini kitakachoshughulikiwa? Tutakuwa tukizingatia juu ya vile tunavyoweza kujitolea. Hii ni mojawapo ya mambo ya kwanza yatakayoshughulikiwa. Kutambua kwamba hisia zile za kwanza za upendo ambazo zilikuwa zenye nguvu na nzuri wakati mwingine zinaweza kusukumwa kando na mihemko mbaya zaidi itakuwa muhimu tunapokuwa tukichunguza kikombe cha mhemko. Uwezo wa kusamehe, vizuizi vya kutaka kwetu kusamehe na umuhimu wa kuweza kukubali ubaya na kuumia katika tabia ya kukiri itashughulikiwa. Kujali, kuamini, kuhitaji na kupenda ndivyo viambatano vinne vya ndoa nzuri ambavyo vitasisitiziwa katika kitabu hiki chote na pia vimepewa kipaumbele maalum katika kikao kimoja. Kipaumbele kimepewa vikwazo tunavyokabiliana navyo wakati kuacha nyumba yetu ya utotoni na hitaji la kuweza kuomboleza na kufarijiwa kutokana na kuumizwa utotoni. Ufahamu utatolewa juu ya tabia zisizofaa tunazokuza katika mafikira yetu ambazo zinaweza kuzuia uhusiano wa karibu na maharusi wetu wa ndoa na kusababisha majibu ya kutokujua kwa njia ambazo hazisaidii na za uharibifu. Kuna vipimo vitatu vya uhusiano wetu wa ndoa, kiroho, kimhemko na kimwili na kikao cha mwisho kinaangalia kuongeza uhusiano wa karibu katika kila eneo. Kudumisha ubora Kuzoesha miili yetu mazoezi na lishe ili kuwa bora kimwili uhitaji kudumishwa kwa muda na kukuzwa mara kwa mara. Kukuwa bora kwa mwezi mmoja kwa mwaka na kurudia tabia za zamani za kutofanya mazoezi na lishe yenye mafuta mengi hakutazaa
mwili mzuri. Miezi kumi na moja ya mwaka itatoa kwa haraka matokeo yote mazuri kutoka kwa ile moja. Iliyobora kabisa ni kubadilisha mtindo wa maisha kwa inayoweza kudumishwa na lengo ambalo linaweza kufikiwa. Katika eneo la mahusiano, “Kutunza Ndoa Vizuri” hutoa nafasi kama hiyo ambayo haitoi tu malengo, bali usaidizi wa kweli wa kufikia malengo hayo ambayo yanaweza kuendelezwa kwa urahisi na vizuri katika maisha yote ya ndoa.
Page 1 Mpango wa Mungu kwa Ndoa Kukumbuka Siku Yako ya Harusi Iwe ilikuwa hivi karibuni au miaka nyingi iliyopita, siku yako ya harusi ilikuwa mwanzo wa kitengo kipya katika uhusiano wako. Ilikuwa ushahidi wa ahadi yenu na chaguo lenu la kushiriki maisha yenu yote pamoja. Kila siku ya harusi ni muhimu na ya kitofauti kabisa kiutondoti. Baada ya sharehe ya harusi, chaguo la jinsi ya kusherehekea hafla hiyo itatofautiana. Keki ya harusi na kikombe cha chai kushirikiwa na familia na marafiki wa karibu nyumbani kwa bi harusi, kachumbari baridi iliyoandaliwa kwa mtindo wa bafe ndani ya ukumbi kanisani, chakula cha jioni cha sehemu tano katika hoteli ya kifahari kwa wageni mia hivi, au mapokezi ya jioni pamoja na disko; mojawapo ya haya inawezakuwa yale uliyoyapitia. Mafikira yako yalikuwa gani asubuhi ya siku ya harusi. “Je! Tumesahau kitu chochote muhimu? Je! Sharehe itakuwa sawa?” Kila maharusi wana hadithi ya kipekee juu ya siku yao. Mawazo mengine ambayo watu wanayo wakati wako karibu kufunga ndoa yanahusu ukubwa wa hatua ambayo wanachukua. je! Kwa kweli niko tayari kuolewa? Je! Tunauhakika kwamba tutafurahiya kuwa pamoja? Kudumu na umuhimu wa kujitolea ambao kutafanywa wakati wa sharehe hiyo humaanisha kwamba nadhiri hizo haziwezi kuchukuliwa kirahisi. Maeneo Tatu ya Ndoa Nzuri Kuimarisha ndoa nzuri iliyokamili, Mungu ametukusudia sisi tukuze usahibu na maharusi wetu wa ndoa katika kila ya maeneo haya tatu: kiroho, kimhemko na kimwili. Ijapokuwa tunaweza kuwa hatujagundua, nadhiri zetu za ndoa zilionyesha mpango wa Mungu wa ndoa kwa vipimo vitatu. Kuahidi “Kupenda, Kuheshimu na Kutunza” tukitambua kwamba uhusiano wetu unahitaji usahibu wa kimhemko. “Kuwasahau wale wengine wote” huelekeza kwa uhusiano wetu wa kipekee wa kimwili na kujamiiana. “Kile ambacho Mungu amekiunganisha pamoja” ukiri kipimo cha kiroho katika uhusiano. Ili ndoa yako isitawi na iwe bora, inahitaji lishe na uangalifu katika kila moja ya maeneo haya. Hii inamaanisha kwamba, ninyi wawili mnapofanyika kuwa kitu kimoja, mnakuwa marafiki wazuri sana mnaokua pamoja katika uhusiano wa kiroho na kimhemko na uhusiano wa karibu wa kimwili. Kila moja ya vipimo hivi vitatu vinaweza kuanzishwa na kukuzwa wakati wote wa ndoa. Uhusiano wenu wa ndoa utaendelea kuwa wa karibu zaidi mnapokuwa mkishiriki kuhusu ninyi wenyewe kwa wenyewe. Mstari kutoka kwa wimbo “Tunawezaje kuwa wapenzi ikiwa hatuwezi kuwa marafiki?” unaonyesha hitaji la uhusiano wa karibu wa kimhemko pamoja na usahibu wa kujamiiana. Ya kuhuzunisha, marejeo ya mahusiano ambayo sisi huona mara kwa mara katika vyombo vya habari na kwenye runinga, huangazia uhusiano wa kimwili il hali inapuuza kukuza uhusiano wa karibu wa kimhemko au kiroho.
Page 2 Mahusiano mengine baada ya ndoa mizani yao huenda upande, wakitumia nguvu nyingi kwa kipimo kimoja tu, au viwili vya mahusiano yao. Na ni vipi kuhusu waliyofunga ndoa hivi karibuni ambao wanapendana sana na wanafurahiya uhusiano wao wa kujamiiana lakini bado wanachukua muda wao mwingi wakiwa kando na marafiki wao wa zamani? Au pengine wale ambao wanatenda kama ndugu na dada badala ya mume na mke wanaofurahiya urafiki wao lakini bila ashiki? Pia pengine maharusi wanaohusika sana na kazi ya kanisa hadi hawana muda wa kufurahiya na kujivinjari. Kwa kila mmoja wa maharusi hawa mizani yao inahitajika kushughulikiwa tena. Kitabu hiki kitawapa maharusi nafasi ya kukuza ndoa zao katika maeneo yote tatu; kimhemko, kiroho na kimwili. Kwa nini Mungu Aliumba Ndoa Je! Ni kwanini Mungu aliumba ndoa? Je! mpango Wake ulikuwa nini, kusudi Lake lilikuwa nini? Rejeleo la kwanza la ndoa linapatikana katika Mwanzo 2:24 “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.” Baada ya Mungu kuumba ulimwengu, aliangalia kila kitu alichokifanya na akaona ni chema sana. Mara sita tunasoma katika Mwanzo mlango wa kwanza kwamba “ni chema.” Adamu alifurahiya uumbaji wa ajabu, cheo kilichotukika, alikuwa bwana wa kila kitu alichoona, alifurahiya uhusiano wa karibu na Mungu. Licha ya haya yote Mungu aliona kwamba si vyema kwa Adamu kuishi peke yake. Hawa aliumbwa kuwa mke wake ili aondoe upweke wake! Mungu alituumba na mahitaji ambayo Yeye huyafikia moja kwa moja na hutamani kuyafikia kupitia mahusiano ya wanadamu ya usahibu. Kwa nini? Kwa sababu “si vyema kwa mtu awe peke yake.” Ndoa ni mojawapo ya mahusiano yaliyotolewa kiuungu ili kuondoa upweke wetu. Familia na kanisa pia ni matoleo Yake! Je! Usahibu ni nini? Kwa hakika ni nini kinachoweza kuondoa upweke? Maneno tatu ya Agano la Kale huonyesha kwa kweli asili ya usahibu ni nini: Yada – ambayo inamaanisha kujua sana. katika Zaburi 139:1-2, mtungaji anamsifu Mungu kwa kumjua sana. Kama vile Mungu anavyotujua, tunastahili kujuana katika ndoa ili tuweze kupitia usahibu. Sod – ambayo inamaanisha kufichua au kufunua . Hii inapatikana katika Mithali 3:32 “Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.” Tunapokuwa tukimjua Mungu kwa sababu yeye huchagua kujifichua kwetu, lazima tuchague kufichuana ili tuweze kujuana. Sakan – ambayo inamaanisha “kutumika, huduma, au faida.” Zaburi 139:3 inazungumzia kuhusu suala hili: “Umeelewa na njia zangu zote!” Mtungaji anatambua nia ya Mungu ya kumjua! Anasema, “Mungu, unanijua ili unilinde!” Pia lazima tuwe na motisha ya kujuana ili tuweze kujali. Kwa hivyo usahibu humaanisha kumjua mtu sana na yeye kukujua pia. Hii hufanyika wakati tunapofichua mawazo yetu ya ndani, tamaa zetu na uwoga wetu, ndoto zetu,
Page 3 malengo yetu, furaha yetu na huzuni kwa yule mwingine. Matokeo yake ni tutakua tukijali yule mwingine. Tunachagua kukubaliana na kujengana badala ya kukosoana. Tunasaidiana, kuhimizana na kuonyeshana heshima. Sis ni watu wawili tofauti ambao mara kwa mara tuna tabia tofauti kabisa ambao Mungu alitoa ndoa ili tuweze kujuana kwa upendo kwa njia hii maalum na ya usahibu. Mungu anataka tumjue na tumfurahiye kama watu, uhusiano wetu ukikua pamoja na Yeye kupitia ndoa yetu, na katika uhusiano na maharusi wetu wa ndoa. Matukio ya Maisha Yanaweza Kubadilisha Usahibu Kwa kweli ndoa hupitia vitengo vinavyoweza kubashiriwa vinavyoletwa na matukio tofauti ambayo yanaweza kujumuisha: • Siku za kwanza pamoja. • Kutulia maishani pamoja. • Mtoto wa kwanza, au kupambana na utasa. • Shinikizo la ajira/kutoajiriwa • Watoto wanaokua. • Shiniko la vijana • Watoto kutoka nyumbani. • Uwajibikaji wa wazazi wanaozeeka. • Kustaafu kwa ajira. Kwa kila moja ya vitengo hivi, vingine ambavyo vinapitana, mahusiano yatakua na kukomaa wakati changamoto mpya zinapokabiliwa. wakati mwingine shinikizo kutoka nje au wasiwasi katika familia husababisha mvuto kwa ndoa na usahibu uliyofurahiwa zamani hupotea. Mtoto akizaliwa, ugumu wa kuwa na muda wa pamoja wakati ninyi wote mna kazi ambazo zina madai na changamoto, muda uliyotumiwa mbali na nyumbani kwa safari za biashara, miaka ya ujana, jamaa, wazazi wanaozeeka, wote huunda madai ya muda na mihemko. Kwa urahisi sana maharusi wanaweza kutengana, wakiitikia madai yanayowashinikiza sana, matokeo yake ni uhusiano wao kuzingatiwa kidogo. Wakati mwingine maharusi hufikia muda wa “kiota kuwa wazi” wakati watoto wamekua na wametoka nyumbani ili kujua kwamba wanashiriki mambo machache. Urafiki katika uhusiano wao unakosa. Kwa kweli wazo la miaka ya kustaafu na kuchukua muda mwingi zaidi pamoja huonekana ya kutisha. Ndoa zinazofikia kitengo hicho hazijavunjika usiku kucha. Umomonyoko umekuwa wa pole pole, mara kwa mara haugunduliwi. Kozi ya Kutunza Ndoa Vizuri imeundwa ili kutuandaa ili tudumishe na hata pia tuimarishe usahibu wetu katika kila kitengo, kupitia kila changamoto ya maisha. Tutazingatia juu ya kuwasiliana kwa upendo na kwa kukubaliana kila wakati na kila siku ili kuongeza nguvu na kujenga uhusiano wa karibu katika uhusiano wetu wa ndoa. Kuchukua nafasi ya kuonyesha upendo wetu kupitia maneno ya shukurani itaimarisha uhusiano. Kwa urahisi tunaweza kuchukuliana kwa kawaida. Unakaribishwa kugeukiana sasa na kusema "ninafurahiya kwamba wewe ni mume/mke wangu kwa sababu ya:
Page 4 k.v. kuwajali wengine, hali ya uongozi, kutaka kujali, hekima ya kufanya uamuzi, hali ya kupenda, anavyofurahisha, anavyopendeza, kutaka kuwa na msimamo wa jambo hata kama inakuwa vigumu. Kupata nafasi za mara kwa mara za kuonyesha shukurani kwa njia hii itaongeza uhusiano wa karibu, haijalishi kitengo cha sasa cha ndoa yetu. Kukadiria Uhusiano – Je! Tuko wapi? Madhumuni ya kozi ya Kutunza Ndoa Vizuri ni kuleta maono mapya na tumaini kwa kila ndoa. Inawezekana kwa kila maharusi kupitia kipimo kikubwa cha uhusiano wa karibu katika uhusiano wao. Mungu anakusudia hivyo kwa sababu ya ndoa hatuko peke yetu. Anatualika kuwa sehemu ya kuhakikisha kwamba waume wetu au wake wetu hawako peke yao kwa kutupatia uhusiano na Yeye ili tupendane pamoja. Unahimizwa sasa kufikiria kuhusu usahibu wako katika kila moja ya vipimo hivi vitatu. • Je! kipimo cha kiroho kinahusu nini katika uhusiano wetu? Hii inaweza kujumuisha mambo kama vile kujua bwana yangu au mke wangu anapendezwa na kuhimiza kukua kwangu binafsi kiroho. Inaweza kumaanisha tunakubaliana juu ya masuala muhimu kuhusu maadili na imani. Maharusi wanaosherehekea wakati mzuri na kuonyesha shukurani kwa Mungu kwa baraka za maisha yao watapitia kipimo cha uhusiano wa karibu wa kiroho. Tunapoumizana tunaweza kukiri makosa na kusameheana. • Je! Inamaanisha nini kuwa marafiki? Kuwa wazuri kuzingatiana vikamilifu na wasikilizaji wazuri. Kuweza kushiriki hisia zetu wenyewe kwa wenyewe na kuhakikishiana na kuelewa kwamba hisia hizo ni muhimu. Kujali mahitaji ya yule mwingine. Kuwa wazuri kuambiana juu ya upendo wetu na shukurani zetu. Kuwa na kumbukumbu za ndoa yetu wakati tunashiriki mihemko nzito, zingine mbaya na zingine zenye furaha. Kuwa wazuri kujulishana mahitaji , tamaa na ndoto zetu. • Je! Inamaanisha nini kuwa na usahibu wa kimwili na mpenzi wangu wa ndoa? Tuko sawa kuwasiliana kuhusu tamaa zetu za kujamiiana na mapendeleo yetu. Tunajali na tunazingatia mahitaji ya yule mwingine wakati wa unyegereshano wa kujamiiana. Mahitaji ya kujamiiana hufikiwa na sisi wote kwa kujali. Tunaridhika na mazoea ya mara kwa mara ambayo tunaanzisha muda wa kujamiiana pamoja. Sasa chukua dakika chache kufikiria juu ya uhusiano wako. Ashiria maoni yako juu ya kiwango cha usahibu katika kila kipimo. Kila mtu akifanya kazi peke yake, weka alama kwa mizani ili ionyeshe maoni yako. Mtashiriki mawazo yako baadaye. Unaweza kuwa na maoni tofauti juu ya ndoa yako lakini lengo la kukamilisha ukadiriaji huu si kukosoa au kukemea bali kutambua maeneo yale ambayo yanaweza kuimarishwa.
Page 5 Kukadiria Usahibu Wetu wa Ndoa Kipimo cha kiroho cha uhusiano wetu ni: Usahibu Usahibu Unakosekana ni Mwingi _____________________________________________________ Je! ni hali gani ya uhusiano wetu wa kiroho ambao ungependa kuona imebadilika au imeboreshwa katika ndoa yako? Kipimo cha mhemko au urafiki cha uhusiano wetu ni: Usahibu Usahibu Unakosekana ni Mwingi _____________________________________________________
Page 6 Je! ni hali gani ya kuwa rafiki wa mpenzi wako ambao ungependa kuona imebadilika au imeboreshwa katika ndoa yako? Kipimo cha kimwili cha uhusiano wetu ni: Usahibu Usahibu Unakosekana ni Mwingi _____________________________________________________ Je! ni hali gani ya uhusiano wako wa karibu wa kimwili ambao ungependa kuona imebadilika au imeboreshwa katika ndoa yako? Upweke Unaweza Kuondolewa aje! Chukulia mawazo yafuatayo kama majibu yanayowezekana kwa swali hili. Kuimarisha Uhusiano wetu wa Kiroho. Hii inaweza kuwa eneo ngumu kwa wengi. Inakadiriwa kwamba 1 tu kati ya maharusi 10 ambao wote wawili ni Wakristo huomba pamoja. Kama hatujazoea kufanya hivyo mawazo ya kuomba pamoja yanaweza kutufanya tuhisi ugumu na vibaya. Kuomba pamoja kunaweza kuwa kwa thamana sana katika uhusiano wa ndoa. Jinsi ya kuanza kuomba pamoja Chukua muda kuzungumziana, kwa kutaja masuala muhimu ya kibinafsi. Shikaneni mikono na kisha muombe mkiwa kimya. Kubana mkono kunaweza kuwa ishara ya kwamba muda wa maombi umekwisha. Maombi ya kuzungumza yanaweza kuwa sawa kwa wengine. Kumbuka kuzingatia kitu cha shukurani kwa mpenzi wako wa ndoa. Onyesha shukurani kwa Mungu kwa ajili ya yule mwingine. Someni Biblia pamoja au msome vifungu sawa wakati wa muda wa kila mtu wa kibinafsi wa kusoma Biblia. Kusoma Mithali pamoja kwa njia hii ni pendekezo moja. Maharusi ambao wote si Wakristo wanawezaje kutarajia kupitia usahibu wa kiroho? Kwa kutaka kujadili masuala ya imani, kwa hivyo kuwa wazi kuzingatia kweli ambayo itawapeleka mbali na mhemko na mwili. Kwa uaminifu kuzingatia maswali kama vile Je! Kuna Mungu?, Je! Nina mwamini Mungu?, Je! Ukristo unaeleweka? Je! Yesu ni nani? inaweza kuwawezesha maharusi kukua katika usahibu wa kiroho. Kuimarisha Urafiki wetu Umoja wa urafiki unajumuisha kutoa muda kwa yule mwingine – hauwezi kuwa karibu na mtu ambaye hayuko. Je! ni lini ilikuwa siku yako ya mwisho uliyofurahiya kitu cha kufana kivyenu pamoja, bila familia au marafiki? Je! ni kitu gani ambacho unatarajia kufanya pamoja ili kutulia na kufurahi pamoja? Inasaidia kila wakati kuwa na tarehe
Page 7 kwenye shajara ambayo mnaweza kutazamia kama wakati ujao ambao mtachukua muda mkifanya kitu cha kutulia na cha kufurahisha pamoja. Masilahi ya Kijumla – Weka kipaumbele kwa masilahi ya yule mwingine lakini pia tazamia kufanya vitu pamoja. Pata kujua ni nini kila mmoja hupata kuwa muhimu au ya kufurahisha. Unaweza kuhusika katika masilahi ya yule mwingine lakini kama haiwezekani kwa nini msichukue masilahi mpya kwa pamoja Hisia – wakati mnapozungumza, chukua nafasi ya kuonyesha unavyohisi. Shiriki mambo mazuri na mambo ambayo si mazuri sana, furaha na hata pia hofu, maumivu na masikitiko. Kuanza kufanya hivi inaweza kuwa changamoto kwa wengi. Uhusiano mkubwa wa karibu hujengwa tunapoendelea kushiriki zaidi kuhusu mihemko tunayohisi katika maisha yetu ya kila siku. Oteni pamoja kuhusu mipango ya usoni Mahusiano mengi ya kando ya kindoa yameanza, sio kwa kuvutiwa kujamiiana, lakini na watu wawili kuweza kuzungumza pamoja kuhusu mihemko yao. Kumpata mtu mwingine ambaye mnashiriki hisia za kindani, haswa kuumwa na uchungu inaweza kuwa mwanzo wa kuhusika na uhusiano wa kujamiiana wa kando ya ndoa. Kuimarisha Uhusiano wetu wa Kimwili Kuonyeshana upendo kupitia umoja wa kujamiiana wakati kila mtu anampa raha kihisia na kila mmoja hupokea raha kwa kushukuru ni masaibu ya kitofauti kwa maharusi wowote. Lakini wakati mwingine usahibu kama huo wa kuridhisha kujamiiana haufikiwi kabisa na huwa jambo ngumu kwa maharusi kuzungumzia kuihusu. Kuzingatia tena juu ya kuongeza maonyesho ya upendo na hisia kwa yule mwingine kwa kuzungumza na kwa njia zingine inaweza kusaidia. Maneno yanayotumiwa wakati wa kuachana na kupatana tena, yanaweza kuonyesha upendo na kujenga hisia. Kwa mfano “Nitakuwa nikikufikiria leo. Ninatazamia kuwa na wewe leo usiku.’ Kuzungumziana kuhusu ndoto, malengo, uwoga, misisimko na furaha huimarisha upendo. Kuhisi kwamba mume wangu au mke wangu anapendezwa na mimi, na kile ninachofikiria kuhusu na ninavyohisi kwa wakati huu itasaidia kuunda matarajio makubwa ya usahibu wa kujamiiana. Maharusi wengi watafaidika kutokana na kiwango kinachoongezeka cha mgusano usio wa kujamiiana, kushikana mikono, kukumbatiana kirafiki, kupakatana pamoja kutazama runinga. Kupitia Warumi 12:15 Njia moja ya kuongeza umoja wa urafiki kila siku ni "Furahini pamoja nao wafurahio…" Fikiria kuhusu kumbukumbu nzuri, ya hivi karibuni au ya zamani .... tukio ambalo lilipendeza ambapo ulijihisi umependwa, umezingatiwa, mtu wa maana n.k. karamu ya siku ya kuzaliwa, krisimasi, kupokea mnyama kipenzi uliyemtaka sana, kuhusika katika mchezo wa kuigiza wa shule, mafanikio ya mchezo, shughuli inayoshirikiwa na rafiki, kufanyakazi pamoja na mzazi kwa kitu fulani......... kushiriki kumbukumbu nzuri na mpenzi wako wa ndoa.
Page 8 Mume anavyoshiriki, mke anaweza kutambua hisia ambazo anazo kwa mume wake k.v. furaha, uchangamfu, msisimko. Angalia ukurasa wa 108 kwa usaidizi wa kutambua hisia hizo. Onyesha hisia hizo kwake “ninafurahiya hiyo ilifanyika; hiyo inanifanya nijihisi ninasisimuka pia; hiyo ni nzuri.” Sasa badilishaneni majukumu. Ulihisi vipi kufurahiya pamoja? Kujibu kwa furaha kuhusu jambo nzuri ambalo yule mwingine amepitia, ni njia rahisi ambayo tunaweza kuongeza tunavyojali yule mwingine. Kushiriki kumbukumbu nzuri humaanisha tumefichua jambo zaidi kujihusu kwa yule mwingine. Ubadilishanaji huu ni mfano wa kinachohusika katika kujuana zaidi kwa kina. Tunaweza pia kulenga kutafuta, kushiriki, jambo moja nzuri kila siku ambalo lilitufanyikia. Baadaye katika kozi hii tutapitia nusu ya pili ya Warumi 12:15 tunapokuwa tukichunguza jukumu ambalo faraja inayo kwa kuongeza kujali kwetu. Wakati wa Maharusi Kushiriki Kumbuka harusi yako na uchukue muda mchache kushiriki kumbukumbu kadhaa za siku hiyo. Zungumza kuhusu kila hatua ya ndoa unayopitia kwa sasa, ukitaja mabadiliko uliyoyaona kwanzia siku za kwanza mkiwa pamoja. Unaweza kutambua shinikizo kadhaa za nje ambazo unapambana nazo sasa kwa uhusiano wako. Unahimizwa pia kufikiria kuhusu nyakati nzuri, mambo ambayo unafurahiya sana katika uhusiano wako na familia na kisha myazungumze pamoja kuyahusu. Rudi kwa Kikundi Dhiki za nje za kikazi, kusimamia fedha, na kulea familia hakustahili kuchukua nafasi ya kuwa karibu ikiwa maharusi wanafanya kazi pamoja kila wakati ili kusimamia matukio ya familia kabla ya kuzidi. Njia moja muhimu ya kukuza na kudumisha usahibu wa ndoa itakuwa kuimarisha na kuwekeza muda kwa muundo wa kuzungumziana na kushirikiana. Nyakati hizi maalum zilizowekwa kando kwa ajili ya yule mwingine zinaweza kujulikana kwa upendo kama Mikutano ya Timu ya Ndoa. Mkutano wa timu au wa wafanyikazi ofisini au sheleni kwa ujumla ni tukio lililowekwa ambalo ni muhimu sana, tukio ambalo huwekwa kwa shajara kwamba mambo mengine hayapaswi kuchukua nafasi yake. Mkutano wa timu ya ndoa unapaswa pia kupewa kipaumbele cha juu. Kuanzisha Mikutano ya Timu ya Ndoa Je! Kwa muda upi? Pendekezo la kawaida litakuwa lisali limoja hadi lisali limoja na nusu kila wiki lililowekwa kando ili maharusi wazungumze pamoja. Panga wakati – isiwe ni wakati unapopata nafasi tu! Wakati wa chakula cha mchana Ijumaa, Jumanne baada ya watoto kwenda kulala, kiamsha kinywa cha Jumamosi asubuhi. Ikiwa wakati lazima ibadilike kila wiki, panga wakati kwa utaratibu k.v. kaeni chini pamoja jioni ya Jumapili na mchague wakati mzuri kwa wiki inayokuja. Pea kipaumbele wakati huo – ifanye isiyoweza kuvunjwa kama iwezekanavyo. Desturi hiyo kila wiki ni muhimu, na manufaa ya kimhemko ya kumpatia kipaumbele yule mwingine kwa wakati huu uhimiza uhusiano wa karibu.
Page 9 Linda wakati huo – kutokana na usumbufu na vizuizi. Tafuta mahali patulivu nyumbani, au nje, bila simu au wageni ikiwezekana. Mikutano ya Timu ya Ndoa – Ajenda ya kawaida Wazo moja la kuogofya kwa maharusi wengi linaweza kuwa “Je! tunapaswa kuzungumza kuhusu nini?” Kuratibisha kalenda – kwa wiki ijayo. Je! Ni nini kinachopangwa? Je! Watoto wanafanya nini na wanahitaji kubebwa aje? Nani anayefanya kazi usiku? Ni shughuli gani za jamii zilizopangwa? Tekeleza kwa kutumia kanuni ya kukubaliana pamoja juu ya muda wa kujitolea ambao unaathiri familia kabla ya kusema ndiyo. Panga muda wako ufwatao wa kwenda nje pamoja kama maharusi na hafla ifwatayo ya familia. Jadili Malengo ya Familia- kufuatilia maendeleo na kufanya kazi pamoja. Malengo ya kila mwaka yaliyoandikwa yanaweza kuanzishwa kwa ajili ya familia na kutathminiwa ili tarehe za malengo ziwe kila muhula au kila mwezi. Je! Fedha zinaonekana kuwa zimeshikamana wiki hii na tunaweza kusaidia kivipi? Matumizi makubwa ya kaya yanayofuata yaliyopangwa ni yapi na tunawezaje kufanya kazi pamoja ili kuyatimiza? je! Tumepata marafiki wowote wapya ambao tunataka kuchukua muda nao wa kujuana vyema mwaka huu? Je! Malengo yetu ya kibinafsi yanaendelea aje .......kusoma, lishe, mazoezi, mambo tunayoyapendelea......na tunawezaje kuhimizana au kusaidiana? Mipango ya Kulea- ni vyema kupanga na kuwa kitu kimoja badala ya watoto kuwagawanya na kuwatawala. Jadili masuala muhimu ya nidhamu; kile kinachoonekana kufanya kazi na kile ambacho hakifanyi kazi? Panga nyakati za familia pamoja, pamoja na nyakati za kibinafsi za kila mtoto. Jadilianeni na mkubaliane juu ya majukumu ya kulea ya wiki ifwatayo au zaidi......k.v. ni nani anayehitaji msaada? Ni nani anayehitaji kupumzika? Ni malengo yapi yanayoonekana ya kueleweka muhula huu kwa watoto wetu katika maeneo ya nidhamu, tabia na majukumu? Tunawezaje kufanya kazi pamoja ili kuyafikia? Nyakati za Kusikiliza – mmoja au yule mwingine atahitajika kuzungumza. Kushiriki dhiki kazini au na urafiki. Kushiriki matumaini na ndoto. Kushiriki hisia na maoni kuhusu usununu wa hivi karibuni. Kushiriki shaka na uwoga kuhusu “sisi”, watoto, fedha, au maisha ya usoni. Hauwezi kubishana wakati mmoja wenu anasikiliza. Mpe usikivu wote, ufahamu, usaidizi na mwangalie kwa macho. Maonyesho Mazuri ya Mahitaji- kwa upendo kushiriki matumaini ya maisha ya usoni. Epuka misemo ya wewe na ujumla kama vile “Wewe hauchukui muda wowote na mimi!" “Kila wakati wewe huchukua upande wa watoto kinyume changu!” Tumia misemo ya mimi kwa uzuri "Nimekosa sana sisi kuwa pamoja peke yetu na ninatumaini kwamba tunaweza kwenda nje mahali tukiwa pamoja hivi karibuni." "Itamaanisha sana kwangu kama tunaweza kukubaliana mbele ya watoto na kujadili mambo yote ya kutosikilizana kwa faragha.” Shukrani – kwa vile mpenzi wako alivyo, na hata pia yale aliyoyafanya.
Page 10 Tumia mikutano yako ya kila wiki kama ukumbusho wa kuwa mume au mke wako ni baraka kwako! Wana sifa nzuri! Mifano: “Asante kwa usaidizi wa ziadi uliyotoa wiki hii na watoto." “Unavyonisalimia tunapopatana siku ikiisha inamaanisha sana kwangu wiki hii kwa kuwa kazi imekuwa ngumu sana.” Kutunza Ndoa Vizuri na Mkutano wa Timu ya Ndoa Wakati wa kozi ya Kutunza Ndoa Vizuri, Mkutano wa Timu ya Ndoa utatoa nafasi ya kupitia masuala yaliyoshughulikiwa katika vikao hivi. Chochote ambacho hautakimaliza kujadili katika Wakati wa Maharusi Kushiriki kinaweza kuendelezwa baadaye. Baada ya kozi kuisha, maharusi wengi huchagua kuangalia tena yale yaliyoshughulikiwa wakati wa kawaida wa Mikutano ya Timu ya Ndoa. Kabla ya kikao hiki cha kwanza kukamilika itakuwa muhimu kuangalia shajara ili uweke kando tarehe na muda wa Mkutano wako wa kwanza wa Timu ya Ndoa. Maombi ya Kufunga Kwa kutumia maneno sawa na haya, toa shukurani kwa Mungu mkiwa pamoja kwa ajili ya yule mwingine. Kushikana mikono unapokuwa ukiomba kunaweza kuongeza usahibu. Asante Bwana kwa mke au mume wangu wa thamani. Ninajua kwamba ni wa thamana pia kwako. Unampenda na ninakushukuru kwa kuwa ninaweza kumpenda pia. Tusaidie tukue pamoja katika umoja wa kimhemko, kiroho na kimwili. Asante Bwana.
Page 11 Mkutano wa Timu ya Ndoa Anza kwa kuonyeshana shukurani kwa kufanya muda wa kuzungumza, wa kusikilizana kwa njia hii kuwa kipaumbele. • Jadili Ukadiriaji wa Usahibu wa Ndoa uliokamilishwa katika Kikao cha Kwanza. Tunapendekeza kwamba mume aanzishe na ashiriki ukadiriaji wake katika eneo la kwanza la usahibu. Shiriki maoni au uliza maswali, ili nyinyi wote wawili mueleweke, na muelewe. Kisha mke ashiriki kwa njia hiyo. Ili kuanza, mume anaweza kushiriki eneo maalum ambalo angetaka kuona limebadilika kwake. Kisha mke anastahili kushiriki. Mifano kadhaa maluum ya aina ya mambo ambayo yanaweza kuonyeshwa:- “Ninapoangalia majibu yako katika eneo la usahibu wa kiroho, ninaona kwamba sikuhimizi vya kutosha kiroho. Ningependa sana kujifunza vile ninavyoweza kubadilisha hiyo." “Ninaona kwamba sikuambii vya kutosha jinsi ninavyokushukuru. Nitatafuta muda zaidi maalum wa kufanya hivyo." “Ninaona kwamba unakosa usikivu wangu wote. Ninataka kuwa tayari zaidi kuchukua nafasi yoyote ambayo inatokeo ili kukupa usikivu wangu wote.” Itasaidia kuangalia njia zinazofaa za kubadilika katika kila moja ya maeneo tatu ya usahibu. kimwili, kimhemko na kiroho. • Jadili vile kila mmoja wenu angependa kutumia Mkutano wa kila wiki wa Timu ya Ndoa. Kumbuka maoni tatu ya kuwa muda kama huo unahitaji kupangwa, kupewa kipaumbele na kulindwa. Utahitajika kuanza kuzungumza kuhusu ni lini na ni wapi muda kama huo utafanyika. Unaweza kuchagua kubadilisha jina la muda huo unapochukua tabia hii kibinafsi. • Unapokuwa ukimaliza Mkutano huu wa kwanza wa Timu ya Ndoa onyeshaneni shukrani kwa kuwa wazi na rahisi na kwa kujitolea kuongeza usahibu wenu wa ndoa. Unaweza pia kutaka kushirika majibu yako kwa swali lifwatalo "Nilichopata kuwa cha msaada sana kutoka kwa kikao cha kwanza ilikuwa . . . "
Page 12 Kwa Kweli Tunahitaji Nini Kutoka Kwa Yule Mwingine? Je! Unajua wimbo wa Paul Simon wa “Mimi ni mwamba”? Pengine wimbo huo hukuanzishia mawazo fulani kwako. Wale ambao wanaishi kama mwamba hawajaribu kuonyesha mhemko na hujilinda wenyewe kutokana na kupitia maumivu yoyote kwa kujaribu kufungia nje hisia. Kwa mpenzi wa ndoa hii inaweza kuleta uchungu mwingi. Ifwatayo ni mfano wa maharusi ambao wana ugumu wa kupitia usahibu. Unapozoea kwa ufupi hali hii, jiulize a) Je! Kila mtu anahitaji nini kutoka kwa yule mwingine? b) Itahitaji nini kumsaidia kila mtu kuhisi amependwa zaidi katika uhusiano wake wa ndoa? Richard na Jean Jones Mara kwa mara Richard hufanya kazi masaa 50-60 kwa wiki. Yeye hupata mshahara mzuri lakini anajihisi anaweza kufanya vyema zaidi. Amejiajiri mwenyewe katika huduma za kifedha. Richard na mke wake Jean wana watoto wawili, mvulana aliye na miaka 9 na msichana aliye na miaka 6. Wakati hafanyi kazi Richard hutoa wakati wake kwa timu ya kandanda ya mtoto wake wa kiume, ambayo husaidia kufunza. Jean hufanya kazi kwa muda maalum wakati wa masaa ya shule kama katibu. Yeye huchukua muda pia kuwapeleka watoto wote kwa shughuli na masomo tofauti. Kwa siri Jean hutamani kwamba Richard aweze kuwa tayari kupata mtoto mwingine. Ilikuwa vigumu sana kwake wakati binti wao alienda shule siku mzima. Richard si mzuri kwa kuwasiliana na Jean. Akifika nyumbani kutoka kazini au kutoka kufunza hutaka kukaa kitako mbele ya runinga. Kwa Jean anaonekana kuwa mbali na asiyeweza kufikiwa. Anataka kujua anachofikiria na anachohisi lakini hasemi mengi. Mara kwa mara hujipata akijihisi mpweke. Kuzungumza na marafiki wake si vile ilivyokuwa. Majibu ya Richard kwa Jean “Kwa nini hauzungumzi na mimi? ninashangaa kama kwa kweli unanijali!” kwa kawaida ni “sina mengi ya kusema! Mimi huchukua siku nzima nikizungumza na watu na nimezungumza vya kutosha.” Je! Unadhania Jean anahitaji nini kutoka kwa Richard? Richard anawezaje kumsaidia Jean kuhisi anapendwa zaidi au anazingatiwa zaidi? Je! Unadhania Richard anahitaji nini kutoka kwa Jean? Jean anawezaje kumsaidia Richard kuhisi anapendwa zaidi au anazingatiwa zaidi? Si Vyema kwa Mwanadamu Kuishi Peke yake Tumeona kutoka Mwanzo Mlango wa 2, kwamba Mungu alimweka Adamu katika mazingira mazuri, yaliyo na matoleo tele na katika uhusiano wa karibu na Yeye. Il hali Mungu alisema “Si vyema kwa mwanadamu kuishi peke yake”. “Haikuwa vyema” kwa sababu Adamu aliumbwa na na mahitaji ambayo Mungu aliumba yaweze kufikiwa katika mahusiano. Tunamhitaji Mungu, na tunawahitaji watu wengine! Mahitaji ni ishara ya ubinadamu wetu. Adamu alikuwa na mahitaji haya kabla ya kuanguka. Sio ishara ya dhambi zetu. Mungu alikuwa amefikia mahitaji ya Adamu ya kimwili na ya kiroho kwa wingi lakini mahitaji yake ya uhusiano yangeweza kufikiwa na mtu mwingine tu. Wakati mwingine Mungu hufikia mahitaji hayo Yeye mwenyewe moja kwa moja k.v. wakati tunapitia faraja wakati wa msiba, au amani kati ya wasiwasi.
Page 13 Mstari wa Biblia unaweza kuleta himizo wakati Mungu anapozungumzia hali yetu kuipitia moja kwa moja. Je! Unaweza kufikiria wakati Mungu alifikia mahitaji yako moja kwa moja? Walakini, Mungu pia huchagua kuwahusisha watu wengine ili kufikia mahitaji yetu ya uhusiano na kwa sababu hii Mungu alianzisha ndoa, familia na kanisa. Kati ya mahusiano haya Mungu anataka tupendane kama tulivyopendwa (John 4:11); tufariji kama tulivyofarijiwa (2 Cor 1:4) na tusamehe kama tulivyosamehewa (Ephes 4:32). Kwanza tunapokea kutoka kwa Mungu na kwa mioyo yenye shukrani tunaweza kushiriki na wengine. Ili kupitia usahibu katika ndoa, familia na kanisa, kutakuwa na utoaji na upokeaji sawa. Je! Unaweza kufikiria wakati Mungu aliwahusisha wengine kufikia mahitaji yako? Kwa wale ambao wamefunga ndoa Mungu anataka ndoa yetu iwe uhusiano msingi ambapo kuna kutoa na kupokea ili kufikia mahitaji. Mahitaji Yaliyofikiwa na Yasiyofikiwa Kati ya mahitaji yetu mengi ya kimwili kuna yale ya chakula na kulala. Ikitegemea na vile tunavyolala tunaweza kuhisi tumepumzika au tumewashwa. Ikiwa tuna chakula cha kutosha tunajihisi tumeridhika, kama hakitoshi tunakuwa wanyonge. Ikiwa mahitaji yetu msingi ya uhusiano yamefikiwa kuna kuridhika, tunahisi tunapendwa na tuko karibu. Ikiwa mahitaji hayajafikiwa kuna dhiki na tunajihisi tunakerwa, hasira na kuumia.
Page 14 Ikiwa mpenzi mmoja katika ndoa hajazingatiwa hata kidogo, hajapendwa au kupewa shukurani anaweza kuathiriwa na usununu, kukataliwa, ulipizaji kisasi, atakosa kuwasiliana na atajitenga. Inawezekana pia kwa mtu huyo kutafuta mahali pengine ili mahitaji hayo ya kimhemo yafikiwe. Hitaji haliwezi kufikiwa ikiwa mpenzi wetu halifahamu kabisa. Hii inaweza kutokea wakati mpenzi wetu anakosa kuwa mwangalifu, au hatufahamu vizuri, pia inaweza kuwa hatutaki au hatuwezi kusema hitaji letu ni lipi, au pengine kuchukua njia ya "hakuna kitu kibaya" hata unapoulizwa kwa ungwana vile tulivyo. Hitaji ambalo halijafikiwa si rahisi kuishi nalo. Wafilipi 4:19 inasema “Na Mungu wangu atawajazeni kila mchachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu." Mstari huu haufahamiki kabisa isipokuwa tukubali kwamba mahitaji yanatolewa na Mungu na ni sehemu muhimu ya utu wetu kama Mungu alivyotukusudia tuwe. Mungu anawahusisha wengine katika maisha yetu, akitupatia mahusiano ambayo tunaweza kuyatoa kwa yule mwingine. Kwa kuwa tunapokea bure kutoka kwa Mungu hivyo pia tunapeana bure. Hatutaacha kuhitaji. Kama vile mtoto hukua anapopokea upendo, anapozingatiwa, na kukubaliwa, hivyo ndivyo maisha yetu yanavyotosheleka zaidi wakati tunapojifunza kupokea na kuendelea kupokea mambo haya. Katika ulimwengu wa sasa kuna mazoea ya kuishi kana kwamba kukua hadi kukomaa ni sawa na kuongeza kujitegemea, kimhemko, kimwili na kiroho. Angalia mchoro wa Kuelewa Mahitaji ya Usahibu, ukurasa wa 28, kwa maoni zaidi kuhusu uwezo kwa maisha yetu wakati mahitaji yanapofikiwa na uchungu unaoweza kuingia maisha yetu wakati yanapopuuzwa. Mungu Anatuambia Ni sawa kuwa na mahitaji na Mungu anatuuliza tuyashughulikie kwa pamoja. Katika Ufunuo 3:17 tunasoma kwamba kanisa la Laokia, ambalo lilisema "Sina haja ya kitu" liliambiwa "hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi". Badala yake ni vyema kuwa tayari kukubali shida zetu kwa kuzungumza na kuhudumiana tukikumbuka kwamba Yesu ndiye kielelezo. Katika Mathayo 26:38 tunasoma “Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami." Yesu alikuwa akihitaji, alishiriki na marafiki wake kwamba angewataka wawe pamoja na yeye. Badala ya tabia ya kujitosheleza binafsi alionyesha marafiki wake kwamba “alikuwa masikini wa kiroho.”
Page 15 Mahitaji 10 Muhimu ya Uhusiano Ridhaa– Kuangalia zaidi ya makosa, utofauti, usumbufu ili kuona thamana. Kujitolea kusio na masharti kwa mtu ambaye hayuko kamili. Upendo – Kusalimiana kwa busu. Kusema “Ninakujali”, “niko hapa kwa ajili yako.” Kukumbatiana na kugusana kwa njia isiyo ya kujamiiana na ya kujamiiana. “Nakupenda” Kushukuru – Gundua mambo ambayo mume au mke anayofanya na ushukuru au utoe maoni. Usichukule mambo mzaha mzaha. Tafuta yaliyo mazuri badala ya kuwa tayari kudokeza makosa. Kukubali – Kutambua mambo maalum kumhusu mume au mke na kumshukuru kwa vile alivyo . Usikivu– Kuwa pamoja, kufanya mambo pamoja. Kuchukua muda wa kusikiliza, kukumbuka kuambiana kuhusu siku. masilahi bila ukosoaji. Faraja – Kuonyesha kujali kihisia wakati mpenzi anaposikitika au kuumia. Kuchukua hisia kwa uangalifu zaidi. Kuumia pamoja na kuhisi uchungu wa yule mwingine. Himizo– Kumsaidia mpenzi kuendelea wakati moyo umekwisha. Sio kukimbilia kuchukua kazi kutoka kwa mpenzi anayepambana wakati himizo linaweza kusababisha kazi hiyo kukamilika. Heshima – Kuheshimiana. Kutoonyeshana madharau mbele ya wengine. Kutumia ucheshi kihisia; kuwa tayari kuwa mkali wakati kichekesho kitaumiza na kitatumia ukosoaji. Usalama – Kujua kwamba usalama unapatikana katika uhusiano wenye nguvu, unaoweze kutegemewa na kufanya kipaumbele cha kumkumbusha mpenzi juu ya kujitolea kwako kwake kwa muda mrefu. Kufanya “mambo madogo” kila wakati . Usaidizi – Kumpatia mpenzi ujumbe wa kwamba unaweza kutegemewa wakati unahitajika. Kutambua nyakati za dhiki fulani na kutoa usaidizi. Kushiriki kazi.
Page 16 Sisi wote tunahitaji yaliyo hapo juu kwa kiwango fulani na haswa wakati fulani. Walakini kutakuwa na baadhi ya mahitaji haya ya uhusiano ambayo utafurahiya kupokea zaidi ya zingine. Unakaribishwa kuchagua mahitaji yako tatu ya juu kabisa na ukisie ni mahitaji gani 3 mpenzi wako wa ndoa anafurahiya sana kupokea. Mahitaji ya Uhusiano Mimi mwenyewe Mpenzi Ridhaa– kunipokea bila masharti; kuangalia zaidi ya makosa yangu na usumbufu wangu, kunikubali vizuri (Warumi 15:7) Upendo – wasilianeni kujali na uhusiano wa karibu kupitia mguso wa kimwili. Niambie unanipenda (Warumi 16:16) Shukrani – sema unavyonishukuru kibinafsi, gundua mafanikio yangu (1 Wakorintho 11:2) Kukubali – nisifu kwa vile nilivyo. Sema mema kunihusu kwa wengine (Waefeso 4:29) Usikivu– onyesha usikivu na usaidizi kwa matatizo yangu; ingia kwa ulimwengu wangu pamoja nami (1 Wakorintho. 12:25) Faraja – shiriki uchungu wangu kwa kuhisi uchungu huo pamoja nami, nifariji kwa unyenyekevu (warumi 12:15) Himizo – nitie moyo wa kwenda mbele vizuri; nisaidie kuvumilia nikielekea kwa lengo langu (1 Wathesalonike 5:11) Heshima – thamini mawazo yangu, heshimu maoni yangu, nionyeshe thamani yangu kwako (Warumi 12:10) Usalama – nilinde kutokana na mabaya, fuatilia upatanifu, nitie moyo wakati nimeathirika (Warumi 12:16a) Usaidizi – kuwa pamoja nami ili kunisaidia kubeba mzigo (Wagalatia 6:2)
Page 17 Sasa linganisha orodha na uandike dondoo ya mahitaji tatu ambayo umechagua pamoja na yale ambayo mpenzi wako wa ndoa amejichagulia. Mahitaji Yako Mahitaji ya Mpenzi 1. 2. 3. Unapokuwa ukilinganisha orodha gundua ni mahitaji yako ngapi ambayo yanafanana. 0 sawa 1 sawa 2 sawa 3 sawa Je! ni nini hufanyika ikiwa orodha mbili zina hitaji moja au hazina hata moja ambayo ni sawa? Kwanza kabisa hakikishiwa kwamba hii inawezekana. Tunaweza kufunga ndoa na mtu ambaye mahitaji yake ya juu ni tofauti na mahitaji yetu. Walakini kile kinachoweza kufanyika ni mazoea ya kumpa mpenzi wetu wa ndoa mambo ambayo sisi wenyewe tungependa kuyapokea. Mpenzi mmoja ana hitaji la juu la upendo na hawezi kuelewa vyema ni kwanini yule mwingine hashukuru kwa upendo mwingi ambao anatoa, wakati kwa kweli heshima inaweza kuthaminiwa zaidi. Na je kuhusu wale ambao orodha zote mbili zinafanana kabisa? Mchanganyiko huu unaweza kusababisha mahitaji kuridhishwa. Walakini kuhitaji kitu wewe mwenyewe kwa kawaida hakumaanishi unajua jinsi ya kutoa kwa wengine. Kupeana maoni ya jinsi hitaji linaweza kufikiwa vyema itasaidia. Maharusi wanaweza kushiriki hitaji sawa lakini inaweza kuwa muhimu kufikia hitaji hilo kwa njia tofauti kwa kila mpenzi. Kwa mfano “Mimi hufurahiya sana kusalimiwa mlangoni wakati ninapofika kutoka kazini. Hii hunionyesha upendo wako.” Au “Kwenda pamoja kwa matembezi mafupi jioni wakati tunaweza kuzungumza kuhusu siku yetu humaanisha sana kwangu. Mimi uhisi unanizingatia kwa njia hiyo.” Matokeo ya hitaji ambalo halijafikiwa? Kuna hatari tatu kuu kwetu sisi wakati mahitaji hayajafikiwa. 1. Uchoyo – tunatafuta kuchukua kutoka kwa wengine badala ya kutoa. Katika ndoa kila mpenzi anaweza kushughulika na mahitaji yake mwenyewe, akitafuta daima kuchukua kile anachokiona kuwa haki yake ya kuwa nacho, bila kuzingatia kutoa kwanza kwa yule mwingine. Kujichukulia hakuridhishi na uhusiano kama huo utasambaratika.
Page 18 2. Kujitegemea mwenyewe – kuamini kwamba yale yote yanayohitajika ili kuponea na kuwa na furaha yanaweza kupatikana ndani yako mwenyewe. Familia zinaweza kuhimiza kujitegemea mwenyewe na kuvunja moyo kuonyesha hisia za kweli kwa wengine. Uwezo wa kuficha hisia huonekana kana kwamba ni uadilifu. Wale ambao wamepitia uchungu mwingi katika maisha yao ya utotoni wanaweza kuwa wamejifunza kwamba ili kuponea lazima wasimwonyeshe mtu mwingine wanaumia. "Wavulana au wasichana wakubwa hawalii”. Ya kuhuzunisha, ni vigumu pia kuhisi mihemko nzuri, kuhisi umependwa na mwingine, ikiwa kujitegemea mwenyewe imekuwa kipaumbele. 3. Kujilaumu mwenyewe – kuamini kwamba kwa kweli hatuwezi kupendwa, kwamba hatuna thamani, na tunawajibikaji wa kila kitu, haswa mambo ambayo yanaenda vibaya. Mtu kama huyo ujihisi mwenye hatia kwamba ana mahitaji na hupata kuwa vigumu kupokea. Zoezi la ziada linapatikana baada ya kutambua mahitaji ya juu. Hii itakusaidia kuchunguza zaidi mahitaji inayoyahisi zaidi. Kujua mahitaji makubwa ya mpenzi wako itakuwezesha kuzungumza kuhusu vile unavyoweza kuyafikia mahitaji yao kwa njia nzuri kama iwezekanavyo. Zoezi hili linaweza kufanyika nyumbani na kujadiliwa wakati wa Mkutano wa wiki wa Timu ya Ndoa.
Page 19 Kifaa cha Kukadiria Mahitaji ya Uhusiano Maagizo: Jibu maswali haya kwa kuweka namba inayofaa kando ya kila msemo: Kabisa Sikubali Sikubali Sikubali/Sikatai Nakubali Nakubali Kabisa -2 -1 0 +1 +2 ____ 1. Ni muhimu kwamba watu wanipokee jinsi nilivyo, hata kama mimi ni “tofauti” kidogo. ____ 2. Ni muhimu kwangu kwamba ulimwengu wangu wa kifedha uwe sawa. ____ 3. Wakati mwingine “ninachoka kufanya mema." ____ 4. Ni muhimu kwangu kwamba watu wengine waniulize maoni yangu. ____ 5. Ni muhimu kwamba nikumbatiwe, ni pambajwe vizuri kimwili, n.k... ____ 6. Ninajihisi vizuri wakati mtu “anapoingia ulimwenguni mwangu.” ____ 7. Ni muhimu kwangu kujua “msimamo wangu” na wale ambao wananitawala. ____ 8. Ni muhimu wakati mtu anapogundua kwamba ninahitaji usaidizi na kisha anajitoa kuhusika. ____ 9. Nikijihisi nimezidiwa, ninataka mtu awe pamoja nami na anisaidie. ____ 10. Ninajihisi nimebarikiwa wakati mtu anapotambua na kuonyesha kujali hisia zangu. ____ 11. Napenda kujua kama “mimi ni nani” inathamani na muhimu kwa wengine. ____ 12. Ni muhimu kwangu kuonyesha—ninachofikiria, ninachohisi, n.k.—kwa wale waliyo karibu na mimi. ____ 13. Inamaanisha sana kwangu kwa mpendwa kuanza kuniambia, "ninakupenda." ____ 14. Ninakataa kuonekana kama sehemu ya kikundi kikubwa tu- uutu wangu ni muhimu. ____ 15. Ninabarikiwa wakati rafiki anapopiga simu ili kunisikiliza na kunitia moyo. ____ 16. Ni muhimu kwangu kwamba watu wanikubali si kwa yale ninayofanya bali kwa vile nilivyo. ____ 17. Ninahisi vyema kabisa wakati ulimwengu wangu uko sawa na unaweza kubashiriwa. ____ 18. Wakati nimetia bidii kwa jambo fulani, ninafurahi wakati wengine wanapoonyesha shukurani. ____ 19. Wakati “ninakosea,” ni muhimu kwangu kuhakikishiwa kwamba bado ninapendwa. ____ 20. Inanitia moyo kwamba wengine wanagundua bidii yangu au mafanikio yangu. ____ 21. Wakati mwingine ninajihisi nimezidiwa na yale yote ninayostahili kuyafanya. ____ 22. Ninataka kushughulikiwa kwa ukarimu na kwa usawa na wote, haijalishi umbari, jinsia, sura, au hali yangu. ____ 23. Ninapenda kusalimiwa kwa mikono au mguso mwingine wa kirafiki unaofaa. ____ 24. Ninapenda wakati mtu anataka kuchukua muda na mimi. ____ 25. Ninabarikiwa wakati “mkubwa” anasema, "Kazi nzuri." ____ 26. Ni muhimu kwangu kwa mtu kunionyesha ananijali baada ya kuwa na siku ngumu. ____ 27. Wakati ninapokabiliana na jambo ngumu, kwa kawaida mimi uhisi kwamba ninahitaji michango ya watu wengine na usaidizi wao. ____ 28. Dondoo zilizoandikwa na simu zikionyesha huruma baada ya kumpoteza mtu au ugumu (unaweza kuwa) muhimu kwangu. ____ 29. Ninahisi vizuri wakati mtu karibu na mimi anaponionyesha kuridhika na jinsi nilivyo. ____ 30. Ninafurahiya kuzungumziwa au kutajawa mbele ya watu wengine. ____ 31. Ninaweza kufafanuliwa kama mtu ambaye anapenda kukumbatiwa au kuguswa kwa upendo. ____ 32. Wakati uamuzi utaniathiri, ni muhimu kwangu kwamba nihusike katika uamuzi huo. ____ 33. Ninabarikiwa wakati mtu anaponionyesha kupendezwa ni kile ninachokifanya.
Page 20 ____ 34. Ninathamini vikombe, mapambo, au zawadi maalum kama makumbusho ya kudumu ya jambo muhimu nililofanya. ____ 35. Wakati mwingine nina wasiwasi kuhusu maisha ya usoni. ____ 36. Wakati ninapoletwa katika mazingira mapya, kwa kawaida mimi hutafuta kikundi cha kuungana nacho. ____ 37. Wazo la kubadilisha (kuhama, kazi mpya...n.k.) huniletea wasiwasi. ____ 38. hunisumbua wakati watu wana upendeleo dhidi ya mtu kwa sababu anavaa au anafanya vitofauti. ____ 39. Ninataka kuwa karibu na marafiki na wapendwa ambao watakuwa hapo "wakati wa ugumu." ____ 40. Mimi hubarikiwa na dondoo zilizoandikwa na maonyesho mengine maalum ya shukurani. ____ 41. Kujua kwamba mtu ananiombea ni muhimu kwangu. ____ 42. Ninakerwa na watu “wanaowaamuru” watu. ____ 43. Ninabarikiwa wakati ninapopokea maonyesho ya upendo ambayo sistahili na ya ihari. ____ 44. Ninafurahi wakati mtu anaponisikiliza kwa makini. ____ 45. Ninabarikiwa wakati watu wanaponisifu kwa tabia ya kiungu ambayo ninaonyesha. ____ 46. Kwa kawaida sitaki kuwa peke yangu wakati ninapotia maumivu na shida. ____ 47. Sifurahii kufanya mradi peke yangu; ninapendelea kuwa na mpenzi. ____ 48. Ni muhimu kwangu kujihisi “sehemu ya kikundi.” ____ 49. Mimi humjibu mtu ambaye anajaribu kunielewa na anayenionyesha ananijali kwa upendo. ____ 50. Afadhali nifanye kazi na kikundi cha watu badala ya kuwa kivyangu. Ili kuweka alama kidadisi, angalia ukurasa ufuatao.
Page 21 Kidadisi cha Mahitaji ya Uhusiano: Alama 1. Jumuisha majibu yako (-2, -1, 0, +1, +2) kwa misemo: 1 ______ 19 ______ 36 ______ 38 ______ 48 ______ Jumla _________ Majibu haya yanahusiana na hitaji la RIDHAA. 2. Jumuisha majibu yako kwa misemo: 2 ______ 17 ______ 35 ______ 37 ______ 39 ______ Jumla ________ Majibu haya yanahusiana na hitaji la USALAMA. 3. Jumuisha majibu yako kwa misemo: 18 ______ 20 ______ 25 ______ 34 ______ 40 ______ Jumla _________ Majibu haya yanahusiana na hitaji la SHUKRANI. 4. Jumuisha majibu yako kwa misemo: 3 ______ 15 ______ 21 ______ 33 ______ 41 ______ Jumla _________ Majibu haya yanahusiana na HIMIZO 5. Jumuisha majibu yako kwa misemo: 4 ______ 14 ______ 22 ______ 32 ______ 42 ______ Jumla _________ Majibu haya yanahusiana na hitaji la HESHIMA. 6. Jumuisha majibu yako kwa misemo: 5 ______ 13 ______ 23 ______ 31 ______ 43 ______ Jumla _________ Majibu haya yanahusiana na hitaji la UPENDO. 7. Jumuisha majibu yako kwa misemo: 6 ______ 12 ______ 24 ______ 30 ______ 44 ______ Jumla _________ Majibu haya yanahusiana na hitaji la USIKIVU. 8. Jumuisha majibu yako kwa misemo: 7 ______ 11 ______ 16 ______ 29 ______ 45 ______ Jumla _________ Majibu haya yanahusiana na hitaji la KUKUBALI. 9. Jumuisha majibu yako kwa misemo: 10 ______ 26 ______ 28 ______ 46 ______ 49 ______ Jumla _________ Majibu haya yanahusiana na hitaji la FARAJA. 10. Jumuisha majibu yako kwa misemo: 8 ______ 9 ______ 27 ______ 47 ______ 50 ______ Jumla _________ Majibu haya yanahusiana na hitaji la USAIDIZI. 1. Je! Jumla zako tatu za juu kabisa zilikuwa zipi? Je! Zinawakilisha mahitaji yapi? 2. Je! Jumla zako tatu za chini kabisa zilikuwa zipi? Je! Zinawakilisha mahitaji yapi? 3. Je! Jumla za juu na chini kabisa za mpenzi wako zilikuwa zipi?
Page 22 Kufikia Mahitaji Kutoa kwa yule mwingine kwa njia ambazo zinafanya kila mmoja kujihisi amependwa na anazingatiwa itakuwa muhimu sana katika kukuza furaha na kutosheka katika ndoa. Mpindukie yule mwingine na umwambie, “ninajihisi unanipenda sana wakati......" kwa mfano “unaponipigia kuniambia wakati utakuwa nyumbani”, “unaponiuliza kwanza kabla ya kufanya mipango yoyote ya kupatana na marafiki wako", "unathamini maoni yangu wakati unapochagua nguo mpya”, "unaniletea kikombe cha chai kitandani’, “unanibusu kwaheri asubuhi”, “unachukua muda wa kunisikiliza wakati ninajihisi vibaya”. Hii siyo nafasi ya kusema “ninatamani kama unge.........”, badala yake ni nafasi ya kumtia moyo mpenzi wako wa ndoa katika jambo ambalo tayari analifanya.
Page 23 Pengine unapenda kutengeneza dondoo ya njia ambazo mpenzi wako wa ndoa alionyesha anahisi unampenda na unamjali. MAALUM KUPOKEA Wakati wa Wakati wa Maharusi Kushiriki, chunguza kutoka kwa mume au mke wako ni nini ambacho angetaka sana kupokea, na uziandike chini. Unda nafasi kwa wiki chache zijazo ili kupeana. Vitu vilivyochaguliwa pia vitatoa maoni ya mahitaji yao ya juu. Orodha kama hii inavizuizi sana kwa hivyo ungetaka kuchukua muda wa kuzungumza kuhusu mambo ambayo ungetaka yaongezewe. Tia alama vitu ambavyo vinakupendeza sana kutoka kwa orodha ifwatayo.
Page 24 Chagua vitu vinne na uvitie alama katika safu ya mimi mwenyewe Mpenzi Mimi mwenyewe Kushikana mikono Kutembea pamoja Kukumbatiwa bila kutarajia Kupata dondoo ya upendo Kupokea zawadi usiyoitarajia Kuandaliwa chakula ukipendacho Kuambiwa “ninakupenda” Kusaidiwa na watoto Kukaribiwa kwa njia ya kujamiiana Kuona nyumba ikiwa safi Kukata nyasi Kupokea sifa juu ya sura yako Kuoga pamoja Hafla ya usiku usiyoitarajia Kusinga misuli ya mgongo Kula chakula cha jioni pamoja Kusifiwa kwa mafanikio Kuzungumza kwa utulivu Vitu vingine vyovyote vya ziada Hisia Nzuri Tabia nzuri Matokeo mazuri Mawazo ya Kweli Mahitaji yaliyofikiwa Usikivu Upendo Shukrani Faraja “Ninapendwa sana!” “Ninaweza kuifanya!” “Mungu ananipenda!” Kupendwa Kuzingatiwa Usalama Shukrani Ukarimu Kuwapa wengine Kujali Kufuata Ubora Familia Nzuri Mahusiano yenye kujali Imani inayokua Tabia na nafsi inayokomaaa Uwezo
Page 25 Uchungu Mahitaji ya Mahusiano Mahitaji ambayo Hayajafikiwa Mawazo yenye ‘kasoro’ Hisia za Uchungu Tabia Mbaya Matokeo Mabaya Kupuuzwa Kutokukubaliwa Kukataliwa Kukosolewa “Siwezi kuifanya” “Mi si muhimu “Nitarajibu zaidi” “Ni nini mbaya na mini?” Uchungu Hasira Hofu Lawama Nadharia ya ukamilifu “Kujifanya” “Michezo” ya hila Shughuli za kuaribu Ukatili Familia yenye mizozo Tabia mbaya Usumbufu wa nafsi Shida za kuishi Kutokomaa
Page 26 Wakati wa Maharusi Kushiriki Zungumza kuhusu majibu yako kwa wazo la kuwa unahitaji. Ikiwa ulitambua nyakati ambazo Mungu alifikia mahitaji yako moja kwa moja au kupitia wengine, yashiriki na yule mwingine. Ambianeni ni mahitaji tatu yapi ambayo ungependa sana kuyapokea. Toa maoni kadhaa ya ziada juu ya vile hitaji hilo linaweza kufikiwa. Rudi kwa sentensi iliyo kwenye ukurasa wa 25 ‘ninajihisi unanipenda sana wakati ..’ na mzungumze kuhusu njia ambazo tayari unajihisi unapendwa na kuzingatiwa. Rudi kwa Kikundi wakati wa kikao hiki unaweza kuwa umepata maoni ya kibinafsi ya mahitaji yako mwenyewe na ukaelewa ni kwanini tabia zako au matendo yako yamekuwa jinsi yalivyo. Hii pia imekuwa nafasi muhimu ya kujua ni nini haswa mume au mke wako anahitaji. Kuelewa vile tabia na mahitaji yanavyounganishwa wakati mtindo usiofaa wa tabia umekua katika ndoa itasaidia. Kuwa tayari kuangalia hitaji chini ya kitendo inaweza kusaidia kuvunja mafuatano kama hayo. Kujitolea kufikia mahitaji ya juu ya yule mwingine itaongeza usahibu wa ndoa. Maombi ya Kufunga Tunakukaribisha kushikana mikono tunapokuwa tukimshukuru Mungu kwa kutupatia mpenzi. Muulize aongeze ufahamu wako wa mahitaji ya yule mwingine. Jitoleeni mbele yake kuwa mko tayari kufanya ufikiaji mahitaji ya mwezi kuwa kipaumbele.
Page 27 MKUTANO WA TIMU YA NDOA Lengo muhimu kwa Mkutano wa Timu ya Ndoa inaweza kuwa kupangia wiki iliyombele pamoja na kuratibisha shajara. Kwa kuongezea, maoni yafuatayo yanaweza kuchukua lisali limoja. • Kwa usaidizi wa ziada wa kufafanua mahitaji tatu ambayo ni ya msaada sana kwako kupokea, kamilisha kifaa cha Kukadiria Mahitaji ya Uhusiano. Hii inaweza kudhibitisha mahitaji ambayo tayari ulikuwa umeyatambua kama kipaumbele, au inaweza kupendeza mengine tofauti. Jadili mapato hayo kwa pamoja na uamue mahitaji yako tatu ya kipaumbele, mkitoa maoni juu ya vile yanavyoweza kufikiwa vizuri. • Ulizaneni haswa vile mnavyoweza kufikia moja au zaidi ya mahitaji hayo wiki hii. Ikiwa kuna lolote ambalo hauelewi uliza ufafanuzi zaidi. Kwa mfano, “ningependa kufikia hitaji lako la himizo, lakini sina uhakika vile ninavyoweza kufanya hivyo. Je! Uko tayari kuniambia zaidi haswa kuhusu njia tofauti ninazoweza kukuhimiza?" • Wakati mahitaji hayajafikiwa, ni gani kati ya vizuizi hivi vitatu vya usahibu ambavyo umepitia; uchoyo, kujitegemea mwenyewe au kujilaumu mwenyewe. Zungumzeni zaidi kuhusu hiyo. • Ambianeni chaguo ambazo mlifanya kutoka kwa orodha ya Maalum Kupokea. Ulikuwa sahihi aje kubashiri majibu ya mpenzi wako? Ikiwa majibu ya mpenzi wako yalikushangaza, chukua muda wa kufikiria na kujadili sababu zinazowezekana za hii. Unaweza kutambua mahitaji kutoka kwa orodha ya Kumi za Juu ambayo yanaweza kufikiwa kupitia chaguo hilo maalum. Kwa mfano, kushikana mikono kunaweza kufikia hitaji la upendo, au usalama. Angalia ili uone kama pia kuna uwiano kati ya chaguo ulizojichagulia, na mahitaji tatu uliyoyachagua kama kipaumbele chako katika zoezi la hapo awali. Jitolee kuanzisha angalau chaguo moja ambalo mume/mke wako alilichagua wakati fulani wiki hii! • Shiriki majibu yako ya swali hili, Ninachohitaji sana kuweka akilini mwangu kutoka kwa kikao hiki ni . . . Wakati huu funga kwa kuomba haswa Mungu aendelee kukusaidia kuwa mume au mke ambaye anataka uwe.
Page 28 Je! Ni nini Kinachojaza Kikombe chako cha Mhemko? Wakati mahitaji yetu ya kihisia yaliyotolewa na Mungu yanapofikiwa, tunapitia usahibu; wakati mahitaji yetu yasipofikiwa, tunapitia uchungu na kupoteza. Tunaweza kuonyesha ukweli huu kama hesabu ya usahibu: Mahitaji ya Usahibu Kufikiwa= Kuhisi mtu wa maana, aliyependwana aliyezingatiwa. Lakini kuna hesabu nyingine ya usahibu ambayo ni muhimu sana: Mahitaji ya Usahibu Kutokufikiwa = Kuhisi mtu usiye wa maana, asiyependwa, asiyezingatiwa na anayeumia. Tumeona kwamba tunahisi tunapendwa na kuzingatiwa wakati mahitaji yetu yanapofikiwa, lakini hitaji ambalo halijafikiwa huleta uchungu. Katika ndoa yoyote tutapitia kutoelewana, masikitiko, uchungu, kukataliwa na kuvunjwa moyo. Mara kwa mara hii haitakuwa kwa kutaka lakini bado itasababisha huzuni, masikitiko na uchungu. Hakuna yeyote awezaye kufikia mahitaji ya mpenzi wake vikamulifu. Hauwezi kuepuka kuumia. Basi swali ni "Ni nini tunachofanya na uchungu tunaoupitia?” Zingatia picha hizi tatu. Picha ya Kwanza Ilikuwa Jumatatu jioni ya kawaida. John alikuwa amekaa sebuleni akitazama runinga. Helen alikuwa jikoni akisafisha baada ya chakula chao. Simu ikalia na John akaijibu. Helen alijua kutoka kwa mazungumzo yake kwamba lazima iwe Kevin, rafiki wa zamani wa John wakiwa shule. "Hiyo ni vizuri kuwa utakuwa eneo hili wikendi inayokuja. Kwa hakika unaweza kuja na kuishi na sisi. Helen hana shida yoyote. Ninauhakika kwamba hatakuwa na shida yoyote. Hatuna mipango yoyote ambayo haiwezi kubadilishwa na ni muda mrefu tangu nilipokuona. kwanza nitapata tikiti za mchezo wa Jumamosi jioni. itakuwa kama zamani.” Helen akamaliza kuosha. Macho yake yakiangalia bahasha iliyobandikwa kwa ubao wa matangazo. Bahasha hiyo ina tikiti za tafrija ya Jumamosi ijayo. John anajua vile ilikuwa vigumu kuzipata na alikuwa amemwahidi kumpeleka. Ilikuwa iwe wikendi ya mahaba kwa hao wawili tu. Badala ya hiyo, alijua John angeweza kupendekeza amuulize mtu mwingine aende na yeye, ili awe huru kufuatilia mechi akila chakula cha Kihindi, kama siku za zamani. Je! Helen anahisi nini wakati huu? Je! Anahitaji nini na kwanini?
Page 29 Picha ya Pili James alikuwa ametoka kazini mapema na alikuwa amefanya mipangilio maalum pamoja na kuchukua hoteli. Alikuwa akitaka wikendi hii iwe yenye makumbusho kabisa kwa mke wake na hata yeye. Ilikuwa maadhimisho ya miaka kumi ya harusi yao. Hafla ya wikendi ya James na Paula ilianza vibaya. Utabiri wa hali ya hewa ulisema kutakuwa na "mawingu machache”, lakini ikageuka kuwa mvua nyingi. Walipokuwa wakitoka njia kuu ilikuwa vigumu kuona ishara za barabarani. James akamwangalia Paula “Mpendwa, unaweza kuchukua ramani, pengine tunaweza kuihitaji? Kukerwa kwa Paula kulionekana alipokuwa akinyoosha mkono kuelekea kishubaka garini. Kwa dakika chache James alimsikia Paula akisema ifwatayo “nilidhania ulikuwa umepanga njia kabla ya kuondoka. Siwezi kuona ramani kwa mwangaza huu. Lazima tuwe tuko mbali. Ikiwa tumepotea hakuna mtu wa kuuliza njia. Daima umekuwa na hisia mbaya ya mwelekeo. Je! Gari likiharibika? Jambo kama hilo likifanyika, hatutaweza kutoka nje na kutembea na mvua hii yote. Ninakuhakikishia hoteli hii haina kitu chochote cha kufanya wakati kuna hali ya hewa ya mvua. Oh James, sidhanii tungekuja?
Page 30 Je! Unafikiria James anahisi nini wakati huu? Je! Anahitaji nini na ni kwanini? Picha ya Tatu Wakati wa kikao cha kutayarisha harusi na mtumishi wao, Tracy na Brian waliulizwa watoe habari kadhaa kuhusu usuli wa familia zao. Brian aliulizwa kwanza. "Maisha yangu ya utotoni yalikuwa mazuri na baba yangu alitoa muda mwingi kwa ajili yangu. Tulikuwa tukienda kutega samaki na tulikuwa tukienda kambini pamoja wakati wa msimu wa jua. Ninatumaini siku moja ninaweza kuwa baba wa aina hiyo kwa ............ wangu" Ghafla wakasikia tanafusi iliyosikiika kutoka kwa Tracy. Akachukua tishu na akatoa kamasi. Mtumishi akamgeukia na akasema “Tracy, ungependa kutuambia kidogo kuhusu baba yako?" Tracey akazuia machozi, na akaweza kujibu, “Baba yangu hakunizingatia hata kidogo. Kila wakati alikuwa na shughuli nyingi. Hadi sasa sijui kama ananipenda au hanipendi. Mama yangu husema ananipenda, lakini sijawahi kuhisi upendo huo. Uniumiza sana kwa sababu baba yangu ndiye mtu wa maana sana katika maisha yangu – na daima itakuwa hivyo!" Je! Ni nini unachofikiria kinaendelea kwa Brian, anapokuwa akisikiliza maoni ya Tracy kuhusu baba yake? Je! Anahisi nini? Je! Anahitaji nini wakati huu? Je! Mihemko ya Tracy ni nini?
Page 31 Je! Anahitaji nini wakati huu? Kushughulikia Uchungu wa Mhemko Wakati tunapopitia uchungu wa kimwili, kwa mfano kuchukua sufuria ambayo ilituchoma, mara moja tunafanya kitu cha kusitisha uchungu huo kuendelea; tunaweka sufuria hiyo chini! Akilini mwetu kuna eneo ambalo linaweza kulinganishwa na kikombe ndogo ambayo hushughulikia mihemko na hisia zetu. Ikiwa kikombe chetu cha mhemko kimejaa mihemko nzuri kwa sababu mahitaji yetu yamefikiwa, basi kikombe chetu kitafurika upendo, furaha na amani. Walakini, hisia mbaya zikijaza kikombe chetu zinaweza kutoa mihemko nzuri. Tunabakia tukihisi mihemko ya aina mbalimbali kama vile chuki, hasira, mwenye hatia, aibu, uwoga, wasiwasi na dhiki. Uchungu Tukio lolote la hitaji ambalo halijafikiwa huleta kiwango fulani cha uchungu, huzuni au masikitiko. Kwa kufahamu tunaweza kukosa kuhisi uchungu huo, lakini upo. Hasira Hisia za uchungu utuacha na huzuni na wanaoweza kuathiriwa na uchungu zaidi na ili kujilinda tunaweza kugeuka nje na kukasirikia wengine au kugeuka ndani na kujitenga. Kwa wengi wetu hasira ni ya moja kwa moja hadi kwa kujua hatupitii hisia za uchungu ambazo zilisababisha hasira hiyo. Hasira hutumika kama kinga dhidi ya uchungu au kupoteza zaidi. Mara kwa mara huficha mihemko kama uchungu au uwoga ambazo hutuacha tukijihisi wanyonge. Tunaona mfano wa Yesu akiwa na hasira kama matokeo ya kuwa na uchungu katika Marko 3: “Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao....” Uchungu wa Yesu na hisia zilizotokea za hasira zilikuwa dhahiri kwa njia aliyowaangalia Mafarisayo. Alijua kwamba hawakuwa na huruma kwa mtu aliyekuwa na ulemavu. Alijua pia walikuwa wakipanga kifo chake. Walakini, matendo ya Yesu ya hasira yake haikuwa kulipiza kisasi, bali kumponya mtu huyo kwa upendo. Ni njia tunayochagua kuonyesha hasira ambayo inaweza kupunguza usahibu wa mhemko katika mahusiano yetu ya karibu. Hasira ina sura nyingi ikijumuisha kutokuwa na subira, kukerwa, kukasirika haraka, uwivu, mfadhaiko, unyogovu. Hasira inaweza
Page 32 kuonyeshwa kwa njia za ujeuri zisizo na hisia – kuwa kimya, ubeuzi, kujiondoa au kuchelewa. Kukuwa tayari kuangalia kinachokua chini ya hasiri utuhimiza kwamba, tukionyesha au kupokea huduma ya uchungu basi hasira itapungua. Mithali15:1 "Jawabu la upole hugeuza hasira; bali neno liumizalo huchochea ghadhabu". Hatia Ulipizaji kisasi kwa ajili ya uchungu uliyopokea unaweza kumaanisha tunawaumiza wengine kwa kuamua kuoonyesha ukatili, ukosoaji, uzushi au kuwaacha. Wakati mwingine sisi uwaumiza wale ambao hawana uwajibikaji wa kusababisha uchungu tuliyopokea. Tunawasababishia wengine uchungu na kisha kupitia uchungu wa ziada wa kuwa wenye hatia. Tunahisi wenye hatia kwa sababu tuna hatia. Mafuatano ya mihemko mbaya inaweza kutokea tena. Ili kuvunja mafuatano hayo, inatubidi tushughulikie vilivyo hatia hiyo kwa kukiri mabaya na kuomba msamaha kutoka kwa Mungu na kutoka kwa yule tuliyemuumiza. Aibu Unaweza pia kuhisi aibu na lawama ikishambulia kujistahi na kuleta hisia za kushindwa. Tunaweza kujilaumu wenyewe visivyofaa na kuhisi tuna uwajibikaji wa uchungu tuliyopokea. Tunaweza kuhisi tunalaumiwa kama matokeo ya maoni mabaya ya kijumla ya kuumiza kutoka kwa wengine kuhusu tabia zetu au nia yetu. Kuvunjika moyo na hisia inayoongeza kila wakati ya aibu inaweza kutokea. Utofauti kati ya aibu na hatia ni, aibu haihusiani na kitendo fulani ambacho unaweza kutubu na kusamehewa. Aibu na lawama hushughulikiwa wakati tunaweza kusikia ukweli kuhusu uwajibikaji wetu kwa mambo ya kuumiza ambayo yalitufanyikia au tuliyoambiwa kwa ubaya. Mara kwa mara Mungu huwausisha wengine kuzungumza maneno hayo ya kweli kwetu sisi. Uwoga Mahitaji ambayo hayajafikiwa au vitendo vya kujua vya wengine vinaweza kusababisha uchungu, hasira na hatia na pia vinaweza kuleta uwoga. Tukiumizwa au jambo tulilofanya likosolewe na kudhihakiwa tunahisi uchungu mwingi sasa lakini pia tunaogopa kuumizwa zaidi katika maisha ya usoni. Uchungu wa jana huleta uwoga wa leo kuhusu kesho. Uwoga unaweza kuchukua maumbile tofauti. Mojawapo ni kujiondoa ili hali hizo ambazo zinaweza kuleta uchungu zaidi ziepukwe kwa njia yoyote ile. Jawabu lingine ni kuwa mwenye kuamuru watu ukiamini kwamba kuwe kwenye husukani kutapunguza uchungu wa maisha ya usoni. Uwoga unaweza kusababisha nadharia ya ukamilifu, ukiamini kwamba utendaji kazi vikamilifu utapunguza nafasi ya kuumia. Kujaribu kutojali uwoga na wasiwasi kunaweza kusababisha wengine kuzoea pombe au madawa ya kulevya.
Page 33 { { { { { Kutohisi Mhemko Mihemko nzuri Kuamuru na Tamaa Kukimbilia kazi, Madawa ya kulevya Unyogovu Kukerwa na Uhasama Shida za Kulala/Kula Malalamishi ya kimwili KIKOMBE CHA MHEMKO I Yohana 4: 18 Yohana 8:32 I Yohana 1:9 Warumi 8:1 Waefeso 4:31-32 Warumi 12:15b Mathayo 5:4 Yakobo 5:16 Lawama Hofu Uchungu / Huzuni/ Kusikitika Hatia Hasira
Page 34 Dalili za Kufurika kwa Kikombe cha Mhemko Je! Tabia zako zinaonyesha kwamba kikombe chako kinajaa mihemko yenye uchungu? Shida ya kulala - kuhisi mchovu kila wakati, hauwezi kulala Hali yenye nguvu - hofu usiokuwa na sababu, unyongovu, wasiwasi, wasiwasi usiofaa Kukosa kudhibiti hamaki – kutokuwa na subira, kukasirika virahisi Shida zinazohusishwa na kula – kula kupita kiasi/kutokula, kula polepole Kukosa nguvu – kutokuwa na uwezo wa kuzingatia, kutokuwa na uwezo wa kupewa motisha Kutokuwa na mihemko nzuri – hakuna raha tena, kutoonyesha hisia, kutokuwa na mahaba, kutoweza kutoa au kupokea upendo Dalili zingine
Page 35 Kutoa vitu kwa kikombe Tunaweza kushikilia mihemko nyingi tu. Ikiwa kikombe chetu kimejaa, mihemko mbaya inatoka wapi? Maumivu Ni vipi na ni nani ambaye nimehisi amenikwaa kwa maneno au kwa vitendo? Hasira Ni nani ninayestahili kumwepuka, kumkataa, kumkosoa, kumpuuza, au kulipiza kisasi? Uchungu Ni nane ninayemtakia mabaya, ninayenena mabaya kumhusu, sitaki niwe kama yeye? Hatia ya Kweli Ni nini nilichofanya ambacho kimewaumiza, kimewakosea au kuwakwaa wengine, au sijamwonyesha mtu mwingine heshima? Hatua ya kwanza ya kutoa mihemko mbaya inayoongezeka ndani ya kikombe chetu ni kutambua haswa kinachotuumiza. Wengi wetu hubeba uchungu mwingi wa kindoa ambao hatujawahi kujaribu kutambua. Tunajua tunaumia, lakini hatujui tufanye nini kuihusu. Ndoa nzuri hupona na kutatua uchungu, hasira, au uwoga ambao hauwezi kuepukika. Walakini wengi wetu wamejifunza kuitikia mahitaji ya mhemko kwa wengine na kwetu kwa njia ambazo si za mhemko. Tunavyofikiria, na hata pia tabia zeti zinaweza kudokeza kwamba mhemko ni batili, haufai au si muhimu. Mara kwa mara tumeanzisha mtindo wa kuitikia mhemko ambao hauzai na ambao unaongeza uchungu. Uhuru kutokana na uchungu wa kukataliwa au kuachwa unawezekana, lakini inahusisha kukubali mihemko inayohusiana na machungu hayo ili uweze kupitia uponyaji. Njia mpya za kuhusiana na sasa zitahitajika kuanzishwa. Kikao hiki kinashughulikia kuponya uchungu wa ndoa. Machungu huja pia kutoka nje ya uhusiano wa ndoa na huchangia kikombe chetu kufurika dalili mbaya. Kuwatuliza maharusi wetu wa ndoa wakati machungu yaliyopokewa kutoka kwa wengine yametambuliwa, ni jawabu la kujali na la kuponya. Hii itashughulikiwa kwa kina zaidi baadaye.
Page 36 Jinsi ya kutoa uponyaji kwa machungu niliyomsababishia mpenzi wangu wa ndoa. Hatua ya kwanza ya kuvunja mafuatano ya uchungu ni kutambua uchungu huo. Baada ya hiyo kufanywa kiri uchungu huo kwa Mungu. Kubali ilikuwa ni vibaya. Usirazinishe au kumlaumu mtu mwingine. Usidadisi hali hiyo na kuondoa uwajibikaji wako. Jaribu kuelewa uchungu huo kutoka kwa maoni ya mpenzi wako. Mpenzi wako anaweza kuwa anaumia kuhusu jambo ambalo haliwezi kukuathiri hata kidogo kwa njia hiyo moja. Ikiwa unaweza kuhisi uchungu huo, unahitaji kuihudumia. Baada ya muda ukimwomba Mungu na kupokea msamaha Wake, tubu uchungu huo kwa mume wako au mke wako na utafute msamaha wao. Ijapokuwa mara kwa mara huwa rahisi kufikiria kwanza njia ambazo tumeumizwa, anza na orodha ya njia ambazo ulimuumiza mume au mke wako. Kisha utakuwa ukikiri machungu hayo kwanza kwa Mungu na kisha kwa mume wako au mke wako. Haitafaa kwa wakati huu kushughulikia mambo ambayo mume au mke hayafahamu. Ndiposa utaratibu wa msamaha wa machungu mengine ndani ya kikombe chako uweze kuanza, utataka pia kuorodhesha njia ambazo uliumizwa. Utahitajika kufanya kazi peke yako. Unapokuwa ukiorodhesha machungu hayo, huu si wakati wa kukasirika au kuona lawama. Hakuna haja ya kuleta masuala ya zamani ambayo tayari ulikiri na kusamehewa na ambayo hausikii uchungu tenga. Orodhesha machungu kwa kutumia misemo ya hisia. k.v. “Ninahisi uchungu na nimekataliwa wakati ulipojitenga nami usiku ule kitandani” “Nilihisi sijathaminiwa wakati haukutambua nilikuwa nimeandaa chakula ukipendacho." “Nilikosa usikivu wako wakati ulipoendelea kutazama runinga na nilikuwa nikikuambia vile siku yangu ilikuwa ngumu".
Page 37 Wakati wa Maharusi Kushiriki Kwa wakati huu mkiwa pamoja mnaweza kutaka kuchunguza mihemko ya sasa ambayo kila mmoja wenu anafahamu vyema. Kwa kutumia mchoro huu wa kikombe tupu, chora laini inayowakilisha vile unavyohisi kikombe chako kimejaa mihemko mbaya. Shirikianeni hisia ambazo mnazifahamu vyema, mbaya na nzuri. Mjibiane kwa maneno ya kujali na ipasavyo. Rudi kwa Kikundi Kati ya vikao inapendekezwa kwamba msipatane kama maharusi tu, bali pia mtafute muda wa kufikiria kivyako juu ya mambo yaliyoshughulikiwa katika kikao hiki. Kutambua uchungu ndiyo sehemu ya kwanza ya njia ya kutoa vitu ndani ya kikombe cha mhemko cha uchungu wa ndoa. Chukua muda ukiwa kimya mbele ya Mungu, ukifikiria juu ya njia ulizomuumiza mpenzi wako. Andaa orodha ya kikao kinachofuata. Kumbuka kutumia ufahamu wako mpya kuhusu mahitaji ya uhusiano yaliyopewa kipaumbele ambayo mume au mke wako anayo, ili kusaidia kutambua njia ambazo unaweza kuwa umemuumizi bila kujua. Fanya kazi peke yako juu ya suala hili kabla ya kikao kifwatacho, ukitumia makaratasi yafuatayo kama kiongozi. Baada ya kufanya hivi unaweza kuhitaji kushughulikia pia machungu ya zamani. Lengo la sasa ni kukiri mbele ya Mungu. Kikao kifwatacho kinashughulikia kukiriana na msamaha. Subiri hadi kikao kifwatacho kabla ya kuzungumziana kuhusu machungu yaliyotambuliwa. Ombeni pamoja, mkimshukuru Mungu kwa kupitia msamaha na uponyaji Wake. Jitoleeni Kwake na mwombe juu ya kuwa wazi kupokea uponyaji Wake katika ndoa yenu.
Page 38 KUTAMBUA UCHUNGU - KUPONYA MACHUNGU YA MHEMKO 1 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya - tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane……” Waefeso 4 : 31-32 1a. Orodhesha njia nilizomuumiza mume/mke wangu na ndoa yetu. (tunapendekeza kutumia karatasi nyingine badala ya kitabu hiki) Mifano: kumbuka mifano ya matukio, mabishano, majibu yasiyo ya kujali yaliyo kuumiza - tumia karatasi nyingine kama inavyohitajika!) Nilikuwa mchoyo, mkosoaji/aliyeona mabaya, asiyejali, asiye na heshima, mwenye matusi, asiyesaidia, asiye na shukrani, mwenye kukataa, asiye samehea, aliyekuwa na vipaumbele mbaya, wakati .... 1b. Kiri kwa Mungu na upokee msamaha Wake. I Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye (Mungu) ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” Mfano: Mungu nimekuumiza sana pamoja na_______(mpenzi wangu) Hii ni vibaya sana na ninakuuliza unisamehe. Asante kwa msamaha wako na ninakuuliza unibadilishe niwe mtu ninayestahili kuwa. KUTAMBUA UCHUNGU - KUPONYA MACHUNGU YA MHEMKO 2 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu – tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane……” Waefeso 4:31-32 PEKE YAKO orodhesha njia nilizoumizwa na mume au mke wangu. (tunapendekeza kutumia karatasi nyingine badala ya kitabu hiki) Mifano: Kumbuka mifano ya matukio, mabishano, majibu yasiyo ya kujali yaliyo kuumiza - nilihisi; aliyekosolewa, asiyekuwa na hisia, asiye heshimiwa, anaye shambuliwa kwa maneno, asiyesaidiwa, asiyethaminiwa, aliyekataliwa, aliyeshutumiwa, asiyepewa kipaumbele wakati ...
Page 39 MKUTANO WA TIMU YA NDOA Kwa kuongezea uratibishaji wa kalenda yoyote, upangaji, utathmini lengo unalohitaji kufanya, tunapendekeza yafuatayo • Kwa kutumia mchoro wa Uwezo wa Mhemko kama rejeleo, zungumza kuhusu dalili za kufurika kwa kikombe cha mhemko ambacho kila mmoja wenu alitambua. Je! Ni zipi kati hizi ungependa kuona sana zimebadilika ndani yako? (Kwa mfano, ni vigumu kulala, ninawashwa, ninakasirika haraka.) • Taja mihemko yoyote unayopata ndani yako ambayo inaweza kuhusiana na mahusiano yale mengine? (Kwa mfano, mimi huonekana kusikia ndungu yangu wakati anapohitaji kitu tu. Nimemkasirikia mkubwa wangu kwa kutoniongeza mshahara ninaostahili.) • Kwa kukumbuka kwamba lengo la kikao hiki ni kusaidia kundoa machungu kutoka kwa kikombe cha mhemko cha mpenzi wako, onyesha mpenzi wako kwamba unatamani sana kuponya machungu ya ndoa yenu. • Sasa kivyenu tengenezeni orodha mbili za machungu ya mhemko mkitumia ukurasa wa 42 kama mwongozo. Ombeni, mkimuuliza Mungu awaonyeshe kweli kuhusu yale yanayostahili kutambuliwa kwenye orodha zote mbili. Katika kikao chetu kinachofuata, tutazingatia haswa jinsi ya kushughulikia orodha hizi zote mbili.
Page 40 Kuponya Machungu Kupitia Kufariji, Kukiri, na Msamaha Katika maisha yetu tunapitia mihemko na hisia nyingi nzuri na mbaya. Baadhi ya huzuni na masikitiko ya mapema maishani yatatolewa kutoka kwa vikombe vyetu vya mhemko kabla ya ndoa, lakini mengine yatabaki. Kikao hiki huanza kwa kushughulikia jinsi ya kuhudumia uchungu na huzuni ambao mume au mke amepitia nje ya ndoa. Kwa maneno mengine machungu ambayo hatuwajibiki. Tutachunguza uwezo wa kufariji katika kuponya machungu. Kuomboleza na Kufariji Sikiliza kinachotendeka kati ya Susan na John katika mfano huu. Itasaidia kuipitia mara mbili, ukizingatia kwanza mhemko unaotekea kati ya Susan na mama yake na kuamua athari ambayo majibu ya John yanaweza kuleta kwa mke wake. Pili, amua ni kitengo kipi ambacho majibu ya John yanaangukia. Mwishowe zingatia ni nini kinachofanya maneno ya kufariji ya John kufanya kazi. Mpangilio John na Susan wameoana kwa miaka kumi. Susan yuko karibu kupata tukio la kukasirisha kutoka kwa mama yake ambaye yuko hospitalini. Wakati Susan anaporudi nyumbani, anashiriki na John tukio hilo la mama yake. Jibu sahihi ni John kumfariji, lakini badala yake, John anatoa majibu kadhaa yasiyofaa. Mwishowe, anazungumza maneno ya kumfariji kweli. [Susan na mama yake wako hospitalini] Susan: Mama, unastahili kula! Hauwezi kuendelea kujinyima chakula Mama: Sina njaa. Susan: Mama, usiwe mgumu, kando na kutokula, mfanyakazi wa hospitali anasema umekuwa ukiishi chumbani mwako pepe yako. Unahitaji kutoka nje na kupata marafiki. Mama: Huyo mfanyakazi wa hospitali hastahili kunichunga kama mwewe. Susan: Hakuchungi kama mwewe. Anakujali na anataka uwe salama na mwenye afya. Mama: Hanijali na hata wewe haunijali! Susan: Mama! Unawezaje kusema hivyo? Mama: Ni kweli. Susan: Si kweli! Mimi huja kukuona karibu kila siku. Mama: Kwanini si kila siku? Susan: Mama, nina watoto watatu wadogo ninaowahudumia; wakati mwingine siwezi kutoka Mama: Kama nilivyosema, haujali. Susan: Mama.....! Mama: Wewe enda sasa.... rudi wakati utaweza. [Baadaye siku hiyo Susan yuko nyumbani na mume wake] Susan: John, nimekasirika sana. Nilienda kumwona mama yangu leo. Anakataa kula chakula chake, amekuwa akiwasumbua sana wafanyakazi wa hospitali, na nilipokuwa karibu kuondoka, alinishutumu kuwa simjali.
Page 41 Vitengo vya majibu Mantiki na Uwazaji Gumzo la Kusisimua Hasira Kuwa Shahidi Ushauri/Maagizo Udhalilishaji Uwoga/Wasiwasi wa kibinafsi John: Susan, nilikuambia watu wazee huwa hivyo, kama ungechukua kura ya maoni ya kila mtu ambaye ana mzazi katika hospitali hiyo wamekuwa na shida kama hizo. Mpendwa unahitaji kuangalia kweli. Ni sehemu ya mviringo wa maisha: Wazazi huzeeka na wanahitaji kuhudumiwa. Aina ya jibu? (Chagua moja kutoka kwa orodha) John: Je! Unakumbuka tulipitia shida hiyo moja na wazazi wangu. Ninaweza kukumbuka nikitatizwa na baba yangu hadi nikadhania nitamwajiri mwuguzi wa kudumu. Na baba yangu hangeweza kuingia hospitalini, alisisitiza kwamba anataka kuishi nyumbani mwake. Angalau hospitalini wanampikia mama yako vyakula, na wanapatikana wakati wa dharura. Kwa haya yote hii imekuja wakati mbaya kwangu; ninashughuli nyingi ofisini na sihitaji mzigo wa ziada wa kushughulikia mama yako. Aina ya jibu? John: Hiyo ni mbaya, lakini ulimwengu haumtegemei mama yako. Tusiichukulie kuwa kitu kikubwa; siyo jambo la pekee katika maisha yetu. Kuna mambo mengi mazuri ya kuzingatia - mechi ya kandada ya Tim iko jioni hii, hafla yetu ya wikendi inayokuja. Usiruhusu tukio hili moja kukuvunja moyo. Ulisema chakula cha jioni ni kipi? Aina ya jibu? John: Eh! Susan, hiyo ni dhihaka. Umekuwa binti mzuri kwa mama yako. Hakuna yeyote anayeweza kukushutumu kuwa haumpendi na kumjali. Wewe ni mmoja wa watu wanaojali sana ambao ninawajua. Isiruhusu ikuvunje moyo! Tumepitia wakati mgumu hapo awali na uliishughulikia vizuri! Sina shaka kwamba utafanya hivyo tena! Aina ya jibu? John: Vizuri, ni wakati wa kufanya jambo kuihusu. Tumpigie simu msimamizi wa hospitali na tupate maoni yake, ninauhakika hii siyo mara ya kwamza jambo kama hili kufanyika. Inaweza kutubidi tulalamike. Kumbuka gurudumu linalofanya kelele hupata mafuta na ikiwa unataka wamhudumie, itakubidi ulalamike. Kwa mambo ya lishe, niamini, mama yako atakula akihisi njaa ya kutosha. Pengine kubadilisha lishe inaweza kuwa vizuri.