The words you are searching are inside this book. To get more targeted content, please make full-text search by clicking here.
Discover the best professional documents and content resources in AnyFlip Document Base.
Search
Published by Relationship Press, 2023-05-31 17:10:52

Keeping Marriages Healthy in Swahili

Whole-life Discipleship

Page 42 Aina ya jibu? John: Hiyo ni habari mbaya. Tayari tulipa sana kumtunza hospitalini. Ikiwa mama yako atafika mahali pa kuhitaji mwuuguzi wa kibinafsi gharama itapanda juu. Tunawezaje kufanya hivyo na kuweza kulipa rehani yetu wenyewe? Ninashinikizwa kazini pia, sihitaji kitu kingine kinisumbue. Aina ya jibu? John: Hiyo inanikasirisha sana! Mama yako anaweza kudhibiti anachofanya. Anafanya hivyo ili aweze kusikilizwa. Anahitaji kugundua kwamba anakuumiza kwa misemo hiyo ya dhihaka. Ninajaribiwa kumpigia simu na kumwambia maoni yangu. Na kwa wasimamizi wa hospitali – niwaitia huduma za jamii kwa haraka sana, vichwa vyao vitachanganyikiwa! Aina ya jibu? John: Susan, pole sana kuwa ulipitia tukio lililokuumiza na mama yako. (John ananyoosha mkono wake na kushika mkono wa Susan.) Sipendi kukuona ukiumia. Ninajua unampenda mama yako, na ni vigumu kusikia akisema maneno kama hayo. Wakati mwingine unapoenda hospitalini wacha niende na wewe. Ningependa kukupatia usaidizi. Aina ya jibu? Ijapokuwa maneno ya kufariji ndiyo mazuri kabisa kwa John kuonyesha anamjali mke wake, maneno hayo yanaweza kusikiika kuwa tofauti na maneno ambayo tumeyazoea kuyatumia. Maneno ya kufariji mara kwa mara hayaji akilini mwetu kwa haraka kama ufafanuzi wa kimantiki, gumzo la kusisimua au jibu la "si mbaya kama unavyofikiria". Wakati wa kufariji tunatumia maneno ambayo yanazungumzia kuhusika kwa mhemko wetu na hali hiyo ya uchungu inayofafanuliwa. Inamaanisha tumeacha matatizo yetu nyuma kwa muda ili kuzingatia uchungu wa wapenzi wetu, tunaacha ulimwengu wetu nyuma na kuingia ulimwengu wao kwa pamoja. Nguvu ya kufariji katika kuponyesha uchungu hufanya istahili kustahimiliwa ili kupata maneno ambayo yanasikiika kuwa ya uaminifu na kweli yanamaanisha hata kama hii inaweza kuonekana geni wakati wa kwanza. Kumfariji Mpenzi wako Kufariji kumbukumbu za utotoni Warumi 12 :15 "..................lieni pamoja nao waliao" Fikiria kuhusu kumbukumbu inayoumiza, pengine kutoka utotoni mwako kabla ya umri wa miaka 12........, kumbukumbu ya wakati ulipojihisi mpweke, asiyependwa, asiyeeleweka, aliyekataliwa, mwoga, asiyezingatiwa.


Page 43 k.v. wakati uliaibika, wakati ulipitia kushindwa kama vile kutopata nafasi katika mchezo wa kuigiza shuleni au timu ya mchezo, mkasa wa familia, kuitwa majina, kushuhudia kitu cha kuogofya.................................................... Shiriki kumbukumbu hii isiyopendeza na hisia zako za uchungu kuihusu na mpenzi wako wa ndoa. Je! Ni hisia gani unazo kwa mpenzi wako unapokuwa ukisikia kumbukumbu hii ya uchungu unayoambiwa? (Unaweza kujipata ukiwa na hasira kuwadia mtu aliyesababisha uchungu huo. Badala yake zingatia hisia zako kwa mume/mke wako akipitia uchungu huu.) Onyesha sasa hisia zako za huzuni na maumivu kwa maneno ya kufariji kama vile “inanihuzunisha kwamba.......ninaumia kwamba....... kwa sababu ninakujali, ninakupenda. Lazima uwe ulijihisi ulikuwa peke yako. Hiyo lazima iwe ilikuumiza sana.” Sasa badilishaneni majukumu. Pengine ulisikia jambo ambalo haujawahi kulisikia tena. Pengine unafahamu vyema tukio hilo lakini umelisikia kwa njia tofauti. Kukumbuka kumbukumbu na kutulizwa hakutafanya chochote ili kubadilisha hali hiyo lakini itatoa fursa ya kuondoa upweke wako katika uchungu huo. Je! Ulihisi vipi mpenzi wako kuhisi pamoja na wewe na kwa ajili yako kwa maumivu yako? Kukiri, Msamaha, na Kufariji Uchungu wa Ndoa. Katika kila ndoa, mzozo, ugumu, na uchungu hauwezi kuepukika. Hata pia katika ndoa nzuri kabisa, waume na wake hufanya makosa, husahau vitu, hupuuza mahitaji, huwa na shughuli nyingi, au kuchukuliana kwa mzaha. Kwa kweli hakuna kitu kama ndoa kamilifu. Kwa nini? Kwa sababu ni uhusiano bayana ya watu wawili ambao si wakamilifu. I Yohana 1:8 inasema hii waziwazi na kwa kusisitiza: “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Ugumu unaweza kuwa mkubwa na mbaya, au unaweza kuwa mdogo na pengine uliyofichika, lakini swali si “je! tunaumizana?” Badala yake, swali ni “Ni lini, na ni vipi, na ni kiasi kipi tunachoumizana, na tunafanya nini kuihusu?” Kutambua uchungu ndiyo sehemu ya kwanza ya njia ya kutoa vitu ndani ya kikombe cha mhemko kilichojawa na hisia mbaya za uchungu, hasira, uwoga na hatia. Ikiwa tunaweza kuondoa mihemko hii yenye uchungu, dalili zetu nyingi zitashughulikiwa. Kufariji huponya uchungu. Hatia huondolewa kupitia kukiri. Hasira na uchungu kupitia msamaha. Kukubali Uwajibikaji Wengi wetu hupata kwamba ni rahisi zaidi kuzingatia makosa ya mtu mwingine badala ya makosa yetu wenyewe. Yesu anarejelea hii katika Mathayo 7:1-5 wakati anapouliza wawezaje kutizama kibanzi kilicho ndani ya jicho la mwingine, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe hauangalii. Kuorodhesha machungu tuliyofanyiwa inaweza kuwa rahisi sana zaidi ya


Page 44 kuorodhesha njia ambazo mpenzi ameumizwa. Hata wakati ni wazi kwamba kuna mabaya yaliyofanywa ambayo yalisababisha uchungu kwa mpenzi wetu, tunaweza kukataa kuchukua uwajibikaji wa hatua hiyo na kujaribu kujitetea au kurazinisha kilichofanyika. Jibu hili halitaleta uponyaji. Ndiposa msamaha na uponyaji ufanyike, kila mpenzi lazima agundue na ahisi uchungu wa yule mwingine. KUKIRI MACHUNGU (tunapendekeza kuandika kwa karatasi nyingine badala ya kitabu hiki) Yakobo 5:16 “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa." 1. Chagua moja kati ya machungu makubwa kutoka kwa orodha ambayo mpenzi wako anafahamu. Ninamuumiza mume/mke wangu kwa


Page 45 2. Jaribu kuangalia uchungu huu kutoka kwa maoni ya mume / mke wako. Usijitetee, kuepuka uwajibikaji au kumlaumu mume/mke wako. Ninapomuumiza mume/mke wangu kwa njia hii, pengine alihisi k.v. kuhisi vibaya, kukasirika, kuvunjika moyo, mpweke, asiyethaminiwa, asiyeheshimiwa, asiyeonekana, asiye na maana, uwoga, aliyejeruhiwa, aliyedharauliwa, aibu, aliyewachwa, aliyetumiwa.. 3. Mume/mke wako anaumia. je! Unajali? Je! Ni hisia gani unazo kwa mpenzi wako unapozingatia vile ulivyochangia uchungu wake? k.v. kuhisi vibaya, kughadhabika, kujuta, uchungu, huzuni, kukasirika, kujali sana. Ni muhimu kuhisi kitu kwa mpenzi wako. Unaweza kuwa unahisi una hatia, aibu, au hasira lakini hizi ni hisia zako au zinazokuhusu. 4. Kubali kitendo. Nilichofanya ni VIBAYA – kwisha. Ilimuuza mtu yule mwingine. Ninahitaji kusamehewa na Mungu na mpenzi wangu. Mungu anaonelea aje nilichofanya? k.v. Mungu huona kwamba siwezi kutegemewa na asiye na hisia. Ilikuwa vibaya kwamba sikuwa nyumbani za kumi na mbili wakati nilisema nitakuwa na kwamba sikupiga simu ijapokuwa ilikuwa saa moja na nusu nilipofika. Kukosa kwangu heshima kwa mtu anayempenda umuumiza Mungu – Yesu alikufa msalabani kwa maovu yangu. Kwa kweli nimemuumiza mke wangu. Anahitaji usalama. Ninapofanya hivi anahisi asiyekuwa na usalama kabisa na asiye na maana. Ninahitajika kumuuliza Mungu msamaha na mke wangu anisamehe. 5. Kukiri kunamaanisha kukubaliana na Mungu kuhusu matendo yetu mabaya. Muulize Mungu akusamehe na usome ahadi ya kutakaswa na Mungu. 1 Yohana 1:9 inasema "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote." Mshukuru kwa kukusamehe.


Page 46 Je! Ni mihemko gani unayohisi sasa? k.v. shukrani, kujawa na mhemko, kupendwa, kukubaliwa, kuthaminiwa. 6. Mwonyeshe mwenzo wako hisia zako za huzuni kwa uchungu uliosababisha. Kwa kutumia maneno kama vile "kwa kweli ninakujali na ninajali hisia zako na inanihuzunisha kwamba nimekuumiza" italeta uponyaji. 7. Unapokuwa ukikamilisha kukiri na kushiriki, maliza kukiri kwako na ombi la msamaha. Muulize mpenzi wako moja kwa moja “Je! utanisamehea?” Swahili hili linaonyesha kiwango kikubwa cha kuweza kuathirika na uvumilivu. Swahili hilo pia linatoa fursa ya kuchagua kusamehea kwa mpenzi anayesikiliza.


Page 47 MSAMAHA Wakati tunapoumizwa, lazima tuwe waangalifu tusiruhusu hisia zozote za hasira ambazo tunazo zibadilike ziwe uchungu, chuki au ulipizaji kisasi. Msamaha husaidia mpenzi aliyekosea lakini hasa yule aliyeumizwa hufaidika kwa kuwa huru kutokana na mihemko mbaya. 1. Tafuta usaidizi wa Mungu unapokuwa ukiitikia ombi la mpenzi wako la msamaha. Niliumizwa wakati 2. Je! Ni hitaji gani ambalo halikufikiwa linalohusiana na uchungu huo? Kwa kweli nilichohitaji ilikuwa


Page 48 3. Tathmini yale Mungu anayohisi kuhusu uchungu huo. Ninahisi kwamba Mungu anajali kuhusu uchungu wangu. Anajali kuhusu kilichonitendekea. Ninajua kwamba amehuzunishwa kwa sababu k.v. ananipenda, mini ni wa maana kwake na anaumia pamoja na mimi wakati ninapokosewa. Ananitakia mema 4. Chagua kusamehe. Waefeso 4:32 “...mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi". Kusamehe ni chaguo, siyo hisia. Ijapokuwa unachagua kusamehe, hautahisi kama kufanya hivyo. Kusamehe kunamaanisha “kuachilia”, “kusahau”. Ni hasira ambayo unaamua kusahau na wakati mwingine, kabla ya kuwa tayari kufanya hivyo, nafasi zaidi inahitajika kwa mpenzi wako kuelewa uzito wa uchungu wako. Msamaha lazime usiwe na masharti, kama vile msamaha wa Mungu kwetu hauna masharti. Kukubali kusamehe ikiwa ahadi imefanywa ya kutofanya hivyo tena si kukubali kusamehe bila masharti. Msamaha kama huo ni wa uwoga na sio njia ambayo Mungu utushughulikia. 5. Mwonyeshe Mungu kusamehe kwako. k.v. Bwana – niliumia wakati mume wangu alinipinga mbele ya watoto. Nilihitaji heshima yake na nilihisi uchungu na hasira nilipokosa kuipokea. Ninajua ninachostahili kusamehe. Kwa uwezo wako, na kwa jina la Yesu, ninachagua kumsamehe mume wangu kwa kutokuwa na heshima. Ninachagua kutoshikilia hasira yangu. Ninasahau. Sitamlaumu zaidi, au kutarajia airekebishe kwa njia fulani. Ninauliza faraja na uponyaji wako.


Page 49 6. Wakati unapofanya chaguo la kusamehea, mshike mpenzi wako na useme msamaha wako kwa kusema "nimekusamehe". Mpenzi wako anahitaji kusikia maneno hayo ili kumsaidia kupokea msamaha wako, kama vile unahitajika kusema ili kutia muhuri uamuzi wako wa kusamehe. Kila kiingilio kwenye orodha ya kukiri kitahitaji kuungamwa na kusamehewa. 7. Kushughulikia Machungu ya Ziada Ninyi wote mtataka sasa kuuliza “Je! Kuna machungu yoyote makubwa ambayo sijaona yanayohitaji msamaha? Tafadhali yashiriki na mimi ili niweze kuyakiri sasa na nitafute msamaha wako". 8. Baada ya kila mpenzi kutoa na kupokea msamaa, haribu orodha hiyo. Someni Yakobo 5:16 kwa pamoja. “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.” Tabia Nzuri "Jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka" Waefeso 4:26 Kukiri kwa Mungu na kwa wengine uchungu tuliyosababisha, pamoja na kuwasamehe wengine ambao wametuumiza, lazima iwe tabia ya kila siku, la sivyo Kikombe chetu cha Mhemko kitaanza kujaa tena mihemko ya uchungu. Wakati mwingine ijapokuwa kwa kweli tumemsamehe mkosaji, bado tutahisi uchungu wa ubaya tuliyotendewa. Majibu yetu kwa uchungu huo itakuwa kuchukua uwajibikaji usiofaa au wa uwongo kwa kutosamehe vilivyo, na kuhisi wenye hatia. Tunachohitaji haswa ili kupunguza uchungu huo na kuondoa uchungu huo kutoka kwa kikombe chetu ni faraja. Kwa ndoa nzuri, kukiri, msamaha na faraja ni viambatano muhimu. Kufariji uchungu wa ndoa Maneno yanastahili kusemwa kwa unyenyekevu na kwa uaminifu. Hakuna kujitetea, kurazinisha, ufafanuzi, kudhalilisha uchungu wa wengine, au kulaumu. Toni ya sauti inahitaji kuwasiliana “ Ninakujali sana na ninajali hisia zako" na "inanihuzunisha kwamba nimekuumiza". Hii husaidia kuleta uponyaji wa uchungu. k.v. Sasa ninafahamu vile kukosa kwangu kuhisi hisia zako imekuumiza wakati nisipokujulisha nitachelewa kuja nyumbani. Nimefanya hivyo mara nyingi. Nimekuwa mtu asiyehisi hisia zako. Haustahili kuwa na wasiwasi kuhusu mahali nipo na kama niko sawa. Pole sana kwa kukupitisha haya yote. Kutokuhisi kwangu na kutotegemewa kumekuumiza na kunamuumiza Mungu. Ninaona vile inavyochangia kutohisi salama – je! utanisamehe? Wakati wa Maharusi Kushiriki Tambua tukio moja jipya la wiki hii wakati ulipomkosea au kumuumiza mpenzi wako. Pengine unakumbuka ukiwa mchoyo, ukisema maneno ya ukali au kukosa kutia moyo. Kosa hili la hivi karibuni linaweza kuwa halikuumiza sana kama zile ambazo tayari umezitambua kutoka zamani, lakini ni nafasi nzuri ya kukiri na kusameheana. Pitia vitengo vyote vinavyohitajika ili msamaha utolewe na kupokewa. Tulizaneni wenyewe kwa wenyewe.


Page 50 “Nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele” Wafilipi 3:13 Zingatia kumbukumbu mpya ya msamaha. Tunapendekeza mshikane mikono mnapoomba mkimshukuru Mungu kwa kukusamehe, kwa kukubadilisha na kuponya uhusiano wenu. Hii inaweza kuwa maombi ya kimya au kwa maneno yanayosikiika, yoyote ambayo uko sawa nayo. Rudi kwa Kikundi Someni pamoja Waefeso 4:31 na 32 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu. Mkasameheane kama na Mungu katika kristo alivyowasamehe ninyi." Kufikiria juu ya machungu inaweza kuwa imeleta masuala kati yako ambayo unaweza kushukuru kuyazungumza na viongozi wa kozi. Ikiwa ni hivyo, unahimizwa kuchukua nafasi ya kupanga muda wa hii kabla ya kikao kinachofuata. Maombi Asante Mungu kwa msamaha wako na faraja. Ninajitolea kwa mpenzi wangu mbele Yako kukiri uchungu niliyosababisha, na kusamehe machungu niliyopokea, na kupeana faraja. Asante Mungu kwa kunileta karibu na mpenzi wangu kwa kuwa machungu haya, ya kujua na kutokujua, yanaponywa.


Page 51 Mkutano wa Timu ya Ndoa Kwa kuongezea uratibishaji wa kalenda yoyote, upangaji, utathmini lengo, tunatumaini kwamba wakati wa mkutano huu utakuwa ukitafuta kuponya machungu ya mhemko ambayo yanaweza kuwa yalikuwa yakijaa katika kikombe chako cha mhemko. Hii ni mojawapo ya mikutano yako muhimu sana ya timu. Ikiwa unaweza, panga karibu masaa 2 ya mfululizo. Baadi ya maongozi: • Ninyi wote mnastahili kuwa mmejiandaa kwa mkutano huu kwa kukamilisha kukiri uchungu kutoka Kikao cha 3. Kwa kutumia orodha hiyo ya njia tulizosababisha machungu hayo, inapendekezwa kwamba mume aanze utaratibu huo. Kwa kufuata maongozi yaliyotolewa kwenye taarifa, kiri kila ubaya ambao umemuumiza mume au mke. Kisha msamaha unastahili kuombwa. Mtu ambaye ameumia anastahili kusema uamuzi wa kusamehe. Hii huweka muhuri chaguo la kusamehe na humpatia mkosaji nafasi ya kupokea msamaha. • Baada ya kupitia kila uchungu uliyoorodheshwa itafaa kusema jambo kama, "Je! Kuna njia zozote ambazo nimekuumiza ambazo sijakiri hadi sasa? “Ningependa uniambia kwa sababu ninajali kwamba unaweza kuwa unaumia”. Kisha rejeleo linaweza kufanywa kwa orodha lililotengenezwa awali la machungu yaliyopokewa. Jibu na kukiri, msamaha na kufariji kwa kitu kingine chochote kilichoshirikiwa. • Funga wakati huu kwa maombi kulingana na Yakobo 5:16 kwamba Mungu aponye machungu yote.


Page 52 Kuchanganyisha Viambatano Vinne vya Usahibu wa Ndoa Kanuni za Usahibu kuwa Hali ya Maisha Ya muhimu kwa yale yote tunayoshughulikia katika kitabu hiki ni kukuza ufahamu wa mahitaji kumi ya juu zaidi ya mhemko ya mume au mke wako. Kuweza kutambua mahitaji yako mwenyewe ya juu na ya mpenzi wako ni muhimu. Tutahitajika kuuliza maswali yafuatayo kila wakati: Je! Mahitaji hayo yamebadilika siku hizi? Ninafanyaje kuyafikia mahitaji hayo vyema? Kukubali Usikivu Upendo Ridhaa Shukrani Himizo Faraja Heshima Usalama Usaidizi Kujua mahitaji ya mpenzi wetu, na kisha kutafuta njia za kuwapatia inavyostahili, ni muhimu sana. Kuhakikisha kwamba mume au mke wetu anajua kwamba tumegundua wakati hitaji limefikiwa kimakusudi pia itafaidisha ndoa yetu. Kuonyeshana shukrani wakati mahitaji yanapofikiwa ni kiitikio chema. Kuwa wazi kusikia haswa kile mume au mke alikihisi wakati wa muda wa uchungu wakati uchungu ulipitiwa, wakati mwingine umaanisha tutasikia mpenzi wetu akikadiria uchungu kuwa 10 kati ya mizani ya 1-10 wakati tunahisi 1 itakuwa kipimo cha kweli zaidi. Itamsaidia mpenzi wetu sana kutoa kipimo cha faraja kinacholingana na ukadiriaji wake wa uchungu na wala sio ukadiriaji wetu. Usahibu wa mhemko utaongezwa tunapoanza kuzoea kushiriki machungu yetu, uwoga na mawazo ya kindani kila wakati. Kama ulivyopitia muda wa kukiri na msamaha wa kikao kilichopita, inaweza kuwa mliweza kuomba kwa njia mpya. Kutambua mabaya, kuuliza msamaha na kuonyesha kutaka kubadilika ukifahamu kwamba si Mungu peke yake anayesikia, bali pia mume/mke, imefafanuliwa kama maombi yanayoathiri. Ni tofauti na kuomba kwamba Mungu ambadilishe mume/mke wako. Wakati mwingine tunatumia maombi ili kumruhusu mume au mke wetu kujua tunafikiria anahitaji kubadilika. Ni vigumu zaidi kuuliza sisi wenyewe tubadilike badala ya maharusi wetu.


Page 53 Viambatano Vinne Muhimu kwa Uhusiano wa karibu wa Ndoa Mojawapo ya uwongo ambao upo sasa kuhusu ndoa, haswa kwa kuwa mahusiano yanaendelea kuonekana kama ya muda badala ya maisha, ni hadithi ya ndoa. Husema kwamba aidha ndoa itatoboa au haitatoboa. Aidha mnaendana au hamwendani. Hadithi hiyo inasema upendo unapaswa kuwa wa ihari na kama hauna hisia za mahaba tena, basi unastahili kutambua imekwisha na pengine unapaswa kumtafuta mtu mwingine ambaye unahisia zake. Uchungu mwingi umetokea kwa wale ambao wamejaribu kukubali hadithi hiyo. Usahibu hautokei tu – unahitaji kufikiria na bidii. Kweli kwamba huchukua jitihada si ishara ya kwamba hii ni ndoa mbaya au inayosambaratika. Kweli ni kwamba ndoa nzuri kabisa ni zile ambazo zina wakati na usikivu, k.v., zile ambazo zinashughulikiwa kila mara. Upande mmoja wa kufanyia kazi ndoa yetu nzuri ni kuchanganya viambatano vinne vya uhusiano wa karibu. 1) Kujali kwa upendo Kujali kwa upendo ni kusema “ninakujali”. Kujali kunajumuisha kumhakikishia mpenzi wako na kumwonyesha upendo, kujali na kusikiliza. Unaonyesha unajali kuhusu mpenzi wako wakati unapomsikiliza vikamilifu wakati anapozungumza, unafanya kumpa upendo kuwa kipaumbele, kuahidi kumwombea mpenzi wako wakati anakabiliwa na Yesu alionyesha umbo la upendo wake wakati "Alipotia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu". Yohana 13:5 Tunasoma katika 1 Petro 5:7 “Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu". Uhusiano usio na kujali utaharibika. Machungu yataongezeka. Kujua vile mpenzi wetu anavyohisi anajaliwa, kinachomfanya ajihisi anapendwa, itatusaidia kuhakikisha hayo ndiyo wanayopokea kutoka kwetu. Maonyesho rahisi sana yanaweza kuwa ya maana sana lakini yanaweza kusahaulika kwa urahisi. Lengo letu linapaswa kuwa kuwajali wapenzi wetu kwa njia ambazo wanafurahiya hata kama njia hizo sio zile tunazopendelea. Fikiria kuhusu uhusiano wako na ukamilishe yafuatayo Ninahisi unanijali wakati na hata pia wakati Kuweza kuonyesha kujaliana kunaweza kuzuiliwa na hasira, uchungu au chuki. Hizi zinaweza kuzuia tunavyomjali mume au mke wetu. Hisia zangu za kukujali zimezuiliwa na


Page 54 k.v. hasira wakati unashuku nia yangu, kuwa na uchungu wakati hauonyeshi shukrani kwa maonyesho yangu ya kujali, chuki wakati unapodharau maonyesho yangu ya kujali. Vizuizi hivi vinaashiria uchungu ambao haujapona. Kujali kwa upendo kunajumuisha mihemko nzuri – kuwa dhahiri kuhusu mambo tunayoyapenda kuhusu yule mwingine, kuwa na furaha kuhusu ndoa, kushukuru kwa sababu ya mpenzi wetu. Kuna nafasi ndogo ya mihemko nzuri wakati kikombe chetu cha mhemko kimejaa uchungu na hasira. Mchakato wa kukiri, msamaha, na faraja utaponya uchungu na kuacha nafasi ya kujali kwa upendo. Tunakumbushwa hapa juu ya umuhimu wa kuondoa vitu ndani ya kikombe hicho kila wakati. 2) Mawasiliano yanayoathiri husema "Ninakuamini" Je! Ni nini unachokitafuta sana kwa rafiki? Wengi wenu mtakuwa na wazo la imani. Hii ni sifa nzuri. Wakati tunapoamini tunahatarisha kuwa wazi kuhusu hisia, mahitaji na machungu yetu. Unaweza kuonyesha imani kwa mpenzi wako wakati mnaposhiriki hisia kuhusu shida za kikazi, kushiriki matumaini na ndoto zako, kumwambia kinachofurahisha (au kisichofurahisha) wakati wenu wa kujamiiana. Yesu alionyesha kwamba aliwaamini wanafunzi wake kama tunavyosoma katika Yohana 15:15 "Lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.” Mawasiliano yanayoathiri yanaweza kuonyesha, “Ninakuthamini”. Inatoa ruhusa ya kuzungumza kuhusu mambo magumu sana ya kibinafsi bila ya uwoga wa kudhihakiwa au wa kutojaliwa. Kumwamini mtu mwingine humaanisha kishiriki badala ya kuficha hisia. Fikiria kuhusu uhusiano wako na mpenzi wako na ukamilishe ifwatayo: Ninaweza kuwa wazi zaidi na mpenzi wangu kuhusu


Page 55 k,v, uwoga wa kuwa sifanyi vyema kazini, wasiwasi kwamba sipendezi, hofu kuhusu vile watoto wangu wanaathariwa na mimi kutokuwa na tamaa ya kula. Mimi na mpenzi wangu tunaweza kudhuriwa zaidi kwa kushiriki k..v. kuhusu ugumu ninao wa kuitikia kingono baada ya mume/mke wangu kusema mambo fulani, uchungu ninaohisi wakati hatushirikiani kufanya kazi za kinyumbani, upweke wangu hata wakati tuko pamoja. Uwoga ni kizuizi cha imani. Fikiria kuhusu uwoga ambao umekuzuia kuwa wazi na unaokudhuru na mpenzi wako. Wakati mwingine nimekuwa wazi au kudhuriwa na hisia zangu au mahitaji kwa sababu ninaogopa k.v. mume/mke wangu atanichekelea, ninaonekana mnyonge au mjinga, mpenzi wangu atasikia vibaya, mume/mke wangu ataisikia kama ukosoaji tu na kujibu kwa hasira. Kujali uwoga wa mpenzi wangu wa ndoa Ni upendo ambao unatoa uwoga. Tunaweza kuhudumia uwoga wa mpenzi wetu kwa kumwahakikishia upendo wetu. Kujali kwa upendo ndio msingi ambao mawasiliano ya kuadhiri yanaweza kujengwa. Nikihisi unanijali, nitaweza kukuamini zaidi na vitu vyangu vya kibinafsi. 3) Mafanikio ya Pamoja husema "Ninakuhitaji" Mume/mke ambaye anajitegemea mwenyewe atamwambia mpenzi wake kwa maneno au matendo "sikuhitaji". Kujitegemea mwenyewe huondoa uhusiano wa karibu na huzuia njia ya upendo tele. Uhusiano wa karibu hutokana na kufurahiya shughuli fulani pamoja. Inaweza kujumuisha kukuza masilahi ya kawaida, au kuweka na kukamilisha malengo ya familia au ya kaya. Yesu anazungumzia umuhimu wa kuhitaji yule mwingine katika Yohana 15:5 “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”


Page 56 Fikiria kuhusu uhusiano wako na mpenzi wako na ukamilishe ifwatayo: Pamoja na mume/mke wangu ningefurahiya Pia ninaweza kufurahiya k.v. kujifunza kucheza skwoshi, kuunda tena bustani, kupoteza uzito kadhaa, kupamba tena chumba chetu cha kulala, kusafisha dari ili kufanya mauzo kwenye buti ya gari.... Kuhitaji mpenzi wako kuwa pamoja nawe, na kufurahiya mafanikio ya pamoja kunaweza kuzuiliwa na tabia ya kujitegemea mwenyewe, uwoga wa kushindwa wakati unapojaribu kitu kipya, tabia ya kukosoa jaribio jipya la mpenzi, kuwa na nadharia ya ukamilifu n.k. Fikiria kuhusu mambo yale ambayo yanakuzuia kusema “nakupenda”. Ninajipata mwenyewe nikikataa kushiriki kazi na mpenzi wangu kwa sababu ya k.v. ninaogopa kukataliwa au kushindwa, ninapenda kufanya vitu kivyangu...... 4) Utoaji Sawa husema "ninakupenda" Uhusiano ambao una watu wawili wanaofikiriana zaidi badala ya hao wenyewe huonyesha utoaji sawa. Ndoa kati ya watu wawili wanaofikiria kuchukua tu kutoka kwa uhusiano huo, badala ya kupeana, itafifia sana. Tunasoma katika Yohana 15:13 "Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake." Yesu alitoa maisha yake kwa ajili yetu na akaonyesha kiwango kikubwa sana cha upendo wake kwa kufa kwake. Yohana 13:34 inataka tuitikie. “Amri mpya nawapa, mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.” Katika ndoa ambayo kuna utoaji sawa, upendo utatolewa na upendo utapokewa. Fikiria kuhusu uhusiano wako na mpenzi wako. Njia moja ninayoweza kutoa kwa mume/mke wangu ni


Page 57 k.v. kumpangia awe na marafiki wake jioni kwa kumshughulikia mtoto, kwenda kumtazama akicheza mchezo, kuamka kuwaangalia watoto usiku, kupika chakula anachokipenda, kumshutua na zawadi. Mambo tunayoambiana yanaweza pia kutoa upendo. Njia moja ambayo ninaweza kuonyesha vile mume/mke wangu ni wa maana ni kwa k.v. kumsifu mbele ya wengine, kumthamini kwa sifa nzuri za utu, kuonyesha vile muda tunaochukua pamoja peke yetu ni muhumu. Uchoyo unaweza kuwa kizuizi kikubwa cha kutoa. Fikiria njia ambazo umekuwa mchoyo katika uhusiano wako na mpenzi wako wa ndoa. Wakati mwingine sishughuliki na hitaji la mpenzi wangu la. k.v muda peke yetu, nafasi ya kufuatilia mambo anayopenda kufanya, mguso usio wa kingono, usahibu wa kingono kuanzishwa. Ninazuiliwa kutoa kwa mpenzi wangu kwa sababu ya uchongo wangu katika k.v. kutaka neno langu liwe la mwisho, kutaka njia zangu, kutothamini mambo ambayo yanamaanisha sana kwake.


Page 58 Vipaumbele Sahihi Kupitia Viambatano hivyo Vinne Kuchanganya viambatano hivyo vinne vya kujali, kuamini, kuhitaji na kutoa katika uhusiano wako wa ndoa unaweza kuleta upendo zaidi na furaha kubwa. Mpangilio wa kujali, kuamini, kuhitaji na kutoa huonekana kufuatana kutoka kwa moja hadi nyingine. Kwa maneno mengine ni vigumu kuamini ikiwa si hisi kwamba unajali. Vigumu kukuruhusu ujue ninakuhitaji ikiwa sina uhakika ninaweza kukuamini. Ni vigumu kupewa motisha ya kutoa ikiwa si hisi kwa kweli unanihitaji. Mungu anawaambia waume: “Wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyopenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake...” (Waefeso 5:25). Baada ya kutuongoza sisiwote " tunyenyekeane katika kicho cha Kristo," (Waefeso 5:21). Anawahimiza wake watii waume zao kama kumtii Bwana, kuwachukulia kama wanavyomchukulia Bwana. (Waefeso 5:22) Kipaumbele tunachopatia mambo ambayo si muhimu kwetu inaweza kupitisha ujumbe kwa mpenzi wetu wa vile tunavyojali, kuamini, kuwa na hitaji la, na kuweza kumpatia. Sasa chukueni muda pamoja wa kuzingatia sasa kile mnachohisi mpenzi wako anakipa kipaumbele na ungependelea kiwe nini. Ninavyochukulia kuwa vipaumbele vyako Tano vya juu ni: Vile ningependa viwe vipaumbele vyako Tano vya juu ni: Maombi ya Pendo Kamili 1 yohana 4 : “Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu." Wakati mahitaji yetu hayajafikiwa au tunahisi tuko chini kwenye orodha ya mume au mke wetu ya vipaumbele, ni rahisi kuwa na hofu kwamba hakuna kitu kitakachobadilika. Hofu kama hiyo inaweza kutunyanyanga usahibu. Yohana anatwambia kwamba pendo lililo kamili huitupa nje hofu. Ni Mungu tu ndiye aliye kamili lakini zawadi ya upendo Wake kwetu humaanisha hatupendi waume au wake zetu tu. Upendo kamili wa Mungu utusamehe na kututia nguvu. Uwezo wa maombi ni kubwa zaidi ya uamuzi wa mwanadamu wa kuwa tofauti. Kwa imani tunaweza kumuuliza Mungu atubadilishe. Kumsikia mume au mke akiombea mabadiliko kama hayo na kujua kwamba ana uwezo wa Mungu wa kufanya hivyo hushughulikia hofu vilivyo.


Page 59 Zingatia kujibu maswali yafuatayo unapokuwa ukifirikia vile unavyoweza kuonyesha upendo wako vyema kwa mpenzi wako: Nataka niwe zaidi na wala sio kuwadia mpenzi wangu. k.v. kujali zaidi, kusaidia zaidi, kupenda zaidi, kusamehe zaidi, kutokosoa, kutoonana mabaya n.k Sasa badilishaneni mkiomba pamoja: Baba wa Mbinguni nibadilishe ili niweze kuonyesha upendo vyema kwa nifanye niwe zaidi na wala sio Sitaki kuendelea kumuumiza. Bwana nibadilishe, ninataka kumpenda mpenzi wangu kwa njia nzuri zaidi.


Page 60 Wakati wa Maharusi Kushiriki Chukua muda mfupi ukizungumza tena kuhusu mahitaji yako ya kipaumbele kutoka kwa Kikao cha pili kwenye ukurasa wa 22. Uliza kama mahitaji hayo yamebadilika hata kidogo na vile vyema yanavyofikiwa. Fikiria kuhusu kiambatano cha kwanza cha usahibu, Kujali kwa Upendo. Zungumza kuhusu kuhisi kuwa yule mwingine anakujali, na vile hiyo inavyoonekana. Kwa mfano: Ningehisi unanijali kama ungenisugua mgogo kabla ya kulala. Au, ninafikiria kwamba uchungu wetu ambao haujapona bado unazuia vile tunavyojali. Ninafikiria ingekuwa vyema kuweka kando muda fulani ili tushughulikie kukiri na kusameheana. Ni lini unafikiria tunaweza kuipangia? Kisha zingatia vizuizi vya Kujali kwa Upendo ambavyo unaweza kuwa ukivipitia. Rudi kwa Kikundi Ombea masuala haya yaliyoletwa leo kama vile uchoyo, ukosoaji, na upuuzaji. Uliza ufahamu zaidi kuwadia mume/mke wako na kutambua mabadiliko ambayo yanastahili kufanywa.


Page 61 Mkutano wa Timu ya Ndoa Kwa kuongezea uratibishaji wa kalenda ya aina yoyote, upangaji, utathmini lengo unalohitaji kufanya, tunapendekeza yafuatayo: • Utakuwa umeangalia kiambatano cha kwanza cha usahibu, Kujali kwa Upendo, wakati wako wa Wakati wa Maharusi Kushiriki. Zungumzeni pamoja kuhusu maoni yako ya viambatano vile vingine vitatu, mawasiliano yanayoathiri, mafanikio ya pamoja, na utoaji sawa. Haswa zingatia vizuizi vya usahibu ambavyo hivajatatuliwa vya hasira, hofu, kujitegemea mwenyewe na uchoyo kwa kila kiambatano. Kwa mfano: Niligundua kwamba mimi kuwa mchoyo kuhusu kudai muda wangu peke yangu wikendi hunifanya nisifurahiye wakati wa raha na wewe na watoto. • Fikirieni pamoja jinsi kupitia mistari ifwatayo ya Biblia katika maisha yenu husaidia kushinda vizuizi vinne vya usahibu.: Waefeso 4:13 1Yohana 4:18-19 Wagalatia 6:2 Wafilipi 4:19 • Kamilisha sentensi hii: “Kile Mungu anataka kubadilisha sana kwangu ni...... Ombeni pamoja, mkimuuliza Mungu aanze kufanya mabadiliko hayo uliyoyatambua. Waume waongoze, wakifuatwa na wake. Mpendwa Baba wa Mbinguni, unajua vile ni rahisi kwangu kumwekea lawama kwa urahisi mume wangu, mke wangu wakati ni mini niliyekosea. Ninataka niweze kukubali kwa haraka wakati nimekosea, na kisha niwe tayari kuuliza msamaha. Sitaki tuwe na uchungu ambao haujapona kati yetu, ili tuweze kuwa huru kujali kwa upendo. Katika jina la Yesu, Amina. • Zungumzeni kuhusu vipaumbele vyenu vya juu na utambuaji na machungu yaliyoponywa wakati vipaumbele vinaonyesha kumpuuza mume/mke wako. • Wiki hii onyeshaneni shukrani wakati mahitaji yanapofikiwa. Hii itasaidia kuongeza tabia ya kutoa.


Page 62 Ukoo “Kwa hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja.” Mwanzo 2:24 Tunapozingatia yale yote tuliyoshughulikia hadi sasa katika kozi hii, tayari tumepitia kiashario cha mpango wa Mungu kwa ndoa. Mpango wa Mungu ulikuwa kwa kupitia ndoa, upwekwe wetu utaondolewa na hiyo hufanyika kwa kutuleta pamoja. Mojawapo ya hali muhimu sana ya kuleta umoja ni kupitia kuacha nyuma asili ya familia yetu; kuwaacha nyuma baba na mama. Kwa kweli tunaweza tu kupitia uhusiano wa karibu na mpenzi wetu, wakati tunapoangalia nyuma kwa familia zetu za utotoni. Tutahitajika kutambua kwamba bado tunashikilia mambo mengine ambayo yanastahili kuachwa nyuma. Ni wakati tuna usalama wa uhusiano tu, ambapo machungu yanaponywa, ambapo kuna kukiri mara kwa mara mabaya na msamaha unatolewa, na ambapo faraja hutolewa na mahitaji yanaonyeshwa kwa njia nzuri ya upendo, ndiyo tunakuwa tayari kuangalia nyuma kwa yaliyopita. Tunahakikishiwa kwamba tutakuwa tukishughulikia mambo yetu ya zamani na wapenzi wetu. Hatutakuwa peke yetu tukifanya hivi. Kuangalia Nyuma Kwa wengi wetu kuna kukataa kuangalia nyuma. Wengine watahisi kwamba mambo ya zamani ni ya zamani, kwa nini tuyafufue? Kuwa na uhakika kwamba ni kwa sababu matukio ya zamani yanaweza kusababisha uchungu sasa na yanastahili kushughulikiwa. Hakuna maoni yaliyotolewa kwamba tunastahili kuangalia nyuma bila sababu. Kuangalia nyuma mambo ya zamani haitupatii ufahamu kuhusu sasa tu, bali tunaweza pia kupitia uponyaji zaidi. Wengine wanaweza kusema “maisha yangu ya zamani hainiathiri na sihitaji kuangalia nyuma”. Tutakua tukichunguza zaidi njia ambazo matukio ya zamani huathiri mahusiano yetu ya sasa. jibu lingine linaweza kuwa “kwa sasa haijalishi”. Kweli ni kwamba Yesu hutuita tuishi maisha tele. Mojawapo ya vizuizi vikuu vya kuishi maisha kwa njia hiyo ni uchungu ambao haujapona. Wewe ni wa maana na wa thamani na unastahili uponyaji wowote unaowezekana. Wakati mwingine ni wale walio na uchungu mwingi kutoka utotoni, na ambao hawajiamini, ndiyo uhitaji kushawishiwa kwamba hao ni wamaana. Wasiwasi kuhusu kutowaheshimu wazazi, na haswa kuhusu kumkosoa mzazi mpendwa ambaye sasa amekufa, inaweza pia kutusababisha tusitake kutambua machungu yoyote kutoka utotoni. Tena, lengo si kulaumu, kushutumu au kukosoa. Kwa kweli Biblia inatuuliza tuwaheshimu wazazi wetu. Tunaweza kuheshimu watu wa kweli tu. Hakuna mtu yeyote kama mtu kamili, hakuna kitu chochote kama familia kamili. Watu wa kweli si wakamilifu. Wakati tunapojaribu kuwaheshimu watu tunajifanya kuwa wakamilifu na tunaingia mashakani. Kama vile katika ndoa ni vigumu kuepuka machungu, mara kwa mara bila kujua, hivyo pia wazazi watafanya makosa, watachagua chaguzi mbaya na kuwasababishia watoto wao wanaowapenda sana uchungu kwa kukosa hitaji fulani. Biblia inatuuliza tuwaheshimu wazazi wetu na pia “tuwaache.” Kuathiriwa pamoja na mpenzi wetu


Page 63 kuhusu wakati wa huzuni, masikitiko na uchungu kutoka siku za utotoni ambazo tulizishughulikia hapo awali peke yetu, inaweza kutupatia nafasi ya kupokea faraja na kujali kwao sasa. Kwa njia maalum sana hii itasaidia kutimiza mstari kutoka Mwanzo kuhusu kuondoka na kuambatana. Kwa wengine wetu ni safari kubwa sana kufikia mahali pa kusema "Baba yangu, mama yangu, walinipatia kila kitu walichoweza kutoa, il hali nilikosa mambo fulani muhimu na hiyo iliniumiza." Kutambua mambo tatu ambayo hayastahili kuachwa. Siku ya harusi ya wapenzi kuna matarajia mengo na furaha kuhusu maisha ya usoni. Karamu inapoisha na kupinduka ili kuangalia familia na marafiki kama mume na mke, mawazo yanaelekezwa kwa maisha mapya wanayoanza pamoja. Hiyo siyo wakati wa kufikiria kuhusu kitu kingine chochote isipokuwa kinachowatarajia mbele. walakini, punde tu maisha ya mapema ya ndoa kuanza inakuwa wazi kwamba kila mmoja ameleta “mzingo" mkubwa kwa uhusiano huo. Mzigo huo unaweza kujumuisha mambo kadhaa. 1. Imani Imani yetu inajumuisha matarajio tunayo ya majukumu katika ndoa. Tutawezaje kuchambua matarajio yetu ya wenyewe kwa wenyewe katika uhusiano huu? Kunaweza kuwa na maoni ya kuwa wanawake wafanye kazi zingine kwa nyumba na wanaume wafanye zingine k.v. yule anayetoa takataka, yule anayefunga milango usiku, anayeendesha gari kwa safari ndefu, anayeosha bafu, anayeangalia mafuta kwenye gari.................................. Hakuna majibu sahihi au mabaya kwa masuala haya lakini tunaweza kuwa na maoni mazito sana, mara kwa mara yanayohusiana na masaibu yetu katika nyumba yetu ya utotoni. Ndiposa uhusiano kuwa na umoja zaidi baadhi ya maoni haya yatahitajika kuachwa nyuma, kwa mfano, wakati haswa uhusiano unafanywa kati ya upendo unaotolewa, na jukumu fulani linalotimizwa; k.v. mume huonyesha upendo kwa kutoa pipa nje! Vile tunavyowaangalia wengine ndani ya familia na nje inaweza kuwa imani nyingine ambayo inaunda changamoto kwa umoja. Mtu mmoja anaweza kuwa amekua na maoni ya “jichunge kwa sababu hakuna mwingine atakayekuchunga” il hali mwingine anaweza kuwa amekua na tabia ya “kila wakati kuwa tayari kumsaidia mtu mwingine" katika nyumba yake ya utotoni. Tunaweza kukosa kugundua familia zingine hazishiriki au kutekeleza maoni sawa na yale tuliyokua nayo. Michakato ya mawazo ambayo tunatumia kuchambua mambo ambayo yanatufanyikia ni hali nyingine ya suala hili. Katika kikao cha baaadaye tutaangalia mitindo ya kuwaza ambayo inaweza kuharibu mahusiano mema. Baadhi ya mawazo ambayo yanaunda ndoa yetu tulijifunza nyumbani wakati wa utotoni. 2. Tabia Tunajifunza pia mitindo ya tabia utotoni. Tunavyofanya mambo mengine ni sehemu ya asili ya maisha ya familia ambayo tunaweza kugundua kuwa si sehemu ya masaibu ya familia ya utotoni ya mume au mke wetu. Tabia iliyofanya kazi katika nyumba yenu ukiwa mtoto inaweza kuwa haifai tena. Wengine wetu wanataka kwenda kinyume kabisa katika tabia zetu za utu uzima. Masaibu yetu ya shughuli zingine kama mtoto yana


Page 64 kumbukumbu ya kuhuzunisha au ya uchungu na tunataka kufanya mambo tofauti kabisa katika maisha ya usoni. Tunaonekana kukumbatia tulichokiona utotoni au kufanya kinyume chake. Pengine njia ya tatu ni kutambua kwamba, katika ndoa uhusiano mkubwa wa karibu utatokea wakati tunapochambua yale tunayotaka kufanya. Mojawapo ya tabia ambazo ni muhimu kwa safari yetu ya kuondoka na kuambatana ni njia ambayo mzozo ulishughulikiwa tulipokuwa tukikua. Mtu mmoja anaweza kusema niliona mizozo nilipokua nikikua, ilikuwa jambo la kawaida. Mtu mwingine anaweza kusema sidhanii niliona mzozo wowote lakini wakati mwingi kuliwa kumenyamaza na kuna baridi nyumbani. Familia zingine zinaonekana kuchukua kila fursa kupigana il hali zingine huepuka mizozo kivyovyote vile. Kila mmoja wetu anahitaji kuchunguza vile tulivyopitia mzozo tulipokuwa tukikua. Wale ambao ni wazazi wanaweza kuzigantia jinsi watoto wao watajibu swali la "Uliona mzozo ukitatuliwa aje ulipokuwa ukikua?” Jibu nzuri ni la mtoto yule anayeweza kusema, mara kwa mara nilimwona baba yangu akimwomba mama yangu msamaha na nikamsikia akimsamehe na nikamwona mama yangu akimwomba baba yangu msamaha na nikamsikia akimsamehe. Mungu amefanya toleo la mzozo kupitia uwezo wa uponyaji wa kukiri na msamaha, na kupitia faraja kwa uchungu unaotokea. Swali lingine linahusu njia ambayo upendo unatolewa na kupokewa. Kila mmoja wetu anahitaji kuuliza swali la, upendo ulifanana aje wakati tulipokua tukikua? Nyumba zinaweza kuwa mahali upendo unatolewa mara kwa mara, kupitia kukumbatiana na kushikana na mahali ambapo upendo husemwa mara kwa mara. Walakini, familia zingine nadra huonyesha upendo kupitia maneno au matendo na huonekana kupata kuwa vigumu kupokea au kutoa upendo. Kukua katika nyumba kama hiyo tunaweza kukumbuka upendo mdogo ukitolewa aidha kwa maneno au kupitia mguso unaofaa. Watu wazima wanaweza kuwa walijaribu kuchukua upendo kutoka kwetu kwa njia isiyofaa iliyoleta kuchanganyikiwa, au uchungu mwingi. 3. Mihemko Ijapokuwa wengi wetu huangalia siku yetu ya harusi kama mwanzo mpya, kwa haraka tunapata kwamba tunaingilia uhusiano wa ndoa na mizigo kadhaa ya mhemko. Kufahamu mpenzi wako vyema na haswa yale yote anayoleta kwa uhusiano huu kutoka kwa zamani, itakupatia ufahamu mwema wa njia za kumpenda sasa. Hasira, hofu, hatia, aibu kutoka utotoni ambazo hazijatatuliwa na uchungu ambayo haujapona kutoka kwa mahitaji ambayo hayajafikiwa zinaweza kuletwa zote kwa miezi na miaka ya kwanza ya ndoa. Mzigo wa mhemko unaweza kuathiri ubora wa ndoa yetu kwa sababu huathiri mawazo yetu, majibu yetu na hisia zetu kuhusu maisha ya familia. Basi “kuwaacha”, itamaanisha kuondoa mzigo huu wa maisha yetu ya zamani, haswa kutoka kwa familia yetu ya utotoni. Tutatambua kile tulichokileta kwa ndoa yetu, tushukuru kwa kile ambacho ni kizuri na cha maana na kisha “tuwache nyuma” kile ambacho si kizuri, kweli au cha maana.


Page 65 Tunapofikiria kuhusu maisha ya utotoni, je! tunatafuta nini? Je! Ni nini ninachoweza kukithamini? Je! Nimeonyesha shukrani hii kwa Mungu na kwa wazazi wangu? Je! Matarajio yangu kuhusu ndoa yametoka wapi? Je! Ni mahitaji gani yanayostahili kuachwa nyumba? Je! nimeleta matarajio yoyote yanayohusu tabia zangu kwa ndoa yangu, ambayo ninahitaji sasa kuacha nyuma? Je! Nina uchungu kutoka utotoni ambayo ninahitaji kuacha nyuma? Je! Ninaweza kushiriki uchungu huo na mpenzi wangu na kupokea faraja? Je! Nimetambua mahitaji ambayo hayakufikiwa utotoni mwangu? Je! Ninaweza kushiriki ukosefu huo na mpenzi wangu na kupokea faraja? Mahitaji ya Usahibu Utotoni Mahitaji ambayo hajafikiwa utotoni bado yanaweza kuathiri uhusiano wetu kama mtu mzima na mahitaji haya yanaweza kueleweka, na upungufu huo unaweza kukabiliwa. Ni muhimu kutathmini kiwango kile ambacho mahitaji ya usahibu yalifikiwa au hayakufikiwa na wazazi/ walezi utotoni. Angalia Mahitaji ya Usahibu yaliyoorodheshwa baadaye na ulize 1. “Je! Mama yangu aliwezaje kufikia hitaji hili kila wakati?” Kama unaweza kukumbuka njia maalum ambayo alifikia hitaji hili, weka mviringo nusu kando ya hitaji hilo kwenye orodha. k.v. unaweza kukumbuka akikusomea hadithi wakati wa kulala ambayo ilifikia hitaji lako la kusikizwa.


Page 66 2. “Je! baba yako aliwezaje kufikia hitaji hili kila wakati?” Ikiwa unaweza kukumbuka wakati maalum na njia ambazo baba yako alifikia hitaji hili , weka alama nusu kando ya hitaji hilo kwenye orodha. k.v. ninakumbuka baba yangu akinikumbatia wakati baisikeli yangu ilipoibiwa na hiyo ilinifariji. Ikiwa ni mtu mmoja tu aliyefikia hitaji, itakubidi uweke alama nusu kando yake. Ikiwa wazazi/walezi wote walifikia hitaji hilo itakubidi uweke alama kamili. Weka X kando ya mahitaji yoyote ambayo ni tupu, inaashiria kwamba mahitaji hayo hayakufikiwa kila wakati na mama au baba. Ikiwa utotoni mwako kuna walezi kando ya wazazi wako wa kibiolojia kwa sababu ya kifo, talaka, au kuchukuliwa, basi kamilisha zoezi hili mara mbili, kwanza ukiangazia vile mahitaji yako yalivyofikiwa na wazazi wa kibiolojia na kisha walezi. Kweli kwamba mzazi mmoja au wote wa kibiolojia hawakuwepo ili kufikia mahitaji inawakilisha ukosefu ambao bado unahitaji kusikitikiwa. Mahitaji ya Usahibu Yaliyofikiwa ( ) au X ambayo haikufikiwa utotoni Ridhaa – mapokezi/majibu ya kutaka na yenye kibali Upendo –kujali kwa upendo uliyoonyeshwa kwa kusema/mguso unaofaa Shukrani – kuonyeshana shukrani ya kibinafsi Kukubali – kufikiria na kuzungumza vyema, kusifu Usikivu – kuchukuliana mawazo, kuingia ulimwengu wa yule mwingine Faraja- kuwa na unyenyekevu na kufariji Himizo – kusisitiza kwenda mbele kuwadia lengo kwa njia nzuri Heshima – kuthamini na kuheshimu; kuonyesha umaana mkubwa Usalama – matumaini ya umoja katika uhusiano; uhuru kutokana na mabaya/hofu Usaidizi – kuwa pamoja na kubeba mzigo kwa ungwana Chukua fursa ya kushiriki vile mahitaji yalivyofikiwa au kutofikiwa utotoni na mpenzi wako. Hii ni fursa nyingine kwa mke kuelewa jinsi ya kumpenda na kumjali mume wake vyema na mume jinsi ya kumpenda na kumjali mke wake kwa ufahamu zaidi. Tunapokuwa tukitafuta kumpa mpenzi mengi ya yale aliyokosa utotoni mwake au kuendelea kutoa kile alichofurahiya kupokea, umoja katika uhusiano wa ndoa na kuwaacha baba na baba huongezeka. Kukasirikia familia ya utotoni ya mume au kufafanua kwa kurazinisha kwanini mahitaji ya mke yalipuuzwa haitaleta uponyaji na umoja. Faraja, huruma, kujali na kujitolea kufikia mahitaji, italeta uponyaji huo na itaongeza uhusiano wako. Shinikizo la Kutendakazi Mojawapo ya mambo ya kuangamiza ambayo wazazi wanaweza kuwaongezea watoto wao ni shiniko la kutendakazi ili kupendwa. Ni shiniko lisilofaa, lakini pia mara kwa mara ni shinikzo linalopeanwa bila ya mzazi kutambua kinachofanyika. Kutarajia au kudai kwamba mtu mwingine atendekazi kwa njia zingine ili kuweza kukubaliwa, kuidhinishwa, na kupendwa ni kiambatano kikubwa katika mahusiano mabaya.


Page 67 Shiniko la kutendakazi huathiri. Mtoto bila kujua anaweza kwa urahisi kuanza kuamni kwamba Utendakazi ni sawa na Upendo. Shinikizo/madai ya kutendakazi yanaweza kuonekana kama yoyote ya yafuatayo: Mzazi kuzingatia kila wakati gredi ya chini sana ya mtoto shuleni. Mzazi kuuliza kila wakati “hivyo ndivyo vyema unavyoweza kufanya?” Kusisitiza kile ambacho hakijafanywa, ambacho hakijakamilishwa, na ambacho hakijatosha badala ya kusifu maendeleo ya mtoto. Kuvunja moyo kwa maneno ambayo yanashambulia thamani au tabia ya mtoto Majina ya utani ambayo ni ya kuaibisha Kulinganishwa na wengine ambao wanaonekana kuwa kamili zaidi Kutovumilia maonyesho ya kawaida ya mhemko wa uchungu, huzuni na hasira. Njia yoyote ya dhuluma – kimwili, kimhemko au kingono Matarajio ya kuwa kama Mama au Baba Shiniko la kutosababisha shida zilezile kama za mtoto mkatili kwa wazazi wako. Ukirejelea orodha hii, zingatia majibu yako kwa yafuatayo: 1. Nikikua katika familia yangu, wakati mwingine nilihisi kama nilihitajika kufikia.... k.v. Matarajio ya mama kuhusu ninavyofanana, mafanikio ya dada/ndugu, mipango ya baba kwa maisha yangu ya usoni, shinikizo la jamii kwa jukumu langu kama mwanaume/mwanamke.................................... 2. Nilipokuwa nikikua nilipokea sifa za k.v. alama nzuri na matokeo ya mtihani, nilivyokuwa navutia, kucheza michezo, kushinda michezo, uaminifu wangu, kufanya kazi nyumbani................. Angalia orodha yako. Je! Mambo mengi uliyosifiwa kuhusu kama mtoto yalihusiana na mambo ULIYOYAFANYA au sifa hizo zilizingatia WEWE NI NANI KAMA MTU? Andika chini mawazo yoyote unayo kuhusu jambo hili.


Page 68 Ukiangalia nyuma utotoni mwako, je! kuna ujumbe wowote uliyopokea kutoka kwa wazazi wako ambao ulionekana kutofaa? K.v. wanaume wa kweli hawalii, kuwa mnono hakukubaliwi, daima lazima nifanye vyema, daima lazima niwe mzuri, wakati ujao utafanya vyema........ Shiniko la kutendakazi katika husiano wa ndoa Orodha ifwatayo ya maswali inarejelea vile kupitia shinikizo la kutendakazi utotoni kunaweza baadaye kuonekana katika tabia ya utu uzima. 1. Upendo unakuwa wa masharti wakati nisipotoa upendo kwa sababu mpenzi wangu haja k.v. kubaliana na maoni yangu, kwa hiari kugundua ninahisi vibaya, kuja nyumbani mapema kutoka kazini, weka petroli kwenye gari, panga hafla ya jioni kwa sharehe maalum..... 2. Wakati mwingine ninahisi shinikizo la kutendakazi kuhusu k.v. kuwa mzuri kwa kazi za nyumbani, kufanya kujamiiana, kutafuta cheo...........


Page 69 3. Wakati mwingine mimi hujipata nikimshinikiza mpenzi wangu kuhusu k.v. kusaidia nyumbani, kuchukua muda na watoto, mara ngapi tunayofanya kujamiiana 4. Baadhi ya “mbinu zangu za kushinikiza" ni pamoja na k.v. kusumbua na kulalamika, kuwa mbali na kujitenga, kusema hapana kwa ngono, kulinganisha na rafiki, ndugu, jirani NYUMBA YA KUPUUZA Katika mazingira haya wazazi hawahusiki vilivyo na watoto wao katika njia zinazofaaa. Kuupuuza kunaweza kuwa kwa sababu tofauti; nyumba zenye walevi au wanaofanya kazi sana, wazazi wenye shughuli, umbali, kufungwa kimhemko. Ujumbe uliyopokewa ni “Wewe si muhimu sana kwangu”. Mtoto anaweza kutafuta kusikizwa kupitia kufanya vyema shuleni au michezoni, au kupitia tabia ya kuharibu au njia zisizofaa za kufikia kujulikana na marafiki.


Page 70 Andika chini mawazo kadhaa kuhusu masaibu yoyote ya wazazi kutohusika vilivyo. Kama mtoto nilijaribu kusikizwa au kugunduliwa kupitia.... Kumbukumbu kutoka utotoni Kutoka kwa kumbukumbu za utotoni, orodhesha neno moja, au kifungu kimoja kinachofafanua kila mzazi wako. k.v. mwenye bidii, rahisi kuzungumza na yeye, mwenye raha, mwamanifu k.v. mwenye nadharia ya ukamilifu, anakasirika haraka, mgumu, anayejitegemea mwenyewe BABA Nguvu Udhaifu MAMA Nguvu Udhaifu Je! Ni nini ulichopenda kujihusu mwenyewe ulipokuwa mtoto? k.v. nilikuwa mzuri michezoni, nilikuwa na marafiki wengi, nilikuwa mzuri kwa wanyama, ningeweza kufanya watu wacheke, nilikuwa mwenye hisia Je! Ni nini haukikipenda zaidi kujihusu mwenyewe ulipokuwa mtoto?


Page 71 k.v. Sikuwa mwerevu shuleni, kila wakati nilikuwa nikiwachwa, nilikuwa mnono, niikuwa nikidhulumiwa kwa urahisi... Ulipokuwa mtoto, ni nani aliyekupatia .....? Upendo Faraja Usikivu Ulipokuwa mtoto, mama angekusifu aje? Ulipokuwa mtoto, mama angekukosoa aje? Ulipokuwa mtoto, baba angekusifu aje? Ulipokuwa mtoto, baba angekukosoa aje? Ulipokuwa ukikua, ulijua aje kwamba mama anakupenda?


Page 72 k.v. angeniambia, alinikumbatia, alininunulia vitu, alinifanyia vitu.... Ulipokuwa ukikua, ulijua aje kwamba baba anakupenda?


Page 73 Mama na baba walishughulikia aje mzozo kati yao na wewe? Baba ange Mama ange Ulijua aje wazazi wako walipendana ulipokuwa ukikua? Walionyesha aje? k.v. walikumbatiana na kubusu sana, walielewana vyema, walicheka sana, walipeana nafasi........


Page 74 Ashiria aidha “Mama” “Baba”, “Wote” “Hamna” kando na vifungu vifwatavyo ili kusaidia kufafanua maisha yako kama mtoto: Kiongozi wa Familia Mtoa nidhamu Mkuu Kukasirika Haraka Alikuwa sawa kunipa upendo Mgumu kupendeza Mzazi niliyehisi karibu sana naye Je! Ni nini kinachofafanua vyema mawazo yako ya utotoni? Familia yetu ilionekana sawa kwa wengine – lakini nilijua haikuwa hivyo Nilizingatiwa kwa sababu ya vitu nilivyofanya Nilipendwa kwa yule niliyekuwa --- tabia yangu Nilikuwa mtu wa nje, mwangalizi wa familia yote Nyumba yetu ilihitaji uangalifu mkubwa, ilitegemea utendakazi, sheria nyingi Mara kwa mara nilijihisi mpweke Kila wakati nilihisi “tulikuwa tukitembea juu ya kaka la yai” nyumbani Kila wakati ilikuwa muhimu kwangu kumpendeza kila mtu Sina uhakika kwamba mtu yeyote alinifahamu vyema Ukifikiria kuhusu familia yako, je! unadhania kuna kitu kilichokosa katika familia yako: Kama ni hivyo, ni nini? Ulihisi aje ulipokuwa ukikamilisha maswali yaliyo hapo juu? Je! Unadhania masaibu yako kama mtoto yanaweza kuwa yakiathiri vile unavyohusiana na mpenzi wako wa ndoa?


Page 75 k.v. sichukulii maoni kwa urahisi kwa sababu inanikumbusha mama yangu mwenye kuamuru, ninahitaji usikivu mwingi sasa kwa sababu niliukosa kutoka kwa baba yangu, ninahisi zaidi ukosoaji kwa sababu ya kudhihakiwa.......... Picha zifwatazo zitasaidia kufafanua majibu yanayofikia lengo wakati tunapoumia, tunahuzunika au kuhisi vibaya. Majibu yanayofaa kwa mume, kwa mke, ambaye ana umia kwa sababu ya uchungu wa kumbukumbu za utotoni, ni faraja. Wakati kumbukumbu ni nzuri, furahieni.


Page 76 Wakati wa Maharusi Kushiriki Zungumzeni kuhusu hisia unazo unapoulizwa uangalie nyuma kwa maisha yako ya utotoni Katika kila eneo la imani, tabia na mihemko tafuta mambo ambayo ni vizuri kuacha nyuma sasa. Hii pia ni nafasi nzuri ya kujenga uhusiano wa karibu katika ndoa kwa kufurahi pamoja kuhusu masaibu mazuri kutoka utotoni. Ikiwa mmoja wenu au ninyi wote wawili mlikuwa na maisha ya utotoni yenye uchungu ambayo hamwezi kuyafurahiya, mshiriki faraja. Hitaji/Uchungu wa Mhemko Nilihisi nimeumia wakati .. ; Ninahitaji dhibitisho la …; Kukubaliwa na kuhimizwa itasaidia sana; Ninahisi vibaya na sijui ni kwanini; Majibu ya Kawaida Yasiyofaa “pengo” la mawasiliano huanza – hatuwezi kuwasiliana } Uwazaji wa mantiki Singefanya hivyo kama .. Hivyo ndivyo ilivyo .. Ukosoaji Una hisi kupita kiasi Singeumia kama Malalamiko Pia mimi nimeumia Natamani kama Kupuuza Tubadilishe mada { Majibu haya kila wakati hukosa lengo la kupatana au kuponya masuala ya mhemko Hitaji/Uchungu wa Mhemko Majibu ya mhemko Kuleta uponyaji, kuelewa, utimilifu, uhusiano wa karibu Majibu ya mhemko daima hujumuisha kuelewa, huruma, ungwana, udhibitishaji, na mara kwa mara hujumuisha kukiri Mifano ya Majibu Mema ya Mhemko “Kwa kweli sioni kama unaumia.”; Ninajuta sana kwa sehemu yangu ya kukuumiza; sipendi kukuona ukiumia; Unaweza kushiriki nami sasa vile nilivyokuumiza; Hiyo ilikufanya uhisi aje? Ninataka kuelewa na kuifanya iwe sawa, ninaweza kuona nilikuumiza kwa…… na hiyo ilikuwa vibaya kwa upande wangu. Je! Utanisamehe?; , ninahuzunika kwamba una hofu sana; Ninakujali sana na ninakupenda; ninajitolea kupitia mambo haya pamoja na wewe.


Page 77 Rudi kwa Kikundi Kwa maombi mshukuru Mungu kwamba ameleta maharusi wote pamoja na kwa njia maalum wanayoweza kuhudumiana sasa. Mshukuru Mungu kwa masaibu mazuri ambayo kila mmoja amekuwa nayo. Ombeeni uponyaji uendelee kwa masaibu ya utotoni yenye uchungu.


Page 78 Mkutano wa Timu ya Ndoa Weka muda wa kuratibisha kalenda yoyote, upangaji, na utathmini wa lengo unalohitaji kufanya. Ikiwezekana, kila moja inastahili kukamilisha majibu yoyote ambayo hayajakamilika kwa maswali yaliyoshughulikiwa katika kikao hiki kabla ya Mkutano wa Timu ya Ndoa kuanza. • Kwa kuanza na njia ambazo mahitaji yako ya usahibu wa utotoni yalivyofikiwa, na nani aliyeyafikia, shiriki majibu yako na yule mwingine. Kipaumbele kinastahili kupewa kusikiliza, na kujibu inavyostahili kwa yule mwingine. Baada ya kufikiria mahitaji hayo, yaliyofikiwa vyema na yale ambayo hayakufikiwa zamani, sasa utakuwa na ufahamu mkubwa wa mahitaji ya yule mwingine. Itasaidia kuwa makini sana kufikia mahitaji ya kipaumbele ya yule mwingine wiki hii ijayo. • Sasa angalia majibu yako kuhusu kiasi cha shinikizo la kutendakazi uliyopitia utotoni. Fikiria kuhusu njia ambazo jambo hili linaathiri ndoa yako. Kwa wengine masaibu hayo yalikuwa kupuuzwa na kutopendwa zaidi ya shinikizo. Onyesha unajali yule mwingine kuhusu kumbukumbu hizi • Unapokuwa ukirishiriki majibu yako ya maswali haya kuhusu kumbukumbu za utotoni, ukianza na nguvu na udhaifu wa wazazi , fikiria juu ya vile mambo haya yanaathiri ndoa yako sasa. Sifa na ukosoaji, kushiriki upendo na njia ambayo mzozo ulivyoshughulikiwa, ni masuala muhimu sana kwa maendeleo yetu ya kibinafsi. • Fanyeni shukrani kwa maneno kwa kipaumbele cha yule mwingine wiki hii. Kudhibitishiana upendo kutejenga pia usalama. • Chukua fursa ya kupanga shughuli kadhaa za kushiriki pamoja kwa siku chache zijazo. Ombeaneni.


Page 79 Kuwa Huru Kutokana na Mawazo Mabaya Tulipokuwa tukifikiria kuhusu familia zetu za utotoni, ilikuwa wazi kwamba wakati nia ya wazazi kwa watoto wao inaweza kuwa nzuri, mbinu wanayoichagua inaweza kuwa si nzuri na inaweza kuumiza. Mzazi anawezakuwa anamtakia mtoto anayempenda sana mema, lakini njia anayopitia ili kuifikia inaweza kuwa haifai. Mzazi atataka kwamba mtoto wake awe na fursa aliyokosa mwenyewe k.v. kujifunza chombo za mziki. Walakini mtoto anaweza kuhisi hana hamu ya masomo na zoezi linalohitajika, na anaweza kuanza kukataa fursa hiyo. Lengo la mzazi lilikuwa nzuri lakini mbinu haikusaidia. Mitindo ya Kuwaza Mtindo wa kuwaza ni tabia ambayo akili zetu huchakata kinachotufanyikia, na kile kinachofanyika karibu nasi. Baadhi ya mitindo yetu ya kuwaza ni nzuri na yenye afya, huangazia kilicho kweli. Mengine si nzuri. Mengine yanaweza kuangazia ugeuzaji kweli ambayo huzuia uwezo wetu wa kustahimili maisha na kupitia usahibu katika mahusiano yetu. Tunaweza kuwa tumeona njia zingine za kuwaza zilizoundwa na wazazi. Tunastahili kuuliza kama mitindo hiyo inaangazia kweli. Mitindo sita mbaya, zilizogeuzwa zitatambuliwa na fursa itatolewa ya kuchambua kama tunaweza kuathiriwa na mojawapo ya mitindo hizi. Kufikiria vibaya kunahitaji kupewa changamoto na kubadilishwa na kweli. Mtindo wetu wa kuwaza kuhusu mambo yaliyotufanyikia unaweza kuongeza uchungu wetu. Kidadisi cha Mawazo Mabaya Hakiki taarifa hizi na ashiria kukubali au kutokukubali kwako na kisha mpenzi wako. Kwa maneno mengine, je! kuna taarifa za kweli kwako? Je! taarifa hizi zinaonekana kweli kwa mpenzi wako? Mimi mwenyewe Mume/Mke 1. ninaona mambo kama kweli sana. 2. mimi hufanya mambo madogo kuwa makubwa. 3. Mara kwa mara mimi huchukulia vitu binafsi. 4. Masikitiko ya zamani yanaonekana kubashiri maisha ya usoni. 5. Ninachohisi ni muhimu zaidi ya kweli. 6. Mara kwa mara nafikiria watu hujiletea shida zao. 7. Kuna mahali pa kila kitu, kila kitu mahali pake. 8. Mambo mengi yanaonekana kuwa suala kubwa. 9. Ni muhimu sana kuhisi kibali cha wengine. 10. Ninajua mambo hayatakuwa mema zaidi.


Page 80 11. Kwa kweli siwezi kuamini ninapendwa isipokuwa nihisi. 12. Ninaweza kushughulikia shida yoyote ambayo inanikujia. 13. Kuwa kamili kwa kile ninachofanya ni muhimu kwangu. 14. Ninaonekana kuhisi sana usumbufu mdogo. 15. Lazima niwe sehemu ya sababu ikiwa mtu katika familia yangu amekasirika, 16. Mimi huwaacha watu wakiniumiza au kunisikitisha. 17. Nikihisi sipendwi, ni kwa sababu hakuna mtu anayenipenda. 18. Hakuna sababu ya kuwa na mhemko mwingi. Sasa angalieni kila taarifa ambayo ilikuwa kweli kwako. Picha iliyo hapo chini inatoa maswali ambayo yanafafana na mitindo hiyo sita mbaya. Pata vitu unavyokubaliana navyo, kisha tambua ni mtindo upi wa kuwaza taarifa hii inawakilisha. Utofautishaji Utiaji chumvi Ubinafsishaji 1, 7, 13 2, 8, 14 3, 9, 15 Ujumlishaji Uwazaji wa Mhemko Udhalilishaji 4, 10, 16 5, 11, 17 6, 12, 18 Mpenzi wetu wa ndoa anaweza kuwa na maoni ya kusaidia kuhusu mtindo wetu mwenyewe wa kuwaza. Maoni yao yanaweza kuwa sahihi zaidi yetu. Sikiliza kwa makini na bila kujitetea maoni ya mpenzi wako. Mtindo wa kuwaza tunaostahili kuzingatia sana itakuwa tuliyopata alama nyingi, tuliyotia alama nyingi. Kulingana na zoezi hili, nina mazoea ya Kulingana na zoezi hili, mpenzi wangu anaonekana kuwa na mazoea ya Mitindo hii mbaya ya kuwaza huchangia uchungu wa mhemko. Kila mmoja huonekana kuwa mhasiriwa wa angalau mojawapo wa mitindo hii. Tunapozingatia njia za kushinda mitindo hii, kuna mistari miwili za Biblia ambazo zitasaidia. 2 Wakorintho 10:5 “Na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo” na Wafilipi 4:8 “Hatimaye ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yoyote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yoyete yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yoyote, yatafakarini hayo.” 1. Utofautishaji: • Kuna njia moja tu ya kufanya kitu. • Kila kitu ni sawa au siyo sawa • Ulimwengu unaonekana kamili.


Page 81 Ufafanuzi Utofautishaji ni mtindo wa mtu mwenye kuwaza nadharia ya ukamilifu ambaye huona maisha kuwa kila kitu au si kitu, nzuri au mbaya, nyeusi au nyeupe. Inaweza kuwa vigumu kuishi nao kwa sababu tabia yao ni ya kuhukumu na kulazimisha. Wanaotofautisha uhukumu utendakazi wao na wa wengine kwa misingi ya viwango vyao visivyowezekana. Wakati wasipofikia wazo lao la ukamilifu hao husumbuliwa na hasira na kuvunjika moyo. Hao huzingatia kilichokibaya badala ya kilichokizuri. Sheria ngumu hushikiliwa ili kutathmini maisha. Hao huridhika kidogo kwa utendakazi mzuri hata kama kumekuwa na bidii halisi. Hata wakati wamefaulu, hao huonyesha furaha ndogo kwa sababu walikuwa wakitarajia kufaulu. Usuli Familia ambazo zinafuata sheria vikamilifu, wakosoaji au zinazotegemea utendakazi zinaweza kukuza tabia hizi za kuwaza nadhiria ya ukamilifu. Katika nyumba kama hizo mtoto huwa na mashaka mengi hofu nyingi. Pengine kila mtoto alichofanya hakikuwa kizuri kabisa. Pengine wengine karibu na yeye walikuwa wakikoselewa na kutathminiwa kila wakati. Nyumba ambazo zilikuwa na mpangilio kupita kiasi zinaweza kuchangia ukuzaji wa tabia hii. Kweli Njia ya kupata kitu, pamoja na bidii na motisha pia ina thamana hata kama matokeo ya mwisho yanasikitisha. Masuala mengine ni nyeusi au nyeupe lakini mengi ni kivuli cha kijivu. Msimamo wa katikati utahitajika kuainishwa na kutambuliwa ili masuala mengi na chaguzi kadhaa zitatue shida. Athari kwa ndoa Wanaotofautisha wanaweza kufafanua kila suala kwa urahisi sana. Hao hutazamia mabaya maishani na hupata kuwa vigumu kufurahiya wakati wa furaha. Hao huvunjwa moyo kwa urahisi na kudanganyika. Hao hukataa na kuwalaumu wengine na huwa na mazoea ya kushambulia, au kuwa na uchungu, wenye chuki au kujitenga. Mfano wa Utofautishaji Hali moja ya mradi unaofanyiwa kazi hukosolewa. Jibu la utofautishaji ni, Mradi huu hauna maana kwanzia mwanzo hadi mwisho. Matokeo ya jibu hilo Hasira inaweza kugeuzwa ndani au kusababisha ulipizaji kisasi. Jibu la kweli zaidi linaweza kuwa Mradi huo haukuwa kamili, lakini kulikuwa na mengo yaliyomema. Ninaweza kuiboresha. Basi Itakuwa rahisi kutathmini ukosoaji, kuzingatia mabadiliko na kuendelea mbele. Kushinda Utofautishaji Mojawapo ya hatua muhimu sana katika mchakato huu ni kufahamu kinachofanyika na kutafiti kilichosababisha jibu lako. “Na tukiteka nyara kila fikira – tukiangusha mawazo” 2 Wakorintho 10:3-5 “Yatafakarini yaliyo kweli". Wafilipi 4:8 Kwa usaidizi wa mpenzi wako, kataa mawazo mabaya na ujifunze majibu mapya. Teka Nyara Mawazo II Wakorintho 10:5 Yatafakarini Yaliyo Kweli Wafilipi 4:8 Badilisha: (k.v.) “ikiwa haifanywi kwa njia hii haitafanya kazi.” Na: “Njia yangu siyo njia ya pekee, njia za wengine zinaweza kufanya kazi pia.” Badilisha: Na:


Page 82 Badilisha: Na: 2. Utiaji chumvi: Kufanya mambo madogo kuwa makubwa. Ufafanuzi Mazoea ya kuongezea chumvi matukio hadi kila kitu kinaonekana kama balaa. Mtu kama huyo ni rahisi kwake kukasirika, kutokuwa na huruma na kujilaumu mwenyewe au kujawa na hofu au kujihurumia. Wengine wanaweza kumwona kama mwenye mawazo mengi, mwenye shughuli nyingi za shida zake mwenye, mlalamikaji na mwenye kuhisi zaidi. Usuli Mazingira ya nyumba ya utotoni inaweza kuwa walikuwa wakifanya vitu vidogo kuwa vikubwa. Nidhamu inaweza kuwa ilipita kiasi na ilikuwa kosa kubwa. Kumwaga maziwa ilisababisha kushambuliwa kitabia. Pengine mzazi alikuwa na shughuli nyingi za hali yake mwenyewe, akipitia upweke, kukataliwa, au hofu, ambayo ilichangia kwake kuona balaa katika kila hali. Mzazi anaweza kuwa alimtazamia visivyofaa mtoto achukue jukumu lililopita uwezo wa mtoto au kukomaa kwake, matokeo yake ni mtoto kuhisi anashindwa. Viashirio vinavyowezekana vya utiaji chumvi Utumiaji wa kila wakati wa maneno mabaya au vifungu kama vile haiwezekani, kila wakati, taharuki, vigumu, kuaribika, kuogofya, mbaya, isiyoweza kurekebishwa, muda umekwisha, zote, hakuna. Mawazo hawa ya kutia chumvi yanaweza kuleta kujilaumu mwenyewe au kuwakosoa wengine. Kweli Vilima si milima. Kila kitu si tukio kubwa. Mahitaji ya asilimia 50 yahitaji jibu la asilimia 50. Wakati mwingine watu hutufanya vibaya, lakini si kila wakati. Wakati mwingine tunafanya vitu vibaya, lakini si kila kitu. Kwa kawaida ni mapema sana kufa moyo. Athari kwa ndoa Ni vigumu kuishi katika mazingira ambapo kila tukio ndogo linafanyika kuwa balaa. Wakati matukio magumu yanapotokea kunakuwa na uwezo mdogo wa kustahimili. Kujaribu kuendelea na maisha kana kwamba kila kitu ni tukio kubwa hutoa nguvu za mhemko. Mfano wa Utiaji chumvi Kikombe cha kahawa kinaangushwa na kuvunjika: Jibu la mwenye kutia chumvi, Ni hivyo, siku yangu yote imeharibika! Matokeo ya jibu hilo Fikra mbaya ambazo zinasababisha siku hiyo kuwa mbaya, kuwaza sana, na kuwa na unyogovu. Jibu la kweli zaidi linaweza kuwa Mambo haya hufanyika, ni kikombe tu ambacho kinaweza kubadilishwa kwa urahisi. Nitasafisha. Kushinda Utiaji chumvi Kuwa mwangalifu kwa maneno ya kuchochea kama vile, daima, kila wakati, hakuna mtu, hamna, mbaya, mbaya zaidi, kutisha, isiyopendeza. Tafiti kilichosababisha jibu la aina hii na kisha uteke nyara mawazo yako, ukiyabadilisha na mawazo ya kweli ya kurazinisha.


Page 83 Teka Nyara Mawazo 2 Wakorintho 10:5 Yatafakarini Yaliyo Kweli Wafilipi 4:8 Badilisha: (k.v.) “Kila kitu kimeharibika!” Na: “Hali hii si nzuri lakini ninaweza kuishinda. Ninashangaa vile Mungu anavyoona kile nilichofanya?" Badilisha: Na: Badilisha Na 3. Kubinafsisha: Matukio ya maisha yanaonekana kama kukataliwa na mashambulizi ya kibinafsi. Kuna mtindo wa kuwaza wa "lazima iwe ni kosa langu" Ufafanuzi Mtu mwenye kubinafsisha hupitia fedheha isiyofaa kwa kuchukua uwajibikaji wa matukio mengi ya maisha. Mambo yanayofanyika huonekana kama kukataliwa au mashambulizi. Mtu anayebinafsisha anaweza kununa na kuumia virahisi, kujilaumu mwenyewe kwa kila kitu. Wengine wanaweza kuwafafanua kama wadhaifu, watoto au wenye kuhisi kupita kiasi. Mara kwa mara huwa na shaka na hujilaumu wenyewe. Usuli Watu wenye kubinafsisha mara kwa mara hutoka kwa mazingira ya nyumba iliyo na ukosoaji na upuuzaji mwingi ambapo walikuwa wakilaumiwa vibaya kwa chochote kilichofanyika. Mtoto anaweza kuwa alikua akiwa na mawazo mabaya ya kuwa kuna kitu kibaya kwake. Kweli Sisi sio lengo au sababu ya kila kitu kinachotufanyikia. Kwa kawaida kile kinachofanyika hakuna chochote cha kufanya na sisi, au mtu mwingine zaidi yetu sisi. Ukweli wa Biblia unajumuisha Warumi 12:3, Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. Wafilipi 2:3-4, Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mpenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. 1 Petro 5:7 Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Athari kwa ndoa Tunapochukulia kila kitu kibinafsi, tunapata hatari ya kutokua na kiasi kwa mpenzi wetu, na kusababisha wasiwasi usiofaa katika ndoa. Mfano wa Kubinafsisha Rafiki anapiga simu ili kughairi kuja kunywa kahawa kwasababu anahitaji kumtembelea mama yake hospitalini. Jibu la mwenye kubinafsisha ni; Hataki kamwe kuja kunywa kahawa. Matokeo ya jibu hilo; Hisia za kukataliwa na kukasirika hutokea na hoja ya kumjali mama ya rafiki hupuuzwa. Wazo linaweza kuja akilini kwamba rafiki huyu anipendi. Ikifwatiwa na, pengine hakuna mtu anayenipenda.


Page 84 Jibu la kweli zaidi linaweza kuwa; Ninasikitika kwamba hatutaweza kunywa kahawa pamoja lakini rafiki yangu lazima aende kumwona mama yake. Ninatazamia kupanga tupatane na yeye siku nyingine. Ninashangaa vile ninavyoweza kumsaidia rafiki yangu wakati mama yake ni mgonjwa. Kushinda Kubinafsisha Anza kwa kugundua matukio ambayo ulibinafsisha mambo. Inaweza kusaidia kuziandika chini. Hisia nzito za hasira, kufadhaika au uchungu zinaweza kuwa ni kwa sababu ya kujilaumu mwenyewe. Muulize mpenzi wako usaidizi. Teka Nyara Mawazo II Wakorintho 10:5 Yatafakarini Yaliyo Kweli Wafilipi 4:8 Badilisha: (k.v.) “nina uhakika si kosa langu.” Na: “Ninaweza kuwa nilichangia shida hiyo, lakini ninahitaji habari zaidi kabla ya kukubali uwajibakaji kabisa.” Badilisha: Na: Badilisha: Na:


Page 85 4.Ujumlishaji: Masaibu ya zamani huwa bashiri ya maisha ya usoni. Ufafanuzi Mtu anayejumlisha huamini kwamba matukio ya zamani yatabashiri maisha ya usoni. Hao uchukulia kwamba chochote kilichofanyika zamani kitafanyika tena. Haya ni maoni ya kiamuzi ambayo hayapagui vya kutosha. Ni mtindo wa kufikiria wa kujiangamiza mwenyewe ambao huzuia uaminifu. Inaweza kufaidisha mtazamo wa kutazamia mabaya. Imani hiyo husema kwamba hakuna kitu kitachakobadilika, au kubadilika kwa mtu yeyote yule. Hii ni fikra mbaya kuwadia maisha ya usoni. Njia kama hiyo ya kufikiria inahusishwa na shaka, hofu na kutokuwa na usalama. Kuna ubunifu mdogo unaonekana na watu wengine hupuuzwa kwa urahisi. Usuli Kuzoea mtindo huu wa kuwaza huanza katika mazingira ya nyumbani wakati inapoundwa na mzazi mmoja au wote. Inaweza pia kusababishwa wakati ulishughulikia masikitiko ya uchungu wa zamani peke yako. Kweli Kilichofanyika zamani si lazima kifanyike tena. Vitu vinaweza kuwa tofauti na hata vyema, ijapokuwa inaweza kuhitaji bidii ili mabadiliko hayo yafanyike. Wakolosai 3: 3- 10 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu ulifichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi:..... ….. mstari wa 10 Mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. Athari kwa ndoa Fikra hukua ambayo husema “Haijalishi tunachofanya, hatutawahi kusikilizana.” Wanaojumlisha hushikilia machungu, kushindwa, na kukataliwa kwa zamani na kuzitumia kama ushahidi wa fikra yao mbaya kuwadia maisha ya usoni. k.v. Kubishana mara moja na jirani lazima kumaanishe hatutakuwa na chochote cha kufanya nao. Mfano wa Ujumlishaji Kula kitu ambacho hakijaruhusiwa kwa lishe mpya Jibu la mwenye kujumlisha ni:- Nilijua kufuata lishe hii itakuwa vigumu sana. Sitaweza kufanya hivyo. Lishe hii haitanisaidia na chochote. Kula kwa kufuata maelekezo haifanyi kazi kamwe. Matokeo ya jibu hilo:- Utawacha kujaribu, utajilaumu mwenyewe, utakula vibaya zaidi. Jibu la kweli zaidi linaweza kuwa Ninadhibiti vile ninavyokula na ninachagua kama nitakula au sitakula. Lishe hii inanitia moyo wa kula vyema zaidi na itaongeza kuwa bora. Ijapokuwa sikuifuta jana, nitaanza tena sasa. Kushinda Ujumlishaji Anza kwa kutambua ni mara ngapi unatoa ujumbe huu na utoe mifano. k.v. Teka Nyara Mawazo 2 Wakorintho 10:5 Yatafakarini Yaliyo Kweli Wafilipi 4:8 Badilisha: (k.v.) “Sijawahi kuwa na alama nzuri, kwa nini nishughulike? Sitawahi kuwa mwanafunzi mzuri.” Na: “Alama zangu za chini hapo zamani pengine zilikuwa kama matokeo ya kutosoma vizuri. Ninaweza kujifunza jinsi ya kusoma na kwa kutia bidii niongeze alama zangu.”


Page 86 Badilisha: Na: Badilisha: Na: 5. Uwazaji wa Mhemko: Kuchanganya hisia na kweli. ‘Nikihisi jambo lazima liwe kweli’. Ufafanuzi Mtu ambaye anawaza kimhemko huweka hisia kwa kiwango sawa na kweli. Hisia, mawazo na kweli zinachanganywa zote na kweli kugeuzwa. Mke ambaye hawezi kuhisi kujali kwa mume wake kuhusu masaibu ya uchungu anaweza kumshutumu bila sababu kuwa hamjali. Msemo sahihi unaweza kuwa "sidhanii unanijali" au "ninahofia kwamba haunijali." Katika msemo huu mhemko wa kweli – hofu – uaminifu huonyeshwa. Usuli Masaibu ya kukua ni muhimu kwa kusababisha mtindo huu wa kufikiria. Kuishi na mzazi aliyeunda uwazaji wa mhemko hufanya iwe vigumu kwa mtoto kutofautisha kati ya hisia na kweli. Unaweza kuwa ulishuhudia kusalitiwa kwa mzazi mmoja mwingine. Wakati ahadi zilizovunjwa zinapitiwa kila mara utotoni, fikra ambayo inasema, "nitaamini wakati nitakapoini” hutokea. Unaweza kuwa umepitia mateso makali ya mhemko utotoni, kama vile dhuluma ya kimwili au kingono. Mtoto ambaye mara kwa mara halihisi hofu lakini hakupokea usaidizi wowote wa kushughulikia hofu hiyo, atakuwa mtu mzima anayepata kuwa ni vigumu kutofautisha kati ya hisia na kweli. Kweli Ijapokuwa niliihisi, inaweza kuwa si kweli. Hisia ni hisia, tosha. Si kweli. Wakati ninasema “ninahisi kwamba......” , kwa kweli ninaonyesha mihemko muhimu kama vile uchungu, hofu, au hasira. Ikiwa ni hivyo, ninahitajika kutambua hisia za kweli ni zipi na kisha kuzionyesha. Athari kwa ndoa Kuchanganya hisia na kweli inaweza kuleta balaa kwa ndoa. Mashitaka yanaweza kutambaa kwa misingi ya hisia wala si ushahidi. k.v. Ninahisi uwivu kwa hivyo mume/mke wangu lazima awe na uhusiano wa kando. Nyumba kama hiyo itatawalwa na hofu na kutoaminiana. Mpenzi hutatitizika sana. Mfano wa Uwazaji wa mhemko Mume au mke amechelewa nyumbani: Anayewaza kimhemko husema Ninajua akona mtu mwingine. Matokeo ya jibu hilo Wakati anapofika nyumbani ninafanya ni kana kwamba alikuwa na mtu mwingine, ninamshutumu, ninamshambulia, ninakasirika nina chuki. Ukosefu huu wa imani hutenganisha sana. Jibu la kweli zaidi linaweza kuwa Kuna ufafanuzi mwingi unaowezekana wa kuchelewa huku. Wakati mume, au mke wangu, anapofika nyumbani ninahitajika kusema ninakuwa na wasiwasi wakati anapochelewa na ninakuwa na hofu kwa sababu ya sababu yake ya kuchelewa. Kushinda Uwazaji wa Mhemko Kubali ukweli wa kuwa hisia zina sehemu yake lakini haziwezi kuchukua nafasi ya kweli. Tambua matukio ambayo uwazaji wa mhemko yaliruhusiwa kutawala. Mruhusu mpenzi wako kuzungumza kuyahusu na wewe. Teka nyara mawazo mabaya na ufikirie kuhusu majibu ya kweli.


Page 87 Teka Nyara Mawazo II Wakorintho 10:5 Yatafakarini Yaliyo Kweli Wafilipi 4:8 Badilisha: (k.v.) “Hivyo ndivyo ninavyohisi.” Na: “Hisia zangu ni muhimu, lakini haziendani na kweli.” Badilisha: Na: Badilisha: Na: 6. Udhalilishaji; Kukataliwa kwa hisia zinazohusishwa na matukio muhimu ya maisha au masuala. Ufafanuzi “Haijalishi” wakati mtu hasipoonyesha au kukubali mihemko yao hao hawatarajii wengine wawe na hisia. Hata wakati wa matukio makubwa ya maisha, mhemko kiasi kidogo huonyeshwa au kutarajiwa. Wadhalilishaji wana shida ya kujua au kupitia mihemko kando na hasira. Wanaposhinikizwa kuwasiliana wanatoa kweli, maoni na sababu badala ya kushiriki mahitaji yao au hisia. Watakataa kwamba hakuna kitu kibaya au kwamba kuna kitu kinachowasumbua. Wanaweza kuweka bidii ili kuweka sura nzuri kwa vitu. Wanaweza kuonyesha kutovumilia wale wanaoonyesha hisia kwa urahisi. Usuli Wadhililishaji mara kwa mara hutoka kwa nyumba ambazo mahitaji ya kibinafsi hupuuzwa na kutozingatiwa. Ili kustahimili uchungu, wamejifunza kunyamaza na kufanya kana kwamba hakuna chochote kibaya. Mtu kama huyo anaweza kuwa alihimizwa kukataa mahitaji yao wenyewe, ambayo hukuza kupoteza kuhisi hisia zao wenyewe. Wanaweza kuwa wanajitegemea au wanajitosha na waliona mtindo huu kutoka kwa wale waliyo karibu nao. Kweli Baadhi ya matukio ya maisha ni makubwa na yanahitaji majibu ya mhemko au ya kitabia. Athari kwa ndoa Wadhililishaji mara kwa mara huwaacha wapenzi wao wakihisi wapweke, wanaotatizika na wenye uchungu, haswa wakati wa matukio mabaya wakati hawaonyeshi hisia zozote. Wanakataa kwamba kuna kitu chochote kinachowasumbua na si wazuri kwa kukubali uchungu kwa wengine. Mfano wa Udhalilishaji Uchunguzi wa kimatibabu huonyesha shida kubwa ya kiafya Jibu la mdhalilishaji ni Niko sawa, usiwe na wasiwasi. Matokeo ya jibu hilo Kutoweza kufikiria utofauti ambao habari hii imenisababishia pamoja na wale waliyo karibu nami. Wale ambao wananijali huwachwa wakiishughulikia peke yao. Jibu la kweli zaidi linaweza kuwa Hii ni habari mbaya. Ninasikitika na ninahuzunika pia, na nina hofu kuhusu maisha ya usoni. Ninawasiwasi kuhusu vile jambo hili litakavyo badilisha maisha yangu lakini ninajua Mungu na familia yangu na marafiki wangu tunaweza kutoboa na kufanya kila fursa kuwa nzuri.


Page 88 Kushinda Udhalilishaji Faraja itahitajika kwanza kwa uchungu wa mahitaji ambayo hayakufikiwa na kisha itawezekana kutambua kwamba kuitikia kwa mhemko mihemko ya uchungu ni jambo nzuri la kufanya. Uhakikisho utahitajika wa kuonyesha mihemko si sawa na kutokua na kiasi. Kumwamini mpenzi wako kutaruhusu mdhalilishaji kuanza kusema hisia zake. Wazo ambalo huonyesha mhemko kuwa ishara ya udhaifu linaweza kutekwa nyara na kuchagua majibu mazuri ya kutambua na kukubali hisia. Teka Nyara Mawazo 2 Wakorintho 10:5 Yatafakarini Yaliyo Kweli Wafilipi 4:8 Badilisha: (k.v) “Hii humfanyikia kila mtu; nitatoboa.” Na: “Ninapokuwa nikihisi uchungu, kuomboleza uchungu huo, na kupokea faraja kutoka kwa Mungu na wengine, nitaweza kutoboa." Badilisha: Na: Badilisha: Na: Jinsi Mitindo hii Sita ya Mawazo Inavyoweza Kuonyeshwa Ulinganishaji John Smith amefanya kazi kwa kampuni kwa miaka tatu iliyopita. Amepokea taarifa kwamba kwa sababu ya ugumu wa kiuchumi, kampuni hiyo itakuwa ikiwafuta kazi wafanyikazi 400, na yeye ni mmoja wao. Je! Ni aina gani ya mawazo ambayo John anayo ya kuitikia habari hizi? "Akitofautisha": “Kwa hivyo uamuzi ni huo - kuachishwa kazi. Ikiwa hawanitaki, hivyo pia mimi siwataki. Hapo ndipo mwisho wa kampuni hii!" "Akiongeza chumvi": “Hili ndilo jambo mbaya linaloweza kufanyika! Maisha yangu yamekwisha! Nimeisha. Nitafanya nini?" "Akibinafsisha": “Nilijua mkubwa wangu hakunipenda. Amekuwa akisuburi nafasi ya kunitoa. Ni nini nilichofanya vibaya?” "Akibinafsisha": “Hii ilikuwa ifanyike hivi karibuni au baadaye. Kila wakati hii huonekana kunifanyikia-- sitawahi kupata kazi ya kudumu." "Akiwaza kimhemko": “Kuna jambo lingine linaloendelea hapa. Hii si kwa sababu ya ugumu wa kiuchumi tu, ninahisi kana kwamba hatupati ukweli wote hapa. Nimekasirika sana kwa sababu ya hii." "Akidhalilisha":


Page 89 “Si jambo kubwa, mambo haya hufanyika. Sitaki kuyazungumzia. Kilichofanyika kufanyika--hakuna chochote mmoja wetu anaweza kufanya.” Kuwa huru Ni muhimu kutambua ni mitindo gani tunayogangana nayo. Mojawapo inaweza kuwa kubwa au kunaweza kuwa na visehemu vinavyopata mizizi. Kukubali kwa mpenzi wetu wa ndoa kwamba tunatambua mazoea ya kufikiria kwa njia fulani, na kuuliza usaidizi wa kushinda matokeo mabaya na kuona ukweli, ni mwanzo mwema kabisa. Ni vigumu sana kusahihisha peke yako. Unaweza kuwa umetambua mtindo mmoja wa kufikiria unaotawala kwako na mwingine kwa mpenzi wako. Wakati mwingine mchanganyiko wake unaweza kuleta dhiki. Mdhalilishaji na mwongeza chumvi wakiishi pamoja watapitia shida kadhaa, kwa mfano. Mume kumwonyesha mke ukweli wa hali, au mke kumwonyesha mume kwa njia ya ungwana na ya kuelewa, inaweza kuleta mabadiliko ya kufikiria kwamba malalamiko mabaya ya kukosoa yatafanya kazi. Kila mmoja anahitaji kutambua kwamba kushinda mawazo mabaya ni mapambano ya kweli ambayo yatahitaji usaidizi na kuelewa. Wakati wa Maharusi Kushiriki Kumpenda na kumjali mpenzi wako ndiyo nia yako ya kusaidia kushinda mawazo mabaya. Mnapokuwa mkizungumza, epuka lawama zozote za kukosoa au mazoea ya kukosoa vibaya. Kushinda mawazo mabaya kutajumuisha kuamini usaidizi wa Mungu na usaidizi wa mume wako, mke wako. Thibitisha usaidizi wako sasa. Zungumza kuhusu usaidizi upi kutoka kwa mpenzi wako ambao unaonekana kukufaa wakati umeitikia hali fulani vibaya. je! Ni nini ambacho hakikusaidii na kinaonekana kama ukusoaji au kuvunjwa moyo? Hii inaweza kujumuisha wakati, eneo, siri, toni ya sauti, mguso, chaguo la maneno. Nia na mbinu zinazotumiwa ni muhimu. Kuchukua muda huu kujenga imani itakuandaa kwa Mkutano wa Timu ya Ndoa wakati utaangalia mitindo ya kuwaza iliyotambuliwa. Rudi kwa Kikundi Someni pamoja 1 Wakorintho 13:4-13 Ombeni pamoja mkimuuliza Mungu awape nguvu ya kuimarisha upendo wenu. Zingatia ufafanuzi mmoja wa upendo kutoka kwa kifungu hiki ambacho ungetaka kuonyesha zaidi katika ndoa yako. Mshukuru Mungu kwa upendo unaopokea.


Page 90 MKUTANO WA TIMU YA NDOA Kwa kuongezea uratibishaji wa kalenda yoyote, upangaji, kukiri na kusamehe, au utathmini wa lengo unalohitaji kufanya, tunapendekeza yafuatayo • Shiriki matokeo ya kidadisi cha mawazo mabaya. Matokeo yake yanaweza kuwa yameangazia tabia moja au zaidi ya mawazo mabaya. Kwa kuanza na waume, zungumzeni kuhusu mtindo wa kwanza wa mawazo mabaya ambayo ungependa kuona yamebadilika kwako ukitumia maneno kama: Ninagundua kwamba hii ni shida. Ningependa sana Bwana anisaidie nibadilike. Kumbuka tukio kama mfano wa jambo hili. Je! Matokeo ya hatua yako ilikuwa nini? Hatua ya kweli zaidi ingekuwa nini? • Zungumzia kuhusu baadhi ya masaibu ya utotoni ambayo yalichangia mitindo hii ya kuwaza. Uliona aje mitindo hii katika familia yako mwenyewe? Je! Ulipitia nini ambayo ilisababisha mitindo yako mbaya ya kuwaza? Je! Kuna uwezekano wowote uliofafanuliwa katika sehemu ya Usuli ya mitindo yako ya kuwaza inayoonekana kuwa kweli. • Ikiwa kumbukumbu zimeanza kutambuliwa na kuonyeshwa, tambua hisia zinazotokea na toa au pokea faraja kwa maumivu au uchungu. Kumbuka kuitikia kimhemko kwa maonyesho yoyote ya uchungu na ya huzuni. • Uliza msaidiane kushinda mitindo hiyo inayohusiana na mawazo. Saidianeni zaidi kuelewa usaidizi huo unafanana aje. Ni nini unachoweza kuambiwa? Kinaweza kusemwa aje? k.v. “Wakati ninaongeza chumvi- kutokua na kiasi kwa jambo fulani – inaweza kunisaidia ukisema kitu kama;- “ninataka ujue ninajali kwamba jambo hili limekufanyikia. Ninadhania unaliongezea sana. Ninataka nikusaidie kushughulika na hali hii kama ilivyo. Ninawezaje kukusaidia?” • Fungeni wakati wenu kwa kuomba kwamba Mungu awape ukweli Wake na uwezo wa kuteka nyara uwongo wa aina yoyote ili kumtii Kristo. Ombeni kwamba Mungu awawezeshe kushinda mtindo huo mbaya wa kufikiria ambao mnapapambana nao sana.


Page 91 Usahibu Kuwa Hali ya Maisha Kuwa Marafiki, Wapenzi na Watakatifu. 1Timotheo 4:7-8 “.....nawe ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ule utakaokuwapo baadaye.” Nidhamu ya Usahibu Kila moja ya vikao hivi vilivyoshughulikiwa hadi sasa vimekua vikiangazia nidhamu fulani ya usahibu inayohitajika ili usahibu ufaidike na kwa hivyo kukua. Kwa ndoa zetu kubakia nzuri, tabia fulani, zingine zilizogunduliwa upya zitahitaji kuwa sehemu kuu ya maisha yetu. Nidhamu si neno ambalo tuko sawa nalo siku hizi. Walakini nidhamu, inaweza kutengeneza tabia, na ni tabia hizi mpya ambazo tumekuwa tukizigundua ambazo zinaweza kubadili ndoa zetu. Kwa hivyo tunahitaji nidhamu, si kwa ajili yake tu, bali ni kwa sababu inaleta kukua na inaongeza uhusiano wa karibu. Mfano mmoja wa nidhamu ya usahibu ni kudumisha kila wakati ufahamu wa mahitaji tatu ya juu ya mhemko wa mume au mke wako na kumsikiliza kila wakati. Kuongeza Usahibi wa kiroho Endeleza usahibu na Mungu ukiwa peke yako na mkiwa pamoja. Mungu hutupa neema Yake kwa wingi, na kwa neema Yake tunaitikia upendo Wake na kushiriki tunachopokea na wengine. Kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka tena tunaweza kuishi ndani Yake, tukipata nguvu, hekima na upendo Wake. Kwa kuongeza kuchukua muda kila siku ukiwa peke yako kwa maombi na kusoma Biblia, pia unaweza kuchagua kuweka muda kando, pengine mwisho wa kila siku, kusoma pamoja mistari kadhaa ya Biblia na kuomba. Kuomba pamoja kwa utulivu kunaweza kuwa lengo la kwanza. Ibada ya Kamwe Sipo Peke yangu inaweza kukusaidia kuzingatia mawazo yako unapokua ukikuza usahibu wa kiroho. Shukrani. Zaburi 103:2 “Eh nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usizisahau fadhili zake zote.” Kumwonyesha Mungu shukrani kwa yale yote aliyokupa itaongeza ufahamu wako wa upendo Wake kwako. Shukrani hutulinda kutokana na roho ya kukosoa vibaya. Pia hutulinda kutokana na kuwa watu wa kuhukumu. Shirikianeni shukrani kwa urafiki wenu na Yesu, msamaha Wake, na Zawadi Yake ya Roho Mtakatifu, na ukweli unaobadilisha maisha kwenye Biblia. Kukiri 1 Yohana 1:9 na Yakobo 5:16 Muda mwingi ukipita kati ya muda wa kukiri basi maumivu na uchungu yataendelea kuongezeka. Tunapokuwa tukipitia ukweli wa mstari kutoka Yohana na Yakobo basi uponyaji utafanyika. Daima fahamu imekuwa muda upi tangu ulipokiri. Msamaha Hii ni tabia ya kuachana na hasira na uchungu. Katika ndoa tutaumizwa kwa njia tofauti. Kunaweza kuwa na masikitiko ya kawaida. Pia kunaweza kuwa na matukio muhimu zaidi ya uchungu ambayo huleta uchungu mwingi. Kujifunza tabia ya kusamehe wakati kukiri kwa kweli kumefanyika itaongeza upendo.


Click to View FlipBook Version