The words you are searching are inside this book. To get more targeted content, please make full-text search by clicking here.
Discover the best professional documents and content resources in AnyFlip Document Base.
Search
Published by Relationship Press, 2023-05-31 17:10:52

Keeping Marriages Healthy in Swahili

Whole-life Discipleship

Page 92 Kuomba kunaoathiri Kuomba kwa Mungu kwa njia ya kuathiri na mpenzi wako wa ndoa itashughulikia hofu. Tendo la kuumiza haliwezi kukiriwa na kusamehewa tu, bali kutaka kubadilisha itakuwa dhahiri pia. K.v. Bwana, ninataka kuhisi zaidi, kujali zaidi na kumsaidia....... (mume/mke wangu); tatafadhali nionyeshe ni aje. Kuanzisha maombi kama hayo kila wakati itasaidia na kuhimiza kila mmoja wenu. Kufariji Mathayo 5:4 “Heri wenye huzuni; maana hao watafarijika". Uhusiano wa ndoa ni chanzo cha kimbilio na usalama. Mahali ambapo mlango unaweza kufungwa kwa muda ulimwenguni, na mahali ambapo kuna faraja badala ya ukosoaji au ushauri. Mahali ambapo uchungu unaweza kuonyeshwa, ambapo kuna kusikilizwa, na mahali ambapo maneno na mguso unaweza kuleta faraha na uponyaji. Toa Neema Waefeso 4:29 “Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.” Hii ni kuhusu kujijenga wenyewe na kutoa shukrani kwa ajili ya yule mwingine. Tunapaswa kuwa waangalifu juu ya vile tunavyozungumziana, haswa mbele ya wengine.


Page 93 Kuongeza Usahibu wa Urafiki Marafiki hupata nafasi ya kuwa na yule mwingine. Kufanya mkutano wa Timu ya Ndoa kuwa kujitolea la kila wiki inaweza kuhitaji bidii nyingi mara ya kwanza, lakini hiki ndicho kifunguo cha kweli cha Kutunza Ndoa Vizuri. Ikiwa muda wa kuzungumza kuhusu masuala yote yaliyoshughulikiwa katika kitabu hiki umeachiwa nafasi, ikiwa hakuna mpango au lengo, basi kuna hatari ya kurudia tabia za zamani. Fanya kuchukua muda pamoja kuwa kipaumbele, kushiriki maslahi, kuwa na chakula cha mahaba kwa pamoja, na kupanga muda wa raha pamoja. Hizi zote ni muhimu. • Marafiki huponya machungu yasiyoepukika kupitia kufariji, kukiri na kusamehe. • Marafiki husema mahitaji yao kwa njia ya upendo - sio kwa kukosoa, sio kwa kulazimisha, sio kwa kunyamaza, na sio kwa udanganyifu. • Marafiki huonyesha shukrani kwa yule mwingine. Unapokuwa ukiangalia orodha ifwatayo chagua sifa za kitabia ambazo zinafafanua mume/mke wako (inapendekezwa 3 au zaidi). Onyesha shukrani yako kwa sifa hizo haswa za mpenzi wako. Hii itamaanisha sana ikiwa unaweza kutambua pia muda ambao unaweza kukumbuka sifa hii ikionyeshwa na ushiriki hiyo pia. 1. RIDHAA – tayari kutaka kupokea wengine bila masharti.(Warumi 15:7) 2. UANGALIFU – kutafuta muongozo unaofaa na unaostahili kabla ya kufanya maamuzi. Kuwa mwangalifu kwa majiribio ya kupotosha na kuangamiza na kuchukua hatua ya kukataa. (Mithali 11:14) 3. HURUMA – Kuhurumia machungu ya wengine na kuwa tayari kufanya chochote ili kuondoa uchungu wa wengine. (1 Petro 3:8) 4. KUTOSHEKA – Kufurahiya mali ya sasa badala ya kutamani mpya au ya kuongezea. Kujua kwamba furaha na amani ya ndani hazipatikana kwa mali au cheo. (1 Timotheo 6:6) 5. UBUNIFU – Kupata njia za kushinda vizuzi ambavyo vinaonekana haviwezekani. Kutambua matumizi ya kweli ya imani na maadili. (Warumi 12:12,21) 6. UAMUZI – Kukamilisha maamuzi magumu kwa misingi ya maadili, kanuni na imani na sio hali ya sasa tu. (Yakobo 4:15) 7. UTOFAUTI- Kudhibiti uhuru wako ndiposa usikosee mapendeleo mazito ya kibinafsi ya wengine. (Warumi 14:13) 8. KUTEGEMEWA – Kujifunza kuwa wa kweli kwa ahadi hata wakati magumu yanapokabiliwa katika kutekeleza wajibu. (Mathayo 5:37) 9. Bidii – Kuangalia kila kazi kama kazi muhimu, na kutumia nguvu zozote na umakini unaohitajika kuikamilisha. (Wakolosai 3:23-24) 10. UTAMBUZI- Kujua unachostahili kutafuta unapotathmini watu, shida na hali. Kuona matokeo ya usoni ya maneno na vitendo. Kuhisi. Kusema maneno mema kwa wakati mwema. (Waefeso 4:29) 11. UVUMILIVU (Kustahimili) – Kudumisha ahadi ya lengo wakati wa shinikizo. Kutambua na kuweka kando vizuizi. (Warumi 5:3-4) 12. MSAMAHA – Kukubali kushindwa kwa mtu na kuwa tayari kukubali na kusamehe makosa ya wengine. (Waefeso 4:32)


Page 94 13. UKARIMU – Kujifunza jinsi ya kuwa kiongozi mwenye hekima na kuwa tayari kutoa kipimo cha mali, pesa au muda ili kuwasaidia wengine. (2 Corinthians 8:9, 9:7) 14. UNGWANA – Kujua kinachofaa ili kufikia mahitaji ya mhemko ya wengine. Kujifunza kuitikia mahitaji kwa ukarimu na kwa upendo. (Waefeso 4:2) 15. SHUKRANI – Kutambua manufaa ambayo wengine wameleta; kutafuta njia zinazofaa za kuonyesha shukrani ya kweli. (Waefeso 5:20) 16. TAKRIMA- Kujifunza kutoa mazingira ambayo yanawafanya wengine kuhisi wameshughulikiwa vizuri na wamekubaliwa. Kuwa tayari kushiriki maisha na wengine. (1 Petro 4:9) 17. UNYENYEKEVU – Kutambua kutoweza kukamilisha chochote ukiwa peke yako. Kuwadhamini wengine kwa michango yao ya matokeo mazuri. (Waefeso 4:2) 18. UVUMBUZI – Kuchukua hatua ya kuongoza na kuchukua uwajibikaji wa usaidizi na kuwahimiza wengine wanaohusika. Kutoa kwanza. (Luka 6:38) 19. UTIIFU – kuchukua mwenyewe matakwa na malengo ya wale wanaotumikiwa. (Wakolosai 3:22) 20. UPOLE – kuonyesha jinsi ya kupata haki ya kusikilizwa badala ya kuamuru kusikilizwa. Kutaka kutoa haki kwa maslahi ya wengine. (1 Petro 5:6) 21. SUBIRA – Uwezo na kutaka kukandamiza kukasirika wakati unapokabiliwa na kukawishwa au shida. Kukubali hali ngumu kama zimetoka kwa Mungu. (1 Wakorintho 13:4) 22. KUTOCHELEWA – Kuonyesha taadhima kwa watu wengine na muda wao kwa kutowaeka wakikusubiri. (Wafilipi 2:3-4) 23. KICHO – Hisia au tabia ya kuheshimu sana. Kutoa heshima. (Mithali 1:7) 24. KUWA NA KIASI – Zuia au kataa mawazo, maneno, na hatua. (Waefeso 5:18) 25. KUHISI – Kuwa mwangalifu kwa nia na magumu ya wengine. Kuangalia zaidi ya kawaida. Kujua jinsi ya kupeana maneno mazuri wakati mzuri. (Marko 8:17) 26. UAMINIFU – Kuwa na nia ambazo ni wazi. Kuwa na hoja halisi ili kunufaisha maisha ya wengine. (Warumi 12:9) 27. UKAMILIFU – kuzingatia vikamilifu maelezo muhimu ya kufaulu. (Yakobo 1:4) 28. STAHAMALA – Kujifunza jinsi ya kujibu ujinga wa wengine bila kukubali kiwango chao cha ujinga. (Wakolosai 3:13) 29. UKWELI - Kupata kibali cha wengine bila kuharibu kweli. Kukabiliana na matokeo ya makosa. Kusema ukweli wote. (Waefeso 4:25) 30. UADILIFU – Kujifunza kujenga viwango vya uadilifu wa kibinafsi ambayo itasababisha ubora na kunufaisha maisha ya wengine. (1 Timotheo 4:12)


Page 95 Marafiki huitikia mhemko na mhemko. Wakati mwingine tunapata hatujui jinsi ya kuweka kwa maneno kile kinachoendelea ndani yetu, haijilishi vile tunavyotaka kumjumuisha mume au mke juu ya vile tunavyohisi. Mume au mke, akitatizika kwa kuwa mpenzi wake anakosa kushiriki, anaweza kukosoa au kulaumu bila kuelewa kwamba, yule ambaye anapambamba na kuonyesha mihemko yao, kushiriki kama huko kunaonekana vigumu kufanya. Kutofautisha mihemko nyingi ambayo tunapitia hata kama ni kwa tukio moja, inaweza kusaidiwa kwa kukuza msamiati mkubwa wa maneno ya kuhisi. Kuangalia orodha kama hiyo ya maneno inaweza kutusaidia kuainisha na kufafanua ugumu wa mihemko tunayohisi. Mihemko 30 nzuri Shukrani Furaha Tumaini Uchangamfu Kupendwa Kueleweka Muhimu Kutulia Huruma Kufaulu Kushangaa Kuamua Ukarimu Ubunifu Kuridhika Msisimko Ufadhili Kusaidia Moyo Utulivu Kupumzika Kuridhika Matumaini Kuwaza Uhakika Kujaa furaha Mshangao Kupendezwa Mzuri Kuhimizika Mihemko 30 mbaya au ya uchungu Kusikitika Kushtuka Fedheha Shaka Kukataliwa Kughadhabika Kukasirika Kuaibika Kuhukumika Kuudhika Chuki Kuchanganyikiwa Kutatizika Majuto Huzuni Uwivu Kufa moyo Unyogovu Kuogopa Kutokuwa na furaha Upweke Kutokua na tumaini Hofu Aibu Kusumbuka Wasiwasi Kuomba msamaha Uchungu Hasira. Kutokuwa na maana Maneno yanapoendelea kutafutwa ili kufafanua mihemko na hisia ni muhimu kuangalia orodha hizi mara nyingi kabla ya kushiriki huko kuwa ihari. Kuongeza Usahibu kama Wapenzi Mungu ameumba usahibu wa kujamiiana kwa kusudi letu na kwa furaha yetu. Walakini wakati mwingine tumejua kusikitika kuhusu wakati wetu wa kujamiiana pamoja. Usahibu wa kujamiiana unaweza kuwa eneo la dhiki na suala la uchungu sasa kwa maharusi wengine. Wasiwasi, hofu, hasira au chuki inaweza kuhusishwa na uhusiano wa kujamiiana. Lengo la kuridhika sawa kingono linaweza kuonekana kama lengo ambalo ni ngumu kulifikia.


Page 96 Kuzungumza kuhusu mahitaji ya kujamiiana mara kwa mara huwa ni vigumu lakini kuwa wazi huwa rahisi wakati tunapobadilisha vile tunavyozungumza kuhusu uhusiano wetu wa kujamiiana. Ikiwa ngono inaonekana kama kitu tunachofanya, basi kwa urahisi inaweza kutathminiwa kama shughuli nyingine. k.v. Mara ngapi? au Ilikuwa aje? Ikiwa ngono inaonekana kama kitu ambacho tunacho basi itakuwa kitu tunachokisimamia au kukubali kwa masharti k.v. Wakati upambaji unapokwisha; au Ikiwa uko nyumbani wakati unaofaa wiki yote. Mizozo inaweza kufuata hila, kujadiliana au maharusi wanaogoma! Inasaidia aje kuzungumza kuhusu ngono kama jambo ambalo unashiriki. Usahibu wa kujamiiana unahusu kuwa na uhuru wa kujitoa vikamilifu kwa mume/mke wako. Tunapojitoa kwa yule mwingine kila mpenzi ujihisi amehifadhiwa na kuthaminiwa. Kuimarisha Mahaba Kutazamia muda wa pamoja wa usahibu wa kujamiiana huongeza mahaba, kama vile kuachana asubuhi na maneno ya kuonyesha tamaa ya kuwa pamoja mwisho wa siku. Zingatia kutoa wala si kuchukua: “Ninawezaje kuongeza furaha yako?" Peaneni kwanza kimhemko. Shiriki hisia, ponya machungu, sifa za tabia, julianeni hali ya siku. Ongezeni mguso usio wa kujamiiana. Zoezi linalojulikana kama ramani ya upendo hutoa fursa ya kuzungumziana kuhusu wakati wa pamoja wa kujamiiana. Ni vizuri kushiriki pamoja, pengine kucheka pamoja! Haitakuwa jambo lisilo la kawaida kwa ramani ya upendo wa mke kutaja kwanza siku kabla ya muda wa usahibu wa kujamiiana. k.v. Kama kiongozi cha Jumamosi usiku, kuja nyumbani wakati onaofaa Jumatano. Tule chakula pamoja Alhamisi na tuzungumze pamoja. Twende nje pamoja Ijumaa jioni. Hii haistahili kuchanganywa na hila au kujadiliana. Muda uliochukuliwa pamoja jioni hizo tatu zinazotangulia Jumamosi ni za kumpatia mke mahitaji ya mhemko, kumwandaa ili aweze kutoa vizuri kwa mume wake. Unapokuwa ukijaza ramani ya upendo inayofuatia kumbuka kwamba ubia wenu ni wa kitofauti na furahiya uhuru ambao mawazo hutoa. Ramani ya Upendo “nao watakuwa mwili mmoja” Mwanzo 2:24 Vizuizi vya usahibu wa kujamiiana Vizuizi vinne vikuu kwa usahibu wa kujamiiana vimeshughulikiwa katika zoezi hili 1. Kutokuwa wazi/kutowasiliana – Ngono si suala rahisi la kujadili kwa maharusi wengine; kuepuka suala hili huwaacha maharusi wengi katika mzunguko wa kuwa wazi kidogo, chuki na shida. 2. Shughuli mbaya ya kupata badala ya kutoa – kwa bahati mbaya wengi wetu (haswa wanaume) walikua na wazo kwamba ngono ni kitu kinachostahili kuchukuliwa, kupatikana au cha hila; kwa hivyo sanaa ya kujitoa kwa yule mwingine ni geni kwetu na mbaya.


Page 97 3. Uchoshi – Kukosa ubunifu/upya - Kitu kimoja huzaa ridhaa na hisia za uwajibikaji, wakati ubunifu huonyesha uvumbuzi, tamaa na marajio. 4. Kukosa Matarajio na Matazamio - "kama mwanaume (au mwanamke) anavyofikiria ndivyo alivyo!" Mithali 23:7 Akili yako ni rasilimali muhimu sana ya kujamiiana; kujifunza kutarajia kiakili muda wa kuwa pamoja na mpenzi wako hujenga msisimko, ubunifu na tamaa. Kila mpenzi anastahili kujibu ifwatayo :- Kwa maoni yangu, usahibu unaofaa wa kujamiiana na mpenzi wangu ni pamoja na”: RAMANI YAKO YA UPENDO. Jumuisha vitu muhimu vya kubinafsi vinavyohusiana na wakati, eneo, mavazi na maandalizi ya mahaba. Utataka kuzingatia matakwa ya kibinafsi yanayohusiana na uvumbuzi, unyegereshano, mikao na “baada ya unyegereshano”. 1 7 2 8 3 9 4 10 5 11 6 12


Page 98 Chagua muda wa kibinafsi na mahali pa kubadilishana ramani zenu za upendo.. Muda wa Maharusi Kushiriki utafaa, au unaweza kupendela kupanga wakati mwingine. Mnapobadilishana ijadili kama uwezavyo. Fafanua na ujibu maswali inavyostahili. Utaendelea kuwa sawa kufanya hivi unapoendelea kurudia zoezi hili. Panga mapema mara mbili ya usahibu ili kukamilisha Ramani zote za Upendo. Kila moja inastahili kumweka huru yule mwingine ili kukamilisha kila ramani ya upendo ambayo yuko sawa nayo sasa. Ni muhimu kutozizitiza, au kumsukuma yule mwingine. Usahibu wa Ndoa ni uhuru wa kujirishika kabia na mtu yule mwingine; mwili, nafsi na roho. Kukamilisha ramani ya upendo ni sehemu ya kuonyesha uhuru huo kupitia kutoa na kupokea kutoka kwa yule mwingine. Mume anastahili kumpa kwanza mke wake kwa kukamilisha Ramani Yake ya upendo. Kisha mke atachagua wakati mwingine wa kumpa mume wake kukamilisha Ramani yake ya Upendo. Ipangie ili ninyi wote muweze kuitazamia siku nzima. Chukua wakati ukitazamia raha ya kuwa kitu kimoja kimwili. Waziwazi jishiriki kabisa na yule mwingine. Kuandaa, kujadili na kukamilisha ramani ya upendo kunaweza kuwa sehemu ya kawaida ya usahibu wa kujamiiana pamoja na nyakati zingine za ihari za kuja pamoja kingono. Usahibu, Hali ya Maisha Kubadilisha ndoa zetu kuwa mahusiano ya ajabu vile Mungu alivyoyaumba yawe, tutahitaji kujifunza nidhamu ambayo kosi hii imetuletea kutika maisha yetu pamoja. Ni tamaa yetu kwamba tayari unapitia umoja mkubwa katika vipimo hivi vitatu, kimhemko, kiroho na kimwili. Itasaidia kuangalia tena utathmini uliyotoa kwa kila eneo moja ya maeneo haya ya ndoa yako katika Kikao cha Kwanza ukurusa wa 7 Katika maisha yetu yote ya ndoa, tuna lengo la kuongeza usahibu katika kila eneo. Majibu yako kwa seti ifwatayo ya maswali itakupa ufafanuzi zaidi, na nafasi ya kushiriki jinsi usahibu unaweza kuongezwa kwa siku, wiki, miezi na miaka zijazo. Kwa makini soma kila moja ya maswali kumi na tano na utie mviringo kwanzia namba 1- 5 ambayo inawakilisha sana masaibu yako.


Page 99 ORODHA YA USAHIBU WA NDOA Nakataa Kabisa 1; Ninakataa 2, Sikatai/sikubali 3; Nakubali 4; Nakubali Kabisa 5 1 Mpenzi wangu anasaidia na kuhimiza katika maeneo ya imani na maadili ya kibinafsi 1 2 3 4 5 2 Tunaonekana kuwa sawa kupeana usikivu kamili wakati tunasikiliza au kuzungumza. 1 2 3 4 5 3 Mpenzi wangu anasikiliza na anahisi mahitaji yangu katika eneo la unyegereshano wa kujamiiana. 1 2 3 4 5 4 Tunaonekana kukiri kwa uaminifu ikifwatiwa na msamaha wa kweli wakati mmoja wetu amemuumiza mwingine. 1 2 3 4 5 5 Wakati ninashiriki hisia zangu, mpenzi wangu uzithamini na anatoa dhibitisho la kuelewa. 1 2 3 4 5 6 Niko sawa kuwasiliana na mpenzi wangu tamaa zangu za kujamiiana na mapendeleo yangu. 1 2 3 4 5 7 Ni muhimu kwetu kushiriki pamoja baadhi ya ndoto na matumaini yetu ya mbali – hata kama zinaonekana za upuzi! 1 2 3 4 5 8 Mpenzi wangu ni mzuri kushiriki vitu hivi viwili, shukrani na kunena upendo. 1 2 3 4 5 9 Tunaonekana kupatia kipaumbele nyakati za kila wakati za kuzungumza na kuwa pamoja vizuri. 1 2 3 4 5 10 Tunaonekana kukumbuka kila wakati nyakati nzuri na baraka tulizozifurahiya. 1 2 3 4 5 11 Ninakumbuka nyakati maalum wakati mpenzi wangu na mimi tulishiriki pamoja mihemko nzito, kama vile kuomboleza, huzuni, furaha. 1 2 3 4 5 12 Nimeridhika sana na kuhisi kwa mpenzi wangu katika kufikia mahitaji yangu ya kujamiiana. 1 2 3 4 5 13 Kwa masuala mengi muhimu yanayohusiana na maadili na imani, mpenzi wangu na mimi tunakubaliana mara kwa mara. 1 2 3 4 5 14 Kusema mahitaji na tamaa zangu kwa mpenzi wangu kuhusu uhusiano wetu ni kawaida kwangu. 1 2 3 4 5 15 Nimeridhika na mazoea ya mpenzi wangu ya kuanzisha nyakati za pamoja za kujamiiana. 1 2 3 4 5


Page 100 KUFASIRI ALAMA ZAKO: Imani na Maadili ya Kibinafsi: Ongeza majibu yako kwa maswali nambari 1, 4, 7, 10, 13 na uweke alama zako hapa: 0 5 10 15 20 25 Urafiki: Ongeza majibu yako kwa maswali nambari 2, 5, 8, 11, 14 na uweke alama zako hapa: 0 5 10 15 20 25 Uhusiano wa karibu wa Kimwili: Ongeza majibu yako kwa maswali nambari 3, 6, 9, 12, 15 na uweke alama zako hapa: 0 5 10 15 20 25 Je! Kuna maoni yoyote mapya au maswali yaliyokujia akilini ulipokuwa ukikamilisha orodha hii?


Page 101 Wakati wa Maharusi Kushiriki Shirika na yule mwingine njia tatu ambazo ungependa kuendelea kuongeza masaibu yako ya usahibu. Kuwa dhahiri kuhusu vile hatua hii ya mpango inaweza kufikiwa na wakati kila moja ya mambo uliyoorodhesha itafanyika. Mpango wa Hatua ya Usahibu Njia tatu ambazo ningependa kuimarisha uhusiano wetu. Njia tatu ambazo mume/mke angependa kuimarisha uhusiano wetu.


Page 102 Mpango wetu wa Hatua ya Usahibu Njia tatu tunazopanga kuimarisha masaibu yetu ya usahibu wa ndoa pamoja: Nini? Aje? Lini?


Page 103 Rudi kwa Kikundi Ili kushiriki vikamilifu yale yote yaliyoshughulikiwa, hata katika kikao hiki cha mwisho, itachukua zaidi ya Mkutano mmoja wa Timu ya Ndoa. Kutakuwa pia na thamani kubwa kurudia vikao vile vingine vyote kwa wiki zijazo, ili kuchunguza kwa kiwango cha ndani kilichoshughulikiwa, na kupitia manufaa katika uhusiano wako. swali la ‘je! Mungu anataka nini na ndoa tangu?’ ni ya maana sana na ni ya muhimu kuuliza. Upendo mwingi wa Mungu kwa kila mmoja wetu ndiyo msingi wa vile tulivyo. Kusudi Lake la ndoa ni kwamba tunastahili kushirikiana na Yeye kwa kuwapenda waume wetu, kwa kuwapenda wake zetu. Upendo Wake ndiyo chanzo, na kusudi la ndoa zetu. Maombi Asante kwa mpenzi wangu wa ndoa. Asante kwa yale tuliyoyashiriki na yale yote uliyotufunza kuhusu jinsi ya kuboresha ndoa zetu. Asante Bwana kwa kuwa unajali mahusiano ya ndoa na kwamba tunajua kwamba yetu ni maalum kwako. Tunaomba kwamba upendo wetu utaendelea kukua na kubarikiwa na wewe.


Page 104 Mkutano wa Timu ya Ndoa: Zungumzeni kuhusu uratibishaji wa kalenda yoyote, upangaji, utathmini lengo, au maonyesho ya shukrani ambayo unastahili kufanya. • Tumia muda wa leo kuweka Mikutano ya Timu ya Ndoa kwenye shajara. Ikiwa mmekuwa mkipata kwa ajili ya kozi hii jioni moja kila wiki inawezekana kuendelea kutunza jioni hii moja kila wiki kwa ndoa yako. Kumbuka kwamba kushiriki nyakati za furaha ni muhimu pia na utataka kupanga mapema wakati wenu. Yafuatayo ni mawazo ambayo yatahitaji zaidi ya Mkutano mmoja wa Timu ya Ndoa ili kuishughulikia. • Kwa kurejelea orodha ya 2 ya maneno ya mhemko, kwa kupokezana tambua baadhi ya hisia ambazo kila mmoja wenu anapitia kwa sasa. Hii inaweza kuwa inahusiana na kazi, familia, kanisa au ndoa. Kuanzisha msamiati wa maneno mazuri ni muhimu kama kuwa na uwezo wa kufafanua mihemko ya uchungu. Utahitajika kuangazia hiyo mnaposhiriki. • Kwa kutumia orodha ya sifa za tabia, chagua tatu zinazomfafanua mume wako au mke wako na uzishiriki na yeye. Kumbuka kutambua nyakati maalum wakati sifa hizi zilionyeshwa. • Kamilisha sentensi hii: “Mambo tatu muhimu ninayotaka kukumbuka sana na kuyafanya kutoka kwa Kutunza Ndoa Vizuri ni ...."


Page 105 Shiriki ulichoandika na mpenzi wako. Kisha muulize mpenzi wako: Ni mambo magani tatu ambayo ungetaka sana nikumbuke na kuyafanya kutoka kwa Kutunza Ndoa Vizuri?" Kisha andika hizo tatu hapa: • Endelea kushughulikia mipango yenu ya usoni ya kuongeza usahibu wa ndoa iliyoanzishwa Wakati wa Maharusi Kushiriki. Utapata inasaidia kuandika chini vitu vya kwanza unavyotaka kuanza kutoa muda, na kupanga ni lini utafanya hivyo. Chagua moja kati ya hizi ili uanze kuishughulikia katika mkutano huu. • Badilishaneni ramani ya upendo na mpango ili nyote mzikamilishe. • Mwisho wa Mkutano wa Timu ya Ndoa, funga na Ombi la Upendo Kamili, ukurasa wa 66. Muulize Mungu akuwezeshe kuwa mwema zaidi, ili uweze kuonyesha upendo zaidi kuwadia mume au mke wako.


Page 106 Kuhusu huduma ya Maisha ya Usahibu Na Mtandao wa Amri Kuu Huduma za Usahibu wa Maisha (ILM) ni huduma ya kufunza na ya msaada ambayo madhumuni yake ni kusaidia kuendeleza Huduma zinazoendelea za Amri Kuu duniani kote. Huduma za Amri Kuu hutusaidia kumpenda Mungu na majirani wetu kupitia kuimarisha usahibu wetu na Mungu na wengine katika mahusiano ya ndoa, familia, kanisa na jamii. Maisha ya Usahibu ipo ili kuhudumia Makanisa ya Mtandao wa Amri Kuu, Huduma, na Viongozi wa Wakristo. Mtandao huu unawajumuisha wachungaji na viongozi wengine wa huduma, makanisa, huduma ya kanisa na ubia wa madhehebu wanaowakilisha zaidi ya makanisa 35,000 nchini Marekani na mengine mengi ulimwenguni kote. Kuhudumia Mtandao wa Amri Kuu, ILM imeanzisha timu inayowajumuisha: • Wakufunzi wa Jamii Wanaosifiwa waliyojitolea kusadia makanisa kuanzisha huduma zinazoendelea za Amri Kuu; • Ushirikisho wa Wataalamu kutoka kwa usuli wa huduma na Wakristo wengine wataalamu, wanaosaidia kwa kuanzisha uchunguzi, ukufunzi na msaada; • Watangazaji wakristo, wachapishaji, vyombo vya habari na washirika wengine wakishirikiana ili kuona huduma za Amri Kuu zikiongezeka; • Wafanyikazi wa makao makuu wanaotoa upangaji mbinu, uratibishaji na usaidizi. Vile Huduma za Usahibu wa Maisha Uhudumia Mtandao wa Amri Kuu 1. Wagalatia 6:6 Mandari ya Viongozi wa Huduma ILM hutoa mandari ya kipeke ya siku mbili ya "Wagalatia 6:6" kwa wahudumu na maharusi wao ili kujitia nguvu upya na kuimarisha tena na kudhibitisha vipaumbele vya huduma na familia. Malezi na vyakula vya mandari hii hutolewa kama zawadi kwa viongozi wa huduma na ubia wanaothamini. Mandari thelathini hadi arubaini hufanywa Marekani yote, Uingereza na Uropa kila mwaka. 2. Ushirikiano na Madhehebu na Huduma Zingine Madhehebu mbalimbali na huduma zimeshirikiana na ILM ili kuwaandaa viongozi wa huduma kupitia Mandari ya Wagalatia 6:6 pamoja na ukufunzi wa mbinu na msaada wa kweli wa huduma inayoendelea. Ushirikiano huu huwezesha mashirika ubia kutumia utaalamu wa wakufunzi wa ILM na msaada ili kuendeleza mfumo wa huduma ya Amri Kuu katika kiwango cha kawaida. ILM pia hutoa mpangilio wa usaidizi wa mizozo ambapo washirika wanaweza kuwatuma wahudumu, maharusi, au familia ambazo zinapambana katika mahusiano yao. 3. Kuwatambua, Kuwafunza, na Kuwaandaa Viongozi wa Mahusiano ILM imejitolea kusaidia kanisa kukuza viongozi wa mahusiano kupitia: • Mfululizo wa Mahubiri juu ya mada za Amri Kuu ili kuwasaidia wachungaji kuwasilisha maoni ya Amri Kuu vizuri na hata pia kutambua na kuendeleza kikundi muhimu cha uongozi. • Nyenzo za kweli za kuimarisha Amri Kuu ya upendo. Kozi zote zinasaidiwa na video na zina vitabu vyenye maelezo ya kina na mwongozo wa viogozi. • Warsha za Wikendi za kuboresha mahusiano na kutekeleza huduma ya Amri Kuu katika kanisa la eneo lako kupitia warsha za ndoa, uzazi, au watu wazima waliyo peke yao.. Ikitekelezwa na Wakufunzi wa Jamii ya Maisha ya Usahibu, warsha hizi ni njia nzuri ya kuanzisha huduma ya Amri Kuu katika kanisa la eneo lako. • Mikutano ya Kuishi Amri Kuu ya kukuza kanisa na umuhimu wa huduma katika


Page 107 ulimwengu wa sasa kwa kutusaidia kujua na kumpenda Mungu kwa vile alivyo, kupitia Neno la Mungu, na kujua na kuwapenda watu kwa upendo Wake. • Mpango Unaosifiwa wa Viongozi wa Huduma ya Mahusiano —Mchakato unaosaidiwa mkondoni, uliyoundwa ili kuwaongoza viongozi wa kanisa kupitia mafunzo ya huduma ya mahusiano. Kwa wale ambao wanataka kutayarishwa vyema kuongoza huduma ya mahusiano katika makanisa yao na jamii zao. 4. Kutoa Usaidizi wa Mizozo na Mafunzo ya Ushauri/Kuhudumia Kituo cha ILM cha Huduma ya Mahusiano (CRC) hutoa tiba na usaidizi wa mahusiano yaliyo na mizozo kupitia Mandari mazito ya maharusi, familia na waliyo peke yao. Mafunzo ya washauri na wahudumu pia inatolewa kupitia semina za siku moja au mbili za Tiba ya Usahibu. Kwa habari zaidi juu ya vile wewe, au kanisa lako, huduma, dhehebu au mfumo unaweza kuwa sehemu ya Mtandao wa Amri Kuu na kuchukua fursa ya huduma na msaada unaotolewa na Huduma za Maisha ya Usahibu, andika au piga siku kwa: Great Commandment Network 2511 S. Lakeline Blvd. Cedar Park, TX 78613 800-881-8008 www.GreatCommandment.net


Click to View FlipBook Version